NI KWELI UMEPATA, LAKINI JE! UMEPATAJE?

Na Godfrey Miyonjo.

BWANA YESU asifiwe wapendwa,
Kwa Neema Ya Mungu nimepata kibari kwa mara nyingine kuandaa ujumbe huu;
Niseme tu atukuzwe Mungu aliyenipa kibari tena siku ya leo, kwakuwa uweza, na nguvu na utukufu na mamlaka zina yeye milele na milele amina,
Huu ndiyo wakati sahihi kwa watu sahihi kujifunza jambo sahihi, mahala sahihi,
Karibu ewe ndugu katika ujumbea huu usemao “NI KWELI UMEPATA, LAKINI JE! UMEPATAJE?”
Ninakukaribisha kwakuwa imeandikwa “Lakini mwonyane kila siku, maadamu iitwapo leo, ili mmojawenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi” WAEBRANIA 3:13.
Ninataka kusema na mtu aliyepata kitu/vitu na kukifurahia/kuvifurahia,
Ni jambo la furaha sana kwa mwanadamu kupata kile alichokuwa anakitaka/anakihitaji.
Ni ukweli kuwa Wanadamu wote hutumia akili zetu ili kufikia malengo yetu,
Likini wakati tunatumia akili zetu ili kufikia malengo yetu ni vizuri tukumbuke kuwa imendikwa,
“Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi, kwa maana wengi hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedhaheshe.” 1KOR 15:34.

Pamoja na Mungu kuturuhusu kutumia akili zetu, Yeye hakuturuhusu kufanya hovyohovyo, anatutaka tutumie akili zetu kama ipasavyo.
Mungu anatutaka Katika harakati zetu za kufikia malengo yetu tutumie njia mbalimbali lakini tuhakikishe kuwa hatutendi dhambi.
Na tukifanikiwa wanadamu ni ruksa Kwetu kujisifu au kusifiwa, kujipongeza au kupongezwa,
Pamoja na uhuru huu tulionao Lakini mimi sitajipongeza katika uovu, wala sitampongeza mwanadamu yeyote, aliyepata kitu/vitu chochote/vyovyote pasipo kujua kuwa amekipataje/amevipataje.
Na nipo hapa leo kupitia ujumbe huu ili kumwuliza kila mwanadamu;
Weweuliyepata chochote, “NI KWELI UMEPATA, LAKINI JE! UMEPATAJE?”
Wewe uitwae mtume, huo utume wako umeupataje?
Wewe uitwae mchungaji, huo uchungaji wako umeupataje?
Wewe uliye na upako, huo upako wako umeupataje?
Wewe uitwae nabii, huo unabii wako umeupataje?
Wewe uitwae Rais/Mfalme huo urais/ufalme wako umeupataje?
Wewe uliye mbunge, huo ubungewako umeupataje?
Wewe uliye askari, huo uaskari umeupataje?
Wewe uliye na mali hizo mali zako umezipataje?
Wewe uliye na mke/mume huyo mke/mume umempataje?
Wewe uliye na cheti kizuri (chenye matokeo mazuri) hicho cheti umekipataje?
Wewe uliyepata mtoto, huyo mtoto umempataje?
Wewe uliye na kazi nzuri, hiyo kazi umeipataje?
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,
SIWEZI KUKUPONGEZA HADI PALE NITAKAPOUJUA UKWELI,
Kwa maana chini ya jua siyo kila aliyepata kitu anapaswa kupongezwa,
Kwa maana kuna wachungaji, lakini huo uchungaji wao wameupata kwa hila,
Kuna mitume waliopata utume kwa njia za kishetani,
Kuna wenye upako, waliopokea huo upako kutoka katika ufalme wa giza,
Kuna wenye watoto, lakini hao watoto wamewapata kwa kuwasaliti wenzi wao,
Kuna waliooa/walioolewa lakini wameoa/wameolewa mahala pasipo sahihi, wamevunja ndoa za watu ndipo wakaoa/wakaolewa wao,
Kuna Marais/Wafalme walioupata huo urais/ufalme kwa njia zisizokuwa za halali,
Kuna walio na mali lakini mali hizo wamezipata kwa njia za ufisadi, wizi, unyang’anyi, N.K
Kuna wenye kazi nzuri lakini hizo kazi wamezipata kwa kutoa rushwa,
Kuna wenye vyeti vizuri (vyenye matokeo mazuri) lakini hivyo vyeti wamevipata kwa njia ya kufanya udanyifu katika mitihani,
Kuna wenye magari mazuri lakini hayo magari wamehongwa na mahawara zao,
NAMI KWA MAMLAKA NILIYOPEWA NA MUNGU NINAWATAKA WATU WATENDAO MAMBO HAYO, NA MENGINE YAFANANAYO NA HAYA WATU LEO.
Ni mimi Mtumishi wa Kristo Yesu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa milki ya Mungu)
WhatsApp 0757649495.
Email godfreymiyonjo@yahoo.com or gmlokole1@gmail.com

Comments