PANA MAPATANO GANI KATI YA HEKALU LA MUNGU NA SANAMU?

Na Peter M Mabula,  Maisha ya ushindi Ministry.


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze neno la uzima.
Pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu?
Sanamu ni ya nini katika hekalu la MUNGU?
MUNGU hataki sanamu katika hekalu lake, kwanini wanadamu wanang'ang'ania sanamu wakati BWANA hataki?
2 Kor 6:15-18 ''   Tena pana ulinganifu gani kati ya KRISTO na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la MUNGU na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la MUNGU aliye hai; kama MUNGU alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa MUNGU wao, nao watakuwa watu wangu.Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema BWANA, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha. Nitakuwa BABA kwenu, Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,   ''
-Kuna upande wa MUNGU na upande wa shetani.
=Upande wa MUNGU kuna KRISTO na upande wa shetani kuna beliari yaani  ufisadi.
=Kuna anayemwamini YESU na kuna ambaye hamwamini MUNGU.
=Kuna Hekalu la MUNGU na kuna sanamu ambayo iko upande wa shetani.
MUNGU hataki tuwe upande wa shetani.
Sanamu iko upande wa shetani.
Sanamu lazima iondolewe katika hekalu la MUNGU.
Hekalu ya MUNGU ni kanisa pahali wanamwabudu MUNGU Pia Hekalu ni wewe mteule wa KRISTO.
-Wewe kama hekalu la MUNGU hutakiwi kuwa na sanamu moyoni mwako, hutakiwi kuabudu sanamu, hutakiwi kuisujudia sanamu wala kutegemea msaada wowote kutoka kwa sanamu.

Isaya 42:8 ''  Mimi ni BWANA; ndilo jina langu; na utukufu wangu sitampa mwingine, wala sitawapa sanamu sifa zangu. ''
-BWANA MUNGU anasema hatawapa sanamu sifa zake, kawnini wewe sifa ya MUNGU na heshima ya MUNGU unaipa sanamu?
-MUNGU hataki heshima yake au sifa yake uipe sanamu.

BWANA anachukia sana kwa sisi wanadamu aliotuumba, kuanza kuabudu sanamu au kuitegemea kwa lolote.
Hata kuiheshimu tu sanamu ni dhambi, sanamu ya nini? haifai na haihitajiki katika hekalu la MUNGU.
Ona mfano huu.

2 Wafalme 17:12-16 '' wakatumikia sanamu, ambazo BWANA aliwakataza, akasema, Msitende jambo hili. Pamoja na hayo BWANA aliwashuhudia Israeli, na Yuda, kwa kinywa cha kila nabii, na cha kila mwonaji, akisema, Geukeni, na kuziacha njia zenu mbaya, mkazishike amri zangu na hukumu zangu, sawasawa na ile sheria yote niliyowaamuru baba zenu, nikawapelekea kwa kinywa cha manabii watumishi wangu. Walakini hawakutaka kusikia, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, kama shingo za baba zao, wasiomwamini BWANA, MUNGU wao. Wakazikataa sheria zake, na agano lake, alilolifanya na baba zao; na shuhuda zake alizowashuhudia; wakafuata ubatili, wakawa ubatili, nao wakaandamana na mataifa waliowazunguka, ambao BWANA alikuwa amewaagiza, wasitende kwa mfano wao. Wakaziacha amri zote za BWANA, Mungu wao, wakajifanyizia sanamu za kusubu, yaani, ndama mbili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali. ''
-Hawa ni watu ambao walianza kuabudu sanamu.
-Walimwacha MUNGU na kuambatana na sanamu.
-kwa neema yake BWANA alikuwa anawatuma watumishi wake ili kuwaonya watu hawa kama vile ambavyo leo BWANA anatuma watumishi kila kukicha ili kuwaonya kanisa kujitenga na sanamu. Israeli hawakuwasikiliza watumishi wa MUNGU waliotumwa kwao kama ambavyo leo wanavyokataa maonyo ya MUNGU.
Isaya 2:18 '' Nazo sanamu zitatoweka kabisa.  ''

Sanamu ni machukizo makuu.
Hata kuabudu wanadamu ni machukizo, hapo juu tumeona kwamba waisraeli walianza kuliabudu jesho la mbinguni yaani walianza kuabudu malaika, hayo ni machukizo makuu. Sasa kama kuabudu malaika ni dhambi kuu je kuabudu wanadamu itakuwa sio dhambi? Ni dhambi ndugu.
Waliompokea YESU kama BWANA na MWOKOZI wao lazima wajitenge mbali na sanamu.
Watakatifu wa zamani walijitenga mbali na sanamu, ona mfano huu wa wateule waliojitenga na sanamu.
1Thesalonike 1:9-10 '' Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia MUNGU mkaziacha sanamu, ili kumtumikia MUNGU aliye hai, wa kweli; na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni YESU, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.  ''
Naamini kuna kitu umejifunza na utajitenga na sanamu. Hutampa sanamu heshima ya MUNGU wala hutatumia sanamu katika maombi wala ibada yako.
1 Kor 10:14 '' Kwa ajili ya hayo, wapenzi wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.  ''

Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine.na kama hujampokea BWANA YESU muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako
Peter M Mabula
Maisha ya Ushindi Ministry.
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments