IJUE HUDUMA YAKO NA ANAYETOA HUDUMA KATIKA MWILI WA KRISTO NA INAVYOTENDA KAZI. (SEHEMU II)

Na Emmanuel Kamalamo.

Bwana Yesu asifiwe!
Namshukuru Mungu kwa kunipa nafasi nyingine kuendelea na somo letu ambalo kama kanisa katika mwili wa Kristo tunapaswa kufahamu jinsi ya kumtumikia Mungu katika HUDUMA tulizo pewa.
Na ni muhimu kujua unatumika katika Huduma uliyopewa Mungu au umewekwa na watu, au kwa ajili ya Pesa? Maana maandiko yasema wazi..."KWA SABABU WALIO HIVYO HAWAMTUMIKII BWANA WETU KRISTO,BALI MATUMBO YAO WENYEWE..." Warumi 16:18.
Mwanzo tuliangalia aina za Huduma, na tukaona kuna hudama tano.
Waefeso 4:9-12.

Tukaangalia je Huduma usomewa vyuoni au kupewa ndani ya kanisa, jibu ni hapana Huduma anatoa Mungu. Waefeso 4:8-11.
Tukaanga kwenda vyuo ni sahii? Ndiyo ni sahihi ili kuweza kukusaidia namna ya kuitumia huduma. Mfano Wanafunzi wa Yesu walifundishwa na Yesu , Paulo alikaa chini ya Anania na Mitume. Mdo 9:17-28.

UTAJUAJE WEWE UNA HUDUMA IPI
AMBAYO MUNGU AMEIWEKA NDANI YAKO?

Mungu akukupa mojawapo ya Huduma tano ndani yako utakuwa na MSUKUMO/MZIGO wa kutaka kutimiza Huduma hiyo. Na kila Huduma ina utendakazi wake, huko mbele tutaziangalia.
Pia Mungu anaweza kusema na wewe kupitia UNABII kukwambia kukwambia Huduma yako.

1.UTAKUWA NA USHAWISHI WA NDANI KATIKA ROHO.
2.UTAKUWA NÀ KARAMA YA ROHO INAYOENDANA NA HIYO HUDUMA.
3.UNAPOIFANYA HUDUMA HIYO UNASIKIA AMANI NA FURAHA HATA KAMA INAUGUMU.
4.UNAVUTIWA NA KUATHIRIWA NA WATUMISHI WENYE HUDUMA KAMA YAKO.
Unapoona hali ya namna hiyo inakupasa uichochoe.Paulo anamwambia Timitheo..."USIACHE KUITUMIA KARAMA ILE ILIYOMO NDANI YAKO, KWA UNABII NÀ KWA KUWEKEWS MIKONO YA WAZEE" 1 Timotheo 4:14.
"...UICHOCHEE KARAMA YA MUNGU, ILIYO NDANI YÀKO KWA KUWEKEWA MIKONO YANGU" 2Timotheo 1:6.

Usijaribu kufanya Huduma ambayo si yako utakwama, maana huna NEEMA ya kukusudia katika Huduma hiyo...Paulo anasema..."KWA NEEMA YA MUNGU NIMEKUWA HIVI NILIVYO; NA NEEMA YAKE ILIYOKWANGU ILIKUWA SI BURE, BALI NALIZIDI SANA KUFANYA KAZI KUPITA WAO WOTE; WALA SI MIMI, BALI NI NEEMA YA MUNGU PAMOJA NAMI" 1 Wakorintho 15:10.
Wewe kama ni Mchg. usijaribu kumuweka mtu kuwa MCHUNGAJI,MTUME, MWINJILISTI
NABII AU MWALIMU kwa kumuoña kwa nje, je Mungu amekwambia? Maana Neema ya kumsaidia katika huduma hiyo haipo. Wewe unamuona Dada kila wakati anakemea DHAMBI yeye ukimpa nàfasi wote mnapigwa SALA YA TOBA Askofu mpaka Mzee wa kanisa alafu unasema..."NIMEPATA MCH.MSAIDIZI AU WA KUMFUNGULIA KANISA" Uwe na uhakika atatawanya kondoo maana hukujua anahuduma hipi ndani yake.

Ni Muhimu kuwekwa kwenye Huduma yako ndani ya kanisa ili kazi ya Mungu iende sawasawa. Ezekia aliwapanga watu sawasawa na Huduma zao. 2 Nyakati 31:2 "Ezekia akaziweka zamu za makuhani na walawi kwa zamu zao, kila mtu kwa kadri ya huduma yake.."
JE, HUDUMA TANO ZINATENDAJE
KAZI KATIKA MWILI WA KRISTO?

Fuatana nami.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA LEO BAADA
YA KUFA NI HUKUMU. Waebrania 9:27

MUNGU AKUBARIKI.

Comments