Na Mchungaji Adriano Makazi, Ufufuo na uzima Morogoro. |
Utangulizi: leo, Somo letu linaitwa “Faida za Kumtolea Bwana Fungu la Kumi”. Mungu amezungumuzia aina mbalimbali za sadaka. Zifuaatzoni aina ya hizo sadaka:
1.
AINA
ZA SADAKA KIBIBLIA
(i).
SADAKA
YA AMANI
KUTOKA
32:6….[Wakaondoka
asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi
kula na kunywa, wakaondoka wacheze. ]… Hizi ni aina ya sadaka za kusababisha amani ndani ya
nchi,familia. Ikikosekana amani mema hayawezi kukujia.
(ii).
SADAKA
YA DHAMBI.
Israeli wakitenda dhambi,
sasdaka hii hutolewa. Mnyama (ng’ombe au kondoo) huchinjwa ili kufanya dhambi za wana Israeli waachliwe
kwenye.
HESABU
6:13-14 …[Na
sheria ya Mnadhiri ni hii, zitakapotimia hizo siku za kujitenga kwake; ataletwa
mlangoni pa hema ya kukutania; 14 naye atasongeza sadaka yake kwa Bwana,
mwanakondoo mmoja mume wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka ya
kuteketezwa, na mwanakondoo mmoja mke wa mwaka wa kwanza mkamilifu, kuwa sadaka
ya dhambi, na kondoo mume mmoja mkamilifu kwa sadaka ya amani,]….
(iii).
SADAKA
YA HATIA
Mtu anakuwa ametenda mambo
yenye kumtia hatia, hata akataka kujiua. Yuda Iskariote, kwa mfano, alijisikia
ndani mwake hatia kwa kumsaliti Bwana Yesu na mwishowe akajinyonga. Wana wa
Israeli pindi wanapojisika hatia ndani ya mmioyo yaowalikuwa wanatoa sadaka ya
hatia kwa ajili yao. Cha muhimu ni
kuziacha njia zako mbaya ili hatia ndani yako isiwepo. Yapo mapepo kabisa ya
kutia hatia ndani yako. Hayo ndiyo huinon’goneza masikio yako kukuambia kwamba
dhambi uliyoifanya ni kubwa na kwamba haiwezi kusamehewa.
WALAWI
5:6-7 …[naye
atalipa kwa ajili ya hilo alilolikosa katika kitu kile kitakatifu, kisha
ataongeza na sehemu ya tano, na kumpa kuhani; naye kuhani atafanya upatanisho
kwa ajili yake kwa huyo kondoo mume wa sadaka ya hatia, naye atasamehewa.]….
Kwa hiyo aina hii ya sadaka huleta upatanisho.
(iv).
SADAKA
YA HIARI
Ni sadaka itolewayo kwa
Bwana kama hiari,ya kumshukuru Bwana kwa
mambo aliyokutendea. Haulazimiki kuitoa, ila ni kuonesha mapenzi mema kwa Bwana,
kwamba unamjali,unapenda aendelee kukuhudumia. Biblia inasema aheri kutoa kuliko kupokea.
HESABU
29:36….[lakini
mtasongeza sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kusongezwa kwa moto, harufu ya
kupendeza kwa Bwana; ng'ombe mume mmoja, na kondoo mume mmoja, na wanakondoo
waume wa mwaka wa kwanza wakamilifu saba;]…
(v).
SADAKA
YA KINYWA
KUMBUKUMBU
32:38…[Uliokula
shahamu za sadaka zao, Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji? Na waondoke na kuwasaidia ninyi; Na wawe hao
himaya yenu.]…. Baadhi ya makabila wana mila zakumwagapombe ardhini, kama
njia mojawapo ya kuwasiliana na mizimu.
2SAMWELI
23:16-17….[Basi
hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile
kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi;
walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana. 17 Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je!
Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa.
Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu.]….
(vi).
SADAKA
YA KUINULIWA
KUMBUKUMBU
12:11…[ wakati
huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua Bwana, Mungu wenu, alikalishe
jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za
kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono
yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa Bwana.]….
Mashambani yapo yale mazao ya kwanza kabisakuanza kukomaa, na waisraeli
wallikuwa wakito aina hii ya sadaka kwa Bwana (kama Malimbuko) kuwa sadaka ya
kutikiswa kwa Bwana. Maana yake, kila
kitui cha kwanza ni cha Bwana.
(vii).
