MLANGO WA MBINGUNI UKO WAZI SASA, INGIA MAPEMA MAANA MLANGO UKIFUNGWA HUTAWEZA KUINGIA.

Na Mtumishi wa MUNGU, Peter Mabula.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze ujumbe wa uzima.
Leo nazungumzia Mlango wa mbinguni.
Mlango ni  nafasi maalumu iliyo ukutani  ili kuingia au kutokea. Hiyo ni maana ya mlango kwa ujumla wake lakini upo  Mlango wa mbinguni, huo ndio ninaouzungumzia leo .

Yohana 10:7,9,11,14 ''Basi YESU aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.   Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; ''
-BWANA YESU ndio mlango wa mbinguni, mlango wa mbinguni ndio mlango wa uzima wa milele maana yake hakuna mtu hata mmoja anaweza kuingia uzima wa milele pasipo kupitia kwa BWANA YESU. Biblia inathibitisha Neno hilo kwamba  '' Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.-Matendo 4:12'' na BWANA YESU anaendelea kuthibitisha kwamba tukitaka uzima basi tumpokee yeye na kuanza kuishi maisha mataktifu katika yeye, BWANA YESU anasema ''  Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.-Yohana 14:6 '' na ndio maana ukweli ni kwamba '' kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la BWANA ataokoka.- Warumi 10:13''

-Lango La Mbinguni Liko Kabisa Ili Wanadamu Waingie Na Kupata Uzima. Lango La Mbinguni Ni BWANA YESU. Yeye Ndie Mlango Wa Sisi Kondoo Kupita Na Kwenda Uzimani. Kama Lango La Mbinguni Limefunguliwa Leo Basi Ipo Siku Litafungwa. Ndugu, Lango Likifungwa Utakuwa Ndani Au Nje?. 
-Kumpokea BWANA YESU Leo Ndio Kufunguliwa Mlango Wa Uzima Ili Wewe Uingie. 
-Jitahidi Kuingia Ndugu Kabla Lango Halijafungwa. Siku Likifungwa Halitafunguliwa. 
-Wokovu Ni Sasa Tena Sasahivi. Wokovu Ni Leo Wala Sio Kesho. -Wokovu Una BWANA YESU Pekee. 
Zaburi 3:8 '' Wokovu una BWANA; Baraka yako na iwe juu ya watu wako.   ''
-Wokovu Ni Mpango Wa MUNGU Kumtafuta Mwanadamu Ila Mwanadamu Huyo Awe Kwenye Milki Yake MUNGU Kwa ajili ya Uzima Wa Sasa Na Kwa Uzima Wa Milele. 
-YESU Anakuita Leo, Anakusubiri Tu Kutubu Kwako Na Kumpokea. 
-Siku Ya BWANA I Karibu. Leo Yako Ndio Itakayotoa Matokeo Ya Kesho Yako Iweje. Leo Ina Faida Kuliko Jana Kama Tu Leo Yako Ukiitumia Vizuri Kwa Kuamua Vyema. Jitahidi Ndugu Kuamua Vyema kwa kumpokea BWANA YESU. Ndugu ingia katika BWANA YESU kabila mlango haujafungwa maana siku ukifungwa hautafunguliwa. Kutubu ni leo wala sio kesho. hakuna kutubu baada ya kufa. kutubu ukiwa kuzimu haiwezi kumsaidia mwanadamu. kutubu ni hapa hapa duniani.

1 Yohana 1:9 ''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote''

- Inawezekana Kabisa Ukimwi Ni Hatari Sana Lakini Ukweli Ni Kwamba Jehanamu Ni Hatari Kuliko Ukimwi. 
-Japokuwa Ebola Ni Hatari Sana Lakini Ziwa La Moto Ni Hatari Kuliko Ebola. Ndugu Zangu, Ni Saa Ya Kuamka Kutoka Kwenye Usingizi Wa Dhambi Kwa Kuokoka. Ukibaki Kwenye Usingizi Wa Dhambi Unaweza Kuamka Ukiwa Ziwa La Fire. Ni Hatari Sana Ndio Maana Kila iitwapo Leo Tunahubiri Habari Moja Tu Kwamba Watu Wampokee BWANA YESU Na Kuanza Kuishi Maisha Matakatifu Ya Wokovu. MWENYE SIKIO LA KUSIKIA NA ASIKIE.
Luka 24:46-48 '' Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba KRISTO atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. '' 
-Mataifa yote watahubiriwa toba na ondoleo la dhambi kupitia jina la YESU KRISTO.
-Unayehubiri pia unatakiwa kuwa mtakatifu na unamtii KRISTO.
 -Sio Wote Wamwitao BWANA BWANA Watakaoingia Paradiso. Huwezi Kugeuza Kanisa Kama Kichaka Chako Cha Kuficha Dhambi Zako Za Usiku Harafu Ukasema Unaenda Mbinguni Wakati Hata Hujawahi Kutubu Toba Ya Kweli. Biblia Inatuonya Kwamba Alitajaye Jina La BWANA YESU Na Aache Uovu. MWENYE SIKIO LA KUSIKIA NA ASIKIE LEO.
2 Timotheo 2:19 '' Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, BWANA awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la BWANA na auache uovu. ''

