KATIKA JINA LA YESU KRISTO ALIYE HAI.


Kila nilichokamata kwenye mikono yangu halafu kikanifunga nakataa kwa Jina la YESU KRISTO. maneno yoyote mabaya yaliyotamkwa leo kwa ajili yangu nayafuta kwa Jina la YESU KRISTO. Ninauteka ulimwengu wa roho kwa Jina la YESU.
Yeyote adui aliyekamata baraka yangu,leo achia kwa Jina la YESU KRISTO. Naziapisha mamlaka zote za kuzimu, kwenye ulimwengu wa roho, yeyote aliyekamata baraka zangu,leo aniachie kwa Jina la YESU KRISTO.
Ewe shetani uliyeweka kambi ofisini kwangu, achia kwa Jina la YESU KRISTO. Ewe adui uliyeweka kambi kwa familia yangu, achia kwa Jina la YESU KRISTO. Mahali popote nilipokamatwa ili nisiende kwangu, na jambo lolote lilinikamata nalikataaa leo kwa Jina la YESU KRISTO. Kuanzia leo natoka kwenye ngome yako adui, natoka kwenye dhiki yako, Kwa Jina la YESU KRISTO. Ninaamuru utawala wa BWANA YESU uwe dhahiri, kwa nguvu ya Damu ya YESU KRISTO ya kuteka nyara iwe dhahiri kwa Jina la YESU.
Leo sitanyamaza, katika Jina la YESU. Chochote kilichowekwa mbele yangu ili ninyamaze, leo sitanyamaza kwa Damu ya YESU.
Ngome yoyote iliyopewa jina ili kunizuia nisipate vyangu niachie kwa Jina la YESU KRISTO. Achia leo kwa Jina la YESU. Yeyote adui unayekuja ili uninyamazishe, leo uniachie kwa damu ya YESU KRISTO. Kuanzia leo, na kuanzia sasa roho yoyote iliyotumwa kwangu ili kuninyamazisha leo naikataa kwa Damu ya YESU KRISTO. Kuanzia leo sitanyamaza katika haki yangu nzuri. Achia maisha yangu, leo nakataa kunyamaza katika Jina la YESU KRISTO.
Leo nauondoa utulivu wowote wa kishetani, uliowekwa ili mimi ninaswe, Leo nauondoa kwa Jina la YESU KRISTO. Ninakataa leo, utulivu wowote aliouweka adui yangu ili anase maisha yangu, niachie leo kwa Jina laYESU KRISTO.
Nakataa kwa Jina la YESU, ewe shimo uliyeandaliwa ili kuyakamata maisha yangu, ninakataa kwa Jina la YESU. Kila gereza lililoandaliwa ili kushika uzao wangu leo nakuagiza unikatae kunishikilia, na uniachie kwa JIna la YESU KRISTO.
Kuanzia leo, nakuanzia sasa, enyi watu waovu mliojipanga kuotea maisha yangu, leo ninawapiga kwa Damu ya YESU KRISTO. Mahali popote ambapo iblisi ametegea mitego ili kuyanasa maisha yangu, nakataa kwa Jina la YESU KRISTO.
Kwa Damu yaYESU, kuanzia leo, na kuanzia sasa, yeyote anayewinda roho yangu aniachie, kila roho iliyo ndani yangu au nje yangu leo niachie kwa Jina la YESU. Ewe mwindaji unayewinda roho yangu, leo niachie kwa Damu ya YESU KRISTO. Ninaikata kila kamba ya mtego iliyonifunga, Uliyetumwa ukae ndani yangu ili uniwinde, leo kwa Jina la YESU KRISTO achia, kwa Jina la YESU.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea.
Amen AMen.
KATIKA JINA LA YESU KRISTO IMEKUA.
AMEN AMEN.

Comments