SADAKA
YA KUNYWEA
Aina hii ya sadaka hufanywa na watu, wakati mwingine
akiwa mzima hakuelezi sababu yake, bali pale akienda bar na kunywa anakuwa na
ujasiri wa kuja kwako na kueleza dukuduku
zake. Nyakati nyingine anakuwepo mtu amenuna moyoni mwake kwa sababu yako. Ni vyema kukaa naye na
kuyamaliza kabla ya kutoa sadaka zako mbele za Bwana.
Yeyote aliyeninywea
mahali popopte,nageuza majeshi yamrudie mwenyewe Kwa Jina la Yesu.
EZEKIELI 20:28…[ Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile,
ambayo naliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na
kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo
la sadaka zao, na huko walifanya nukato la kupendeza, na huko walimimina sadaka
zao za kunywewa.]….
(viii).
SADAKA
YA KUSONGEZWA
WALAWI 7:30….[
mikono yake mwenyewe
itamletea hizo sadaka za kusongezwa kwa moto; mafuta yake pamoja na kidari
atayaleta, ili kwamba hicho kidari kitikiswe kuwa sadaka ya kutikiswa mbele ya
Bwana.]….
(ix).
SADAKA
YA KUTEKETEZWA
MWANZO 22:1-2…[Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia,
Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. 2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa
pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya
kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.]….
MWANZO 8:20….[Nuhu akamjengea Bwana madhabahu;
akatwaa katika kila mnyama aliye safi, na katika kila ndege aliye safi,
akavitoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu.]…
Nuhu aliitoa sadaka
ya kutekekzwa juu ya madhabahu.
2WAFALME 3:26-27….[Naye mfalme wa Moabu alipoona ya
kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga
ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. 27 Ndipo akamtwaa
mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya
kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka
kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe.]….
Vita ilimlemea Mfalme
wa Edomu na ndipo ili ashinde vita ilimlazimu kumtoa mwanae kuwa sadaka ya
kuteketezwa. Kuna watu wanatoa sadaka zao ili kuishinda vita. Hata katika
taifahili letu, wapo watu wanaowania uongozi (urais, ubunge, udiwani n.k) kwa
uchaguzi mkuu mwaka huu wakitaka
kushinda kwa kutoa aina hii ya sadaka.
(x).
SADAKA
YA KUTIKISWA
WALAWI 10:15….[Mguu wa kuinuliwa, na kidari cha kutikiswa, Watavileta pamoja na
dhabihu zisongezwazo kwa njia ya moto, za hayo mafuta ili kuvitikisa viwe
sadaka ya kutikiswa mbele za Bwana; kisha vitakuwa ni vyako wewe, na vya wanao
pamoja nawe, ni haki yenu milele, kama Bwana alivyoagiza.]…
(xi).
SADAKA
YA SHUKRANI
Ni kuonesha shukrani
mbele za Mungu.
YEREMIA 17:26…[Nao watatoka miji ya Yuda, na mahali palipo pande zote za
Yerusalemu, na nchi ya Benyamini, na Shefela, a na milima, na upande wa Negebu,
b wakileta sadaka za kuteketezwa, na dhabihu, na sadaka za unga, na ubani,
wakileta pia sadaka za shukrani, nyumbani kwa Bwana]…
(xii).
SADAKA
YA UNGA
KUTOKA 40:29…[Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani
ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama
Bwana alivyomwamuru Musa.]…
(xiii).
SADAKA
YA MALIMBUKO
HESABU 15:21
….[Malimbuko ya unga wenu
mtampa Bwana sadaka ya kuinuliwa, katika vizazi vyenu.]….
(xiv).
SADAKA
YA FUNGU LA KUMI
Ni sadaka yenye
mkataba/agano na Mungu. Na mungu ametoa maelekezo kwamba endapo mtu hatatoa
aina hii ya sadaka zipo adhabu zitakazofuatia baada ya yake.
MWANZO 14:20…[Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi
mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.]….
Hapa aina hii ya sadaka initwa fungu la kumi.
WALAWI 27:30…[ Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni
matunda ya nchi, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.]… Hapa
aina hii ya sadaka inaitwa ‘zaka’. Ni sadaka
ambayo mbele za Bwana ni ‘takatifu’, kwa
ajili ya matumizi ya kazi ya Bwana.
MWANZO 28:22…[Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya
Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.]….
Ni sadaka ambayo pia hujjulikna kama fungu la kumi.
Kawaida, mtu akila
vitakatifu vya Bwana hukumbana na adhabu. Vile uvifanyavyo vyaweza kufa,
ikiwemo mifugo, kazi n.k.
