NI VIZURI KUMHESHIMU MCHUNGAJI WAKO.

Peter Mabula nikiwa na Mchungaji wangu Elly Botto.


BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Nakukaribisha kujifunza Neno la MUNGU.
Leo nazungumzia baba zetu wa kiroho na umuhimu wao.
Baba zetu wa kiroho wanaweza kuwa wachungaji, mitume, manabii, walimu au wainjilisti ilimradi tu wanaongoza makanisa yao ambayo MUNGU amewaweka kuongoza.
Wachungaji hawa wana agizo la MUNGU la kutuchunga sisi.

Matendo 20:28 '' Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo ROHO MTAKATIFU amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake MUNGU, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.'' 

Kila Mkristo ana baba yake wa kiroho.
Baba wa kiroho ndiye yule ambaye MUNGU humpa neno kwa ajili yako kila wiki na kukufundisha kanisani kwenu.
Kuna wakati watumishi hawa huchukua muda mrefu sana kuombea ujumbe ili ujumbe huo utusaidie.
Kama baba wa kimwili alivyo na umuhimu kwako, vile vile baba yako wa kiroho ana umuhimu sana kwako.
Kumheshimu baba yako wa kiroho ni jambo jema kabisa mbele za MUNGU.
Kama Hutamheshimu Wewe Baba Yako Wa Kiroho, Hawezi Kuheshimiwa Nje Ya Kanisa. 
Kama utamsema vibaya mchungaji wako huko nje ya kanisa, hiyo itakuwa ni hasara kwa kanisa zima.
1 Petro 2:13 '' Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya BWANA; ikiwa ni mfalme, kama mwenye cheo kikubwa; ikiwa ni wakubwa, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.''
 
Mnaweka mkabaki waumini 10 kanisani kwenu miaka nenda rudi na hamjui tatizo ni nini.
Kumbe tatizo ni nyie waumini kuwa na ushuhuda mbaya juu ya baba yenu wa kiroho hata watu hawawezi kuja kanisani kwenu, maana kwa maneno yenu pataonyesha kabisa kwamba hapafai, japokua nyie waumini ndio hamfai na sio mchungaji.
Ulishawahi kujiuliza swali hili?
''Mchungaji amewekwa na MUNGU ili awe mchungaji wako, na huyo mchungaji yuko sahihi kabisa mbele za MUNGU, Je MUNGU anakutazamaje wewe unayepotosha?''

Waefeso 4:11-12 ''
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa KRISTO ujengwe;''
MUNGU alitoa watu ili wawe wachungaji na hiyo ni kazi MUNGU aliwapa.
Kipindi mimi Peter Mabula naokoka kule Zanzibar, mchungaji wangu alikuwa kwenye mazingira magumu sana. Alikuwa ana kazi yake lakini MUNGU akamwambia aache kazi ili akamtumikie, alikuwa na ujuzi mzuri ambao ungempa kazi nzuri lakini bado agizo la MUNGU lilikuwa kwenda kumtumikia. aliendelea na uchungaji lakini ilifika kipindi alitamani kufanya kazi nyingine pia huku na uchungaji akiendelea nao, hali kiuchumi ilikuwa sio nzuri. Alipoanza kufanya kazi tu nje na uchungaji, MUNGU alimpiga na aliacha kazi ile huku akilia. Agizo la MUNGU lilikuwa ni akatumike katika nafasi ya uchungaji tu basi.
Najua wako wachungaji wa aina hiyo wengi tu ambao MUNGU amewaachisha kazi ili wamtumikie. Na MUNGU anawaandalia waumini ambao ndio watakuwa na wajibu wa kuwatunza wachungaji hao kiuchumi, na MUNGU atawabariki waumini hao kwa kujitoa kwako ili wamhudumie mchungaji wao. Lakini katika makanisa mengi haiko hivyo na kuwaacha wachungaji wakiteseka tu. 
Mchungaji Ndio Nabii Mkubwa Kanisani, Sisi Wengine Hata Kama Tuna Upako Kumzidi Lakini Bado Sisi Ni Manabii Wadogo Na Yeye Ni Nabii Mkubwa. 
Hakikisha Unakua Baraka Kwa Nabii Wako. 
MUNGU Anataka Uwajibike Kwa Nabii wako, Lakini Awe Mchungaji Anayeihubiri Kweli Ya KRISTO.
Kama Anaagiza Yanayokataliwa Na Biblia Mkatalie, Usiwe Na Nidhamu Ya Woga Bali Nidhamu Ya Sahihi Kwanza Kwa MUNGU Kisha Wanadamu. 
KRISTO Kwanza Kisha Mengine. 
1 Petro 2:17-18 '' Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni MUNGU. Mpeni heshima mfalme. Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wao walio wema na wenye upole tu, bali nao walio wakali.''
 
