MATENDO YA MUNGU NI MAKUU NA HAYAELEZEKI.

“Basi ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya BWANA siku zote, kwakuwa, mwajua yakwamba taabu yenu siyo bure katika BWANA” 1KOR 15:58.
Shalom watu wa Mungu.
Na Godfrey Miyonjo
Atukuzwe Mungu wa wote wenye mwili milele.
Hakika hakuna neno lililo gumu ambalo laweza kumshinda Mungu.
Mimi Godfrey Mertus Mtava Miyonjo nimemwona Mungu akitenda mambo makuu katika maisha yangu.
NINAKUMBUKA ILIKUWA NI TAREHE 31/01/2012 MUDA WA SAA 4 ASUBUHI.
Ni siku ambayo niliwekewa chupa kwenye unga, ambao mimi pasipo kujua niliutumia kuandaa uji.
Siku hiyo Mungu alinitendea jambo la ajabu ambalo hakika sitakuja kulisahau katika maisaha yangu yote.
Siku hiyo hakika mimi binafsi nilijiona ni mfu, na nikawa nawaza vile mwili wangu utakavyosafirishwa kutoka Meatu Shinyanga na kupelekwa kwetu Ulanga Morogoro tayari kwa mazishi.
Niliyawaza hayo mara baada ya KUKUTANA NA VIPANDE VYA CHUPA kwenye uji niliokuwa nakunywa.
Sikuyaamini macho yangu nilipo vitema vipande viwili VYA CHUPA mezani.
Hakika haikuwa rahisi kwangu mimi Godfrey kuamini kuwa kama ingewezekana mimi kuendelea kuwa hai chini ya jua hata kwa dakika 5 baaba ya lile tukio.
Ni kweli niliomba kwa machozi nikisimamia andiko hili MARKO 16:18 lakini baada ya kumaliza maombi nikajikuta naishiwa nguvu kabisa.
Lakini ninamshukuru Mungu pomoja na kuishiwa nguvu, kupoteza matumaini ya kuishi, Yeye mwenyewe alisimama na kunitia nguvu tena na kunipa tumaini jipya.
Ninasema mwacheni Mungu aitwe Mungu kwasababu alininusuru na kifo.
Shetani alikusudia nife tarehe 31/01/2012 lakini Mungu akasimama kunipigania.
Sina cha kumlipa Mungu wangu zaidi ya kuendelea kumtumikia.
Ni maombi yangu mbele za Mungu siku zote, juu wote wenye mwili ili kila mmoja apate kumjua sana huyo Mungu aliyekamata Vipande vya chupa hata visilete madhara yoyote ndani ya tumbo langu.
Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu)

Comments