USITAFUTE KICHAKA, JISALIMISHE KWA YESU.

Na Mtumishi Godfrey Miyonjo.

”Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone”
MWANZO 3:8.
BWANA YESU asifiwe.
Wapendwa ninawasalimu kupitia jina La Yesu,
Binafsi Ninamshukuru Mungu anayenitetea hadi hivi leo.
Ni Mungu pekee ndiye atupiganiaye na kutuepusha na mabaya yote ambayo yule mwovu hukusudia juu yetu.
Mtu wa Mungu, BWANA amesema nami ili niseme na wewe kuwa “USITAFUTE KICHAKA”
Kwa maana sisi wanadamu hatuna uwezo wa kujificha mbele za Mungu ili asituone.
Ijapokuwa akili zetu zinatudanganya kuwa twaweza kujificha mbele za Mungu ili asituone, lakini ukweli ni kwamba hatuna uwezo huo.
Ndani ya biblia kuna mifanomingi ya watu wengi waliojaribu KUTAFUTA KICHAKA ili wasionekane mbele za Mungu lakini ilishindikana,
Tukisoma katika kitabu cha MWANZO 3:9-10 tunakuta Adamu baada ya kuitwa na Mungu na kuulizwa “Uko wapi?”Adamu anamwambia BWANA kuwa nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwakuwa mimi ni uchi. Nikajificha.
Yona naye baada ya kupewa agizo na Mungu la kwenda Ninawi kupiga kelele (kuhubiri) alikataa, akaamua kutafuta kichaka (Tarshishi) ili ajifiche huko. (YONA 1:1-3.
Wapo na wengine wengi waliojaribu kujificha, Lakini Mungu aliwaona huko huko mafichoni.
Ndiyo maana BWANA anasema hivi;
“Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawatelemsha toka huko.
Nao wajapojificha katika kilele cha karmeli, nitawatafuta na kuwatoa toka huko; na wajapojisitiri katika vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka huko, naye atawauma”
AMOSI 9:2-3.
Mungu kwa neno lake anadhihirisha kuwa mwanadamu hana uwezo wa kujificha mahala popote pale ili asionekane mbele zake.
Mungu anasema Yeye ni Mungu aliye karibu si Mungu aliye mbali.
YEREMIA 23:24 IMEANDIKWA
“Je, mtu yeyote aweza kujificha mahala pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA”
Hivyo asiwepo mwanadamu miongoni mwetu adhaniaye kuwa amejificha mahali ambapo Mungu hamwoni.
NAMI KWA NENO LA BWANA NINASEMA NA WEWE UNAYEDHANI KUWA HAPO ULIPO NI KICHAKANI (MAFICHONI) MUNGU HAKUONI,
Mungu anakuona sana na anakutaka UJISALIMISHE KWAKE.
Ewe uliyejificha kwenye dini na matendo yako bado ni maovu, hayampendezi Mungu,
Huu ni wakati wako wa kutoka kichakani na kujisalimisha kwa Yesu.
Huu siyo wakati wa kijiteteaa,
oooooooooh! Nami nina dini,
siwezi kuisaliti dini yangu,
mara dini yetu ni kubwa,
sijui ilianzishwa na mitume,
mbona nasi huwa tunakusanyika na kufanya ibada,
Kama ni zaka na sadaka huwa tunatoa,
nasi hushaherekea sikukuu za kidini, N.K,
Mungu anasema hivi:
“Mimi nazichukia sikukuu zenu, nazidharau, nami sitapendezwa na mikutano yenu ya dini, Naam, ijapokuwa mnanitolea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka zaenu za unga, sitazikubali; wala sitaziangalia sadaka zenu za amani na za wanyama walionona”
AMOSI 5:21-21.
Ewe uliyejificha kwenye mafanikio/utajiri,
Ooooooh! Mimi nimefanikiwa bwana
Nimesoma na nina kazi nzuri
Nina pesa za kutosha sina shida,
Mimi ni mkuu wa idara, mimi ni mkuu wa nchi, mimi ni mkuu wa majeshi, mimi, mimi, mimi sina shida tena, Yesu ni kwa ajiri ya maskini, walio na shida, ombaomba, N.K.
IMEANDIKWA
“Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote ili tuvitumie kwa furaha”
1TIMO 6:17.
Ewe uliyejificha kwenye umaskini,
Mimi ni maskini siwezi kuokoka,
Nitaokoka nikifanikiwa,
IMEANDIKWA
“Usijisifu kwa ajili ya kesho; kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja”
MITHALI 27:1.
Ewe uliyejificha kwenye ndoa,Wazazi/walezi, ndugu, N.K
Mume/mke wangu ananikataza kuokoka;
Mme/mke wangu amesema nikiokoka tu ataniacha (tutaachana)
Oooooh! Nilifunga ndoa ya kudini kabisa,
Msimamizi wa ndoa yangu hatanielewa nikiokoka.
Wazazi wangu watanifukuza nikimwamini Yesu,
Baba na mama wamesema hawataki kusikia hata siku moja kuwa nimeokoka.
IMEANDIKWA
“Apendaye baba au mama kuliko mimi anistahili; wala apendaye mwana au binti kuliko mimi hanistahili”
MATHAYO 10:37.
Ewe uliyejificha kwenya kazi;
Kazi yangu hainiruhusu kuokoka,
Mimi ni muuza pombe,
Mimi ni mpokea rushwa,
Nikiokoka nitafukuzwa kazi,
Ninakwambia ni heri ukose kazi ukampata YESU, kwa maana YESU ni mambo yote (ndiyo kila kitu), YEYE ni Alfa na Omega, (Mwanzo na ni Mwisho).
Ewe uliyejificha kwenye wokovu (mwenye wokovu bandia),
Haujaokoka lakini unajifanya umeokoka,
Unajibanza pammoja na waliookoka huku matendo yako ni maovu,
Ninasemaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
USITAFUTE KICHAKA, JISALIMISHE KWA YESU, KWANI YESU ANA HAJA NA WEWE,
Simama na utubu dhambi zako, MUNGU ni mwingi wa rehema atakusameha kabisa.
Ni mimi ndugu yenu
Godfrey Miyonjo (Mtu wa Milki ya Mungu)
WhatsApp 0757649495
Email godfreymiyonjo@yahoo.com or gmlokole1@gmail.com

Comments