JE MALANGO YAKO YA KIROHO YANATUMIWA NA NANI NA KUPITISHA VITU GANI KUJA MAISHANI MWAKO?(4)

BAADHI YA MALANGO YA KIROHO NA VITU VINAVYOPITA HAPO LANGONI:
Tunaendelea na somo letu.
12.( Malango ya kupitishia Utajiri wako )
Kati ya jambo ambalo linawafanya watu wengi waishi maisha ya umaskini pamoja na kujitahidi kufanya kazi ni kutojua kwamba kuna malango ya kupitisha utajiri wao kiroho ili uwafikie kimwili.
Sikiliza kwenye ulimwengu wa roho kuna malango yako ambayo ndio MUNGU anayotumia kuupitisha utajiri uje maishani mwako ila shetani akitaka usiwe tajiri hapa duniani anatafuta malango yako ya utajiri na kuyafunga na akishafanya hivyo utajikuta kimwili unaishi maisha ya umaskini pamoja nakwamba unajitahidi sana kufanya kazi za mikono.
Huwa naumia sana moyoni mwangu ninapomuona mtu tokea akiwa kijana mpaka anafikia umri wa mzee amejitahidi sana kufanya kazi kwa nguvu zake halafu ukichunguza hana hata mafanikio na anabaki kuwategemea watoto wake na wajukuu na wasipomsaidia huanza kuwalaani kwa maneno; sasa huwa najiulizaga kwamba huyu mtu amefanya kazi miaka mingi kwanini asiwe tajiri? Lakini jibu lake nikalipata kwamba shetani ameyawahi malango yake yanayopitisha utajiri na ameyafunga.
Fahamu kwamba ili uwe na maisha ya utajiri hapa duniani unaanza kutajirika kwanza katika ulimwengu wa roho, sasa shetani akitaka usiishi maisha ya utajiri huwa anayafunga malango yako ya kiroho ambayo MUNGU anayatumia kupitisha utajiri wako, sijui unanielewa rafiki yangu?
Tusome kitabu cha ISAYA 60:11 Inasema kwamba "Malango yako nayo yatakuwa wazi daima; Hayatafungwa mchana wala usiku; ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa, Na wafalme wao wakiongozwa pamoja nao".
Hapa umeona Biblia inasema kwamba Malango yako yanatakiwa yawe wazi daima mchana na usiku yasifungwa ili uweze kupata utajiri, kwahiyo inamaana kwamba malango yako yasipokuwa wazi mchana na usiku hutaweza kuwa tajiri hata kama utajitahidi kufanya kazi namatokeo yake utajikuta umetumia nguvu nyingi sana lakini hakuna mafanikio uliyopata makubwa maishani mwako.
Sasa nikuulize rafiki yangu je wewe kwenye ulimwengu wa roho malango yako ya utajiri yako wazi au yameshafungwa na shetani?. Kuna dhana isiyo sahihi imejengeka kwa watu kwamba hapa duniani kuna watu ambao wao ndio wanatakiwa wawe matajiri hiyo sio kweli Bali kila mwanadamu anayeishi duniani MUNGU amemleta duniani awe tajiri sawa na kitabu cha MWANZO 1:26-28. Kwahiyo nikusudi la MUNGU wewe uwe tajiri hapa duniani kwasababu MUNGU amekuumba kwa Sura na Mfano wake.
Ukisoma pia Biblia katika KUMBUKUMBU LA TORATI 8:18 Inasema "Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye Nguvu za kupata Utajiri; ili alifanye imara agano lake, alilowapa baba zako, kama hivi leo".
Kwahiyo Mungu ndie anayetoa Nguvu za kupata utajiri kwa mwanadamu.

Sasa Leo hii ukichunguza matajiri wengi huwa wametajirika kwa kumtegemea shetani na kutumia nguvu za Giza, wala sio kumtegemea MUNGU aliye waumba. Nahili nijambo ambalo sio zuri kabisa na linamkasirisha MUNGU, usije ukajaribu kutumia nguvu za giza za shetani ili uwe tajiri Bali tumia nguvu za MUNGU aliyehai na kumtegemea yeye tu basi.
Watu wengi kwasababu shetani amefunga malango yao ya utajiri wamejikuta wamemfuata na amewaingiza kwenye maagano mabaya sana mpaka wamefikia kutoa makafara ya damu za watu kwa kuwaua ili wapate utajiri, na maagano hayo yamefunga mpaka vizazi vyao. Na wakijaribu kutoka hawawezi namatokeo yake siku wakifa huenda kuzimu na siku ile ya hukumu watatupwa kwenye ziwa la moto wa jehanamu.
Wengine wameambiwa ili wawe matajiri nilazima wafanye mapenzi( ngono ) na wasichana mabikira au watoto wadogo au wazazi wao au watoto wao wa kuwazaa au bibi vikongwe, wengine wameambiwa waende makaburini kuwaomba watu waliokufa au kulala juu ya makaburi n.k, nao huu ni uongo kabisa wa shetani kwani utajiri hauji kwa kufanya mambo hayo, acha kabisa.
Sasa nimalizie kwa kusema hivi ukitaka uwe tajiri hapa duniani sawa sawa na kusudi la Mungu fuata mambo haya;
1. Uishi maisha ya kumpendeza Mungu kila siku.
2. Fanya maombi yà kufungua malango yako ya utajiri kwa kutumia Damu ya Yesu Kristo na Jina la Yesu Kristo.
3. Uwe ni mtoaji sana Sadaka mbalimbali kwa MUNGU zile nzuri sawasawa na Roho Mtakatifu anavyokuongoza.
4. Uwe unatumia fedha zako kuujenga Ufalme wa Mungu yaani kutoa fedha ili kazi ya MUNGU isonge mbele.
5. Saidia watoto yatima na wajane nawale wasiojiweza.
6. Hakikisha kila siku unautafuta Ufalme wa MUNGU kwa bidii zako.
7. Fanya kazi kwa bidii zako ukiwa umemtanguliza MUNGU, na usikate tamaa.
UTAJIRI HAUKO KWA SHETANI RAFIKI YANGU BALI UTAJIRI UDUMUO UKO KWA MUNGU WETU ALIYE HAI.
Ukitaka kuwasiliana nami kwaajili ya kuhitaji Maombi au Ushauri utanipata kwa Namba hii
+255 765 867574. Pia kwenye WhatssAp utanipata kwa namba hiyo
Au kwa Emaili ni: Samwelikibiriti@gmail.com.com

NAKUTANGAZIA KUANZIA MUDA HUU MALANGO YAKO YA UTAJIRI YAFUNGUKE KWA JINA LA YESU KRISTO NA UTAJIRI WAKO UYAFIKIE MAISHA YAKO.
KUMBUKA KAMA HUJAOKOKA NILAZIMA UOKOKE ILI UENDE MBINGUNI.
BÀRIKIWA SANA NA BWANA YESU

Comments