FUTA LAANA KWA DAMU YA YESU KRISTO KUPITIA MAOMBI HAYA.


Katika jina la YESU KRISTO,Leo naiondoa laana katika ardhi ambayo katika hiyo ardhi mimi nilitwaliwa, Kwa Jina la YESU KRISTO. BABA wa Mbinguni, ninaomba msamaha BWANA, yamkni kuna jambo nimelifanya limeleta laana kwenye uzao wa tumbo langu, naungama uovu wangu nilioufanya mimi, au walionitangulia, ndugu zangu, watawala wa nchi yangu, nami leo BWANA napitia uhairibifu kwa laana hiyo, ya nchi au ukoo wangu, naomba msamaha kwako BWANA, kwa ajili ya laana iliyoachiliwa kuja kwangu, kwenye kazi yangu, kwenye nchi yangu, naitumia Damu ya YESU, Damu ya Agano Jipya, leo initakase, inene mema kwa ajili yangu. Naivunja laana kwenye ardhi. Naitumia Damu ya YESU mwenye haki, kuvunja laana, inenayo mema kuliko damu ya Habili. Naiharibu laana, ya taifa, ya ukoo, ya wachawi, ya shetani kwa Damu ya Mwanakondoo
Mashetani wote manaoshikilia mwili wangu kwa sababu ya laana iliyotamkwa katika nchi, leo nawasambaratisha kwa Jina la YESU KRISTO. Ewe laana kwenye ardhi uliyenisababishia nisiwe na makao duniani, leo nakuvunja kwa Jina la YESU KRISTO aliye hai. Leo natoka mavumbini kwa Jina la YESU. Enyi mavumbi mniachie kwa Jina la YESU KRISTO, kwa maana mimi ni udongo lakini uliohuishwa kwa Jina la YESU KRISTO Naitegua mitego yote iliyotegwa mavumbini kwa Jina la YESU.Kwa Jina la YESU, nilikufa pamoja na KRISTO, nikaa kaburini siku zote tatu pamoja na KRISTO, nikafufuka pamoja na KRISTO siku ile ya tatu. Ndoa yangu imefufuka pamoja na KRISTO. Kazi yangu imefufuka pamoja na KRISTO. Mimi na Watoto wangu tumetoka mautini na kuingia uzimani kwa Jina la YESU KRISTO. Enyi wachawi na waganga mlionipandia balaa, magonjwa mlionipandia, leo nayango’a yote kwa Jina la YESU KRISTO. Ewe mtawala wa dunia, Lusifa na mashetani wako, nakushambulia kwa Jina la YESU KRISTO.
MUNGU BABA naomba unisaidie, kama kuna mtu aliyelia machozi ka ajili yangu naomba unikumbushe, na unipe ujasiri wa kumfuata na kumalizana naye kwa Jina la YESU.
Nimepokea ushindi mkuu kwa jina la YESU KRISTO kupitia maombi haya. Asante BWANA YESU kwa ushindi huu. Ni katika jina la YESU KRISTO nimeomba.
Amen Amen.


MUNGU akubariki sana.

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutaomba tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
0714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma na kuomba maombi haya.

Comments