 -Kuna Watu Hujidanganya Kwamba Hakuna Jehanamu Ya Moto. Ndugu Anayekuhubiri Hivyo Ni Wakili Wa Shetani Wala Sio Wa MUNGU. 
-Kuna Watu Husema Kwamba MUNGU Ni Wa Rehema Sana Hivyo Hawezi Kuwaangamiza Wanadamu. Ndugu Anayekuhubiri Hivyo Ni Wakala Wa Shetani Wala Sio Wa MUNGU. 
Matukio Ya Gharika Ya Nuhu Au Sodoma Na Gomora Yakupe Ufahamu Kwamba MUNGU Huwa Anaweza Kuangamiza Waasi. -Kuna Watu Huwaombea Wafu Wakijidanganya Kwamba Watawabadilishia Makazi Marehemu Hao. Ndugu Anayekuhubiri Hivyo Hajui Hata Moja Alitendalo. 

''sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? .......(Waebrania 2:3)''

-Kumbe Kuna Wokovu Mkuu, Ni Wakati Wa Kuufuata Wokovu Mkuu. Wokovu Mkuu Una BWANA YESU Pekee(Matendo 4:12). -Ndugu Zangu, Huu Ni Wakati Wa Kuufuata Wokovu Wa BWANA YESU. Wokovu Ni Leo Wala Sio Kesho. MWENYE SIKIO LA KUSIKIA NA ASIKIE LEO. 

-Ndugu,Naamini umejifunza na utachukua hatua njema ya kumpokea BWANA YESU kama hujaokoka ili awe BWANA na MWOKOZI wako tangu leo na utaanza kuishi maisha matakatifu

KAMA UNATAKA KUTUBU RUDIA MANENO HAYA KISHA TAFUTA KANISA LA KIROHO UKAJIUNGE NA KUANZA KUISHI MAISHA MATAKATIFU.

''BABA katika jina la YESU KRISTO Niko mbele zako mimi mwenye dhambi, lakini leo nimetambua kosa langu na naomba unisamehe dhambi zangu zote, nisamehe dhambi ninazozikumbuka na pia zile ambazo sizikumbuki. futa jina langu katika kitabu cha hukumu na uliandike jina langu katika kitabu cha uzima. Neno lako katika Warumi sura ya 10 Mstari wa 9 na wa 10 Neno lako linasema ''Kwa sababu, ukimkiri YESU kwa kinywa chako ya kuwa ni BWANA, na kuamini moyoni mwako ya kuwa MUNGU alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu '' . BWANA YESU mimi nimekuamini leo na hivyo naamini sasa napokea wokovu wako na hakika nimeokoka. Kuanzia leo Naufunga ukurasa wa dhambi na ninaufungua ukurasa wa matendo mema na matakatifu. BWANA nipe ROHO wako Mtakatifu ili aniwezeshe kushinda dhambi na anasa zote za dunia. Kuanzia leo mimi nimeokoka na ni mtoto wa MUNGU mwenye haki zote. ninafuta laana zote na kila roho ya shetani inayonifuatilia naiharibu kwa jina la YESU KRISTO kama neno la MUNGU linavyosema katika Yeremia sura ya kwanza mstari wa 10. BWANA YESU nakushukuru sana kwa kuniokoa. Yote haya kwa imani nimepokea na niko tayari sasa kwa ROHO MTAKATIFU kunitumia. Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea .
Amen.''

Kama umetubu toba ya kweli hakika wewe kuanzia sasa ni mshindi na ni shujaa. Kwa sasa naishia hapo, MUNGU akitupa nafasi tutajifunza tena siku nyingine. ulishindwa kumpokea BWANA YESU nafasi yako bado ipo na muda wa kumpokea ni leo wala sio kesho, amua leo na atakuandika jina lako katika kitabu cha uzima na utaanza kuukulia wokovu kwa mafundisho kanisani. MUNGU ana makusudi kabisa na wewe, hataki upotelee motoni anataka uende uzimani aliko KRISTO BWANA.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula
+255714252292
mabula1986@gmail.com
MUNGU akubariki sana uliyesoma somo hili.

Comments