Ngoja nikuambie kitu hiki muhimu.
Na Mtu Asipoheshimu Jina Lake Mwenyewe Hawezi Kuheshimiwa. 
Jiheshimu Kwanza Mwenyewe Kisha Utaheshimiwa. 
Kuwaogopa Wanadamu Huleta Mtego Bali Amchaye BWANA Ataheshimiwa.
Usipomheshimu mchungaji usitarajie watu wa nje kumuheshimu.
Mtii MUNGU na neno lake na Neno la MUNGU linatutaka pia kuwaheshimu watu wakiwepo baba zetu wa kiroho.

  ''Kila Neno La MUNGU Limehakikishwa; Yeye Ni Ngao Yao Wamwaminio. Usiongeze Neno Katika Maneno Yake; Asije Akakulaumu, Ukaonekana U Mwongo-Mithali 30:6-7.


Leo kuna baadhi ya viongozi kanisani unakuta ndio wanaofanya kampeni za kuzuia waumini kutoa fungu la kumi na sadaka, hiyo ni laana yenye uzito wa juu sana.
Leo Kuna watumishi hutafuta madhabahu za mitandaoni na kufundisha watu wasitoe zaka makanisani kwao, Kuna watumishi hutamani waachiwe madhabahu kanisani ili wawafundishe kanisa  kuacha kutoa zaka kwa sababu tu wao hawanufaiki na zaka hizo au sadaka hizo.  
MUNGU alimchagua mama wa Sarepta kumlisha Eliya nabii.
1 Wafalme 17:9 ''Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.'' 
-Hata leo MUNGU amewaamuru kanisa kuwasaidia wachungaji wao vitu vya mwilini ili awachungaji wawasaidie kanisa vitu vya rohoni.
-Kupitia zaka yako na sadaka hapo utakuwa unasaidia kazi ya MUNGU kwenda mbele zaidi.
Kama Mchungaji hatakuwa na chakula nyumbani kwake, nakuhakikisha sahau kuhusu kukuombea ili ndoa yako iliyokufa irejeshwe upya, bali wakati huo atakuwa busy kuombea kupata chakula katika familia yake.
Kama vijana hamumtunzi mchungaji wenu na kila siku kwake ni njaa tu, msitarajie aombe ili mfunguliwe kwenye vifungo vya kutokuolewa au kuoa maana atakuwa busy na yeye kulia mble za MUNGU kwa ajili ya familia yake.
MUNGU ana sababu sana kukuweka wewe katika kanisa, ili uwe baraka hata kwa mchungaji wako. 
Mchungaji mmoja  baada ya siku kadhaa bila chakula nyumbani kwake, na mpaka mkewe amemkimbia na watoto wanalia tu ndani maana hakuna chakula, huku waumini wake wanakatisha tu mitaani na magari alisema neno hili

  ''Ukinibariki Mimi, Kuna Watu Wengine Watakubariki, Ukinilaani Mimi, Watu Wengine Watakulaani Na Wewe. Tenda Yale Unayopenda Wewe Utendewe.''

Ndugu yangu, nakuomba sana kuhusika na mchungaji wako, msaidie na mtunze maana ni wajibu wako.
Sio kwamba MUNGU hawezi kumtunza ila MUNGU amekuandaa wewe kumtunza na wewe MUNGU atakubarikia sana.
MUNGU alishawahi kutuma kunguru kumlisha Mtumishi wake, unadhani anashinda kumsaidia?
 1 Wafalme 17:2-4 ''Neno la BWANA likamjia, kusema, Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. ''
BWANA alikuwa amewaamuru kungura kumlisha mtumishi wake.
Je atashindwa kukutumia wewe mwanadamu kwa ajili ya mtumishi wake?
Unapomsaidia mchungaji wako naomba utambue kwamba humsaidii kwa sababu yeye ni masikini bali ni wajibu wako na agizo la MUNGU kwako. 

 Ukifanya Kazi Ya MUNGU Kama Ya MUNGU Haitakusumbua Lakini Ukifanya Kazi Ya MUNGU Kama Ya Kwako Itakusumbua Sana, Kila Kitu Utaona Kigumu
BWANA YESU anasema juu ya watumishi wake.

 ''Awapokeaye ninyi, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi, ampokea yeye aliyenituma.Ampokeaye nabii kwa kuwa ni nabii, atapata thawabu ya nabii; naye ampokeaye mwenye haki kwa kuwa ni mwenye haki, atapata thawabu ya mwenye haki.Na mtu awaye yote atakayemnywesha mmojawapo wa wadogo hawa ngaa kikombe cha maji ya baridi, kwa kuwa ni mwanafunzi, amin, nawaambia, haitampotea kamwe thawabu yake. -Mathayo 10:40-42.''
Kuna faida kubwa katika kusaidia injili isonge mbele.
Kuna faida kubwa katika kuwasaidia watumishi wanaojitoa kwa ajili yako ili ujue kweli ya MUNGU.
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com

Peter Mabula.

Comments