USHUHUDA WA MATENDO MAKUU YA MUNGU YA ULINZI KWANGU.

Na Mtumishi Samwel Kibiriti

Shalom watumishi wa Kristo Yesu naomba niwashirikishe huu ushuhuda.
Jana nimeingia huku Mafinga Iringa kuna familia ambayo wameniita na hii ni mara ya pili kuja ndani ya mwezi mmoja na nusu hapa kuisaidia hii familia kutokana na mateso na vifo walivyopitia miaka mingi.

Sasa wakati nikiwa Arusha Ngorongoro kwenye huduma za semina naza wanafunzi Roho Mtakatifu alinionyesha hapa nyumbani kwenye hii familia kuna binti mfanyakazi za ndani ni mchawi nami nikafanya nae maombi kwa njia ya simu ndipo roho ya uchawi ikadhihirika. Nikawaambia kuwa huyo binti amebeba siri kubwa na wakimbana ataongea nakweli akaanza kuwaeleza mambo mengi sana sana yanayohusiana na matatizo ya familia na vifo vilivyotokea.

Sasa ndipo jana Mungu akanipa kibali nije kushughulikia mambo furani na kuzidi kuifungua hii familia. Kwa kweli safari ya jana ijumaa ilikuwa na vita sana kwenye usafiri ila nawashukuru sana kwa maombi yenu

Sasa Mungu alifunua mtu anayetesa familia hii kuwa ni mama mdogo na jana nilipoingia ucku alikuja kwa lengo la kuniona kwani kumbe ucku wa ijumaa walinitegeshea dawa za kichawi njiani ili nife kwa ajali na kwenye jana ni mkono wa Mungu tu ulitulinda kwasababu gari zilitaka kugongana uso kwa uso kati ya basi letu na semitilela iliyobeba mbao tukiwa tunapandisha mlima wa nyangoro baada tu ya kutoka pale bwawa la mtela, kwahiyo jana ucku alikuja kuhakikisha kwamba nilifika kweli na jambo la kumshangaza akanikuta nimefika bila kufa kwa ajali.

Kwahiyo huyu mtoto mchawi nilipoongea nae leo jumapili akasema jana mama mdogo alikasirika sana alipokuona umefika, kwahiyo ucku wa jana akaenda kwenye vikao vyao vya uchawi na akamueleza mkuu wao kuwa nimefika salama bila kufa kwa ajali pamoja na kunitegea dawa zao 

Ndipo mkuu wake wa uchawi akampatia dawa nyingine na kumtuma aje leo hapa nyumbani ili anitegee hiyo dawa. Na kweli alikuja mchana wa leo jumapili nikiwa bado namhoji huyu binti waliyekuwa wanafanya nae uchawi na alipokuja akaingia ndani akanikuta nimekaa sebuleni nikiwa na Biblia na vitabu na baada ya muda akaondoka


Kumbe alipokuja alikuja na dawa na akataka aimwage mlangoni ili nikiivuka miguu ivimbe kisha nifariki ili yeye aendeleze uharibifu kwenye hii familia.

Unajua nikamuuliza huyu mtoto kuwa nikwanini huyu mama mdogo anataka kuniua alishindwa kwenye ajali jana na leo kaja na dawa pia akashindwa kuiweka ili aniue, ndipo huyu binti akasema anataka kuniua kwasababu naisaidia hii familia kwa maombi pia mipango yake haikamiliki pia anasema nilipokuja kwa mara ya kwanza nilivyokuwa naomba anapata shida sana kule kwake.
Kwahiyo namshukuru sana Mungu Baba anazidi kunipigania na kunilinda pamoja na kwamba huyu mchawi kanishindwa kiroho ndipo sasa anakuja kimwili ila ninajua jambo moja kwamba hakuna mchawi anayeweza kuniua kwasababu uhai wako ameuficha Bwana Yesu.

Jambo ninalotaka kusema kwako nikwamba Ombea sana watumishi wa Mungu kwasababu tunatafutwa sana na shetani ili atuue kwa lengo la kuua kusudi la Mungu ndani ya watumishi lile Mungu aliloliweka. Na unajua kuwa shetani anapambana kuwaua watumishi walio tishio kwenye ufalme wake endelea kuwaombea
Pia endeleeni kuniweka kwenye maombi ili kusudi la Mungu kunileta tena kwenye hii familia litimie na aendelew kuifungua hii familia.

Nataka nitamke neno hili kwamba usiogope hakuna cha shetani wala wachawi na washirikina wanaoweza kukuua kwasababu bado Mungu anakazi na wewe hapa duniani. Jamabo la muhimu endelea kuishi maisha safi ya utakatifu na kumtumikia yeye Mungu.
Asante sana Uwe na ulinzi wa Bwana wa majeshi.
By Mtumishi Samwel Kibiriti
 +255 765 867574.

Comments