IMANI NI NGAO YA KUIZIMA MISHALE YENYE MOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Na Godfrey Miyonjo

“zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima michale yote yenye moto ya yule mwovu” EFESO 6:16.
BWANA YESU asifiwe sana.
Ninamshukuru Mungu kwakuwa amenipa neema ya kuyapiti baadhi ya mambo flaniflani ili nijifunze kitu kwa ajili ya kuujenga ufalme wake.
Nimejifunza vitu mbalimbali kupitia mimi mwenyewe na kutoka kwa watu wengine wasio na YESU namna ya kujikinga kwa jinsi ya dunia.
Mimi mwenyewe kabla sijaokoka niliwahi kurongwa na kutibiwa kwa mganga wa jadi.
Niliwahi kupigiwa bao na kuelezwa mambo flaniflani yanayonihusu na kunifanya niwaamini waganga wa jadi (wachawi) kuwa ni watu waliowekwa na Mungu ili kuwasaidia wanadamu.
Lakini ashukuriwe Mungu aliyenipa neema ya kujua kuwa hao watu (waganga wa jadi/wachawi) siyo watumishi wa Mungu bali ni watumishi wa shetani.
Ashukuriwe Mungu kwa Kunifundisha kuwa kinga dhidi ya wachawi siyo hirizi wala kuchanjwa chale wala kupewa kitu kingine kiwachochote bali kinga ni kumwamini YESU (kuwa na imani).
Ninamshukuru Mungu kwakuwa kwa neema yake tu mimi nilitoka huko,
Sikuwahi kutenda jambo jema lolote ambalo naweza kusema ndilo lilimfurahisha Mungu hata akaamua kunitoa huko.
Bali ni kwa neema ya Mungu (upendeleo) tu nimetoka huko,
Mimi nimetoka huko na wengine bado wapo hukohuko wakiendelea kuchanjwa chale, wakipewa hirizi, N.K kwa ajili ya kujilinda.
Na wengine ni waumini wazuri wa dini lakini kwakuwa hawana imani ya kweli wameendelea kuwa watumwa wa mambo hayo.
Wamekosa kujua kuwa Biblia inasema kuwa kupitia imani tunaweza kuizuia mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
Wamekosa kujua kuwa magonjwa na shida zote wanazopitia zinasabzbishwa na mishale ya moto ya Yule mwovu.
Kwakuwa nimepata hii neema name ninawaambia wote wasiyojua kuwa Kupitia imani ya kweli tunaweza kujikinga hata tukawa salama.
Imani hiyo siyo nyingine bali ni hii itokanayo na kumkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni BWANA nakuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu. RUMI 10:9.
Ukiwa na imani hiyo hakika utakuwa na ngao ambayo itakuwezesha kuizima mishale yenye moto (ya shetani) katika ulimwengu wa roho.
Ukiwa na hii imani hata kama wachawi wote wa duniani watajipanga ili wakuangamize hakika hawataweza, na mwisho wa siku wataangamia wao kama wasipotubu.
Ewe rafiki yangu uliyeusoma ujumbe huu
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
CHUKUA LEO NGAO YA IMANI ILI UWEZE KUIZIMA MISHALE YA MOTO YA MWOVU KATIKA ULIMWENGU WA ROHO.

Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu

Comments