2. TARATIBU ZA UTOAJI WA FUNGU LA KUMI
Ni mpango wa Mungu wa
Kuwabariki watu waliookoka.
MITHALI 15:8…[Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa Bwana; Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.]…Dhambi
ni kikwazo cha kupata majibu kutoka kwa Bwana.
EFESO 2:8-9…[Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo
haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; 9 wala si kwa matendo, mtu
awaye yote asije akajisifu.]… Mtu hapaswi kujisifu
kwamba ameshabarikiwa, kwa sababu ni kwa neema tu. Ndiyo maana baadhi ya
watu shida haziishi miongoni mwa
waliookoka.
YOHANA 3:16…[Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa
Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.]…
Hata uzimawa milele tulio nao unatokana na utoaji wa Mungu kwa ajili yetu.
Ibrahimu alitoa
fungu la Kumi (MWANZO 14:17….[Abramu
aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye,
mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme.
18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani
wa Mungu Aliye juu sana. 19 Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu
Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. 20 Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana,
aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.]….
Mungu ana uwezo wa kuvaa mwili wa kibinadamu. Melkisededki ni mfano wa aina
yake katika Biblia. Tafsiri ya jina la huyu mfalme ndiyo inayotupa uhakika wa
kuwa Mungu alijifunua kwa namna ya kipekee.
EBRANIA 7:1-3...[Kwa maana Melkizedeki huyo, mfalme wa Salemu, kuhani wa Mungu
aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu alipokuwa akirudi katika kuwapiga hao
wafalme, akambariki; 2 ambaye Ibrahimu alimgawia sehemu ya kumi ya vitu vyote;
(tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemu, maana
yake, mfalme wa amani; 3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku
zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo
adumu kuhani milele.]…. Kawaida, tafsiri ya jina la mtu
huwa moja, na hayupo mtu wa kawaida
awezaye kuwa na jina lenye maana nyingi
zaidi ya moja.
Hata katika Agano
Jipya, watu walitoa fungu la kumi.
MATHAYO 23:23…[Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa
zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani,
adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine
msiyaache.]… Ni mpango wa Mungu kwa watu kutoa fungu la kumi.
3. KAZI YA FUNGU LA KUMI
Ni kuhakikisha kuwa nyumbani mwa Mungu pana chakula.
MALAKI 3:8-9…[Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi.
Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mmeniibia zaka na dhabihu. 9 Ninyi mmelaaniwa
kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, taifa hili lote. 10 Leteni zaka kamili
ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama
sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo
nafasi ya kutosha, au la.]… Kwa hiyo mojawapo ya
kazi ya fungu la kumi ni kuona kuwa kipo
chakula katika nyumba ya Bwana.
Chakula kwenye nyumba
ya Bwana kina maaba gani?
YOHANA 4:34…[Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. 33 Basi
wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? 34 Yesu akawaambia,
Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize
kazi yake.]… Chakula katika nyumba ya Bwana ni kufanya kanisani pasiwe
ukiwa, bali Injili ya Mungu iweze kusonga mbele.
4. FAIDA YA KUTOA FUNGU LA KUMI
Mungu atakaufunulia
madirisha ya mbinguni. MALAKI 3:10….[Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo
chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue kama
sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo
nafasi ya kutosha, au la.]...
Mungu atamkemea
ibilisi alaye biashara zetu, afya zetu, ndoa
yak n.k. (MALAKI 3:11…[ Nami kwa ajili yenu nitamkemea yeye
alaye, wala hataharibu mazao ya ardhi yenu; wala mzabibu wenu hautapukutisha
matunda yake kabla ya wakati wake katika mashamba, asema Bwana wa majeshi.])….Ibilisi
anakula. Kanuni inasema kuwa, Kama humtolei Bwana fungu la kumi, basi unamtolea
Yule alaye. Ndiyo maana, unamkuta mtu
Mataifa yatakuita
heri. MALAKI 3:12…[Na mataifa yote watawaiteni heri;
maana mtakuwa nchi ya kupendeza sana, asema Bwana wa majeshi.]…
Siyo kwamba kwa kutoa fungu la
kumi,Mungu atakupa fedha, bali atakaupa
vitu vya rohoni, mfano akili nzuri, karama, ujuzi n.k ambavyo vitawafanya
watu/mataifa kukuita heri.
5. NANI WA KUTOA FUNGU LA KUMI?
Kila mtu ana wajibu
wa kutoa fungu la kumi. 1WAFALME
17:10-14…[Basi,
akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke
mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji
kidogo chomboni nipate kunywa. 11 Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema,
Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako. 12 Naye akasema, Kama
Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na
mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie
nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe. 13 Eliya akamwambia, Usiogope; enenda
ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha
ujifanyie nafsi yako na mwanao. 14 Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema
hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata
siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.]…
Siri ya kutoa siyo kwa sababu vipo vingi, bali hata katika vidogo ni muhimu
kutoa fungu la kumi. Baraka zetu zimeambatanishwa na kutoa, tena hasa kwa watumishi wa Bwana.
6. MSINGI WA UTEKELEZAJI KATIKA KUTOA FUNGU LA KUMI
Kwa wale
wafanyabiashara, endapo umechukua mkopo wako benki kwa ajili ya bishara,
unapaswa kutoa sehemu ya kumi ya ule mkopo (mfano: mkopo wa sh.100,000 funugu
lake la kumi ni shs. 10,000 na hivyo mtaji wako utakuwa shs. 90,000). Endapo biashara hii itaongezeka kwa kutoa
faida. Mathalani mtaji na faida umefikia sh. 150,000, cha
kufanya hapo ni kuondoa ule mtaji lakini kwenye faida (sh.60,000) unapaswa
kutoa fungu la kumi ambalo ni sh. 6,000. Kawaida mtaji hautolewi fungu la kumi
kama awali ulishatolea fungu la kumi.
Mke asiye na kazi,
hapaswi kuigusa pesa ya matumizi anayoachiwa na mumewe ili iwe fungu la kumi. Kama mumewe ameshalipa
fungu la kumiyatosha. Hata hivyo, mume na mke wakiwa na kazi, kila mmoja anapaswa
kutoa fungu la kumi.
Mwanafunzi aweza
kutoa fungu la kumi la ile
pocket money apewayo na wazazi wake. Hata hivyo haipaswi kutoa fungu la
kumi la fedha ya ADA upewayo ukiwa mwanafunzi kulipa shuleni.
7. MAMBO YA KUZINGATIA
Fungu la kumi
hutolewa nyumbani mwa Bwana (Kanisani) mahali
ambapo wewe ni mshirika,
unapolelewa. Halitolewi tu kila mahali, bali pale ambapo Bwana ametuelekeza.
Halitolewi kwenye
mikutano ya Injili, wala kwa wajane wala kwa masikini na wagonjwa
8. LAANA YA KUTOTOA FUNGU LA KUMI
ZEKARIA 5:1-4…[Basi, nikainua macho yangu tena, nikaona, na tazama, gombo la
chuo lirukalo. 2 Akaniuliza, Unaona nini? Nikajibu, Naona gombo la chuo
lirukalo; na urefu wake ni dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi. 3 Ndipo
akaniambia, Hii ndiyo laana itokayo kwenda juu ya uso wa nchi yote; maana kwa
hiyo kila aibaye atatolewa kama ilivyo upande mmoja, na kwa hiyo kila aapaye
atatolewa kama ilivyo upande wa pili. 4 Nitaituma itokee, asema Bwana wa
majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwivi, na katika nyumba yake yeye
aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katikati ya nyumba yake, na
kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.]….
Haijalishi wizi unaofanyika ni wa aina gani, lakini kutotoa fungu la kumi ni
wizi kama wizi mwingine. Na adhabu ya mwiiz imeoneshwa hapa katika maandiko ya
Biblia siku ya leo.
UKIRI
Baba
Mungu naomba unisamehe, kwa kuwa nimetenda dhambi ya kutokuwa mwaminifu kwa kutotoa zaka
kamilifu, na laana imeingia katika
nyumba yangu. Leo ninakuomba Bwana unisamehe,
nilijihesabia haki kwa kuwa mimi nilikuwa sina, lakini kumbe siri na njia ya kuwa navyo vingi ni kutoa,
kwa mfano wa Yule mama mjane aliyekubali kumtengenezea Nabii Eliya mkate, na
kwa kufanya hivyo hakupungukiwa na kitu.
Ninatubu
leo dhambi ya kutokuwa mwaminifu. Nisamehe Bwana. Kuaznia leo nitakuwa natoa
zaka kwa ukamilifu wake. Ponya ndoa yangu, ponya biashara yangu kwa kuwa
imeandikwa akusamehe maovu yako yote na kukuponya magonjwa yako yote. Naomba
Bwana Yesu unisamehe katika Jina oa
Yesu. Amen
|
Comments