KUITA DAMU YA YESU KRISTO ILI IWE UKUTA WA MOTO KUKUZUNGUKA.

Na Mtumishi Peter Mabula

BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze kisha tuombe maombi ya ushindi.
Siku moja usiku katika ndoto, kulikuwa na vita sana, mambo yalikuwa magumu lakini ghafla akaja mtu mwenye utukufu mwingi akisema ''Tumie Damu ya YESU KRISTO''
Hakika damu ya YESU KRISTO na jina la YESU KRISTO ndio ushindi mkubwa zaidi wa Mkristo.

Zakaria 2:5 ''Kwa maana mimi, asema BWANA, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa huo utukufu ndani yake.''

Katika maombi ni muhimu sana  kuita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kukulinda.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuilinda ndoa yako na kitanda chako na chumba chako.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kuilinda biashara yako.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kulinda baraka zako ulizopewa na MUNGU.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuwalinda watoto wako na mke/mume wako.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuinusuru ndoa yako iliyo katika kuangamia.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuilinda huduma yako uliyopewa na MUNGU
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto Kuilinda nyumba yako au kiwanja chako au eneo lako la biashara.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kulinda uchumba wako mtakatifu.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kuwalinda ndugu zako na ukoo wako na familia yako.
-Ita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kukukinga na kila mishale ya shetani.
Ita damu ya YESU KRISTO katika kitu chako chochote unachotaka kilindwa na nguvu za MUNGU.

Jambo la kuzingatia kwanza ni utakatifu tu, kama hujaokoka hakikisha unaokoka kwanza na tubu uovu wako na kuuacha maana viwango vya MUNGU kukujibu na kukuzingira ni pamoja na wewe kuwa mtakatifu.
Kataa ya dunia maana hayo yataisha.

 Kumbuka Biblia imesema kwamba MUNGU atakuwa ukuta wa moto ili kulinda mji, na katika mji kuna watu hivyo MUNGU atawalinda watu. wewe ni mteule wake na una haki ya kulindwa na MUNGU BABA. ukuta wa moto haiwezekani adui kuuvuka hata akakuroga na kukudhuru.
Biblia pia imsema kwamba tunamshinda shetani kwa damu ya YESU KRISTO na kwa Neno la ushuhuda.

Ufunuo 12:11  '' Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa. ''

Ni muhimu sana kuita damu ya YESU ili ikuzingire adui zako wasikuone.
Damu ya YESU ndio inaweza kugeuka ukuta wa moto na kukulinda.
Usikubali adui zako wakakuona tena kwenye tv zao za kichawi.
Usikubali wachawi wakuroge tena bali ita damu ya YESU KRISTO ambayo haijawahi kushindwa. Damu ya YESU KRISTO ina kazi 4 kwetu na moja ya kazi hizo nne ni kutulinda hivyo utakuwa salama kama utaita damu ya YESU KRISTO katika maisha yako, kazi yako, biashara yako, huduma yako, masomo yako, ndoa yako n.k.

Maombi hapa chini ni ya kukufundisha ili wewe uombe katika hitaji lako na uombe kwa imani na kwa muda mrefu.

Maombi ya kuita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kukuzunguka.

JEHOVAH MUNGU uliye hai ninakuabudu na ninakutukuza. Ni wewe MUNGU mbinguni, ni wewe MUNGU duniani na ni wewe MUNGU kwenye ulimwengu wa roho na kwenye ulimwengu wa mwili pia.
Nakushukuru MUNGU wangu kwa uzima ulionipa na nakushukuru maana hata sasa ninaishi kwa ulinzi wako.
Nakuita BWANA siku ya leo nikiamini kama neno lako linavyosema kwamba ''Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. - Marko 11:24'' 

 Naamini sasa kwamba ninayoomba nitapokea kwa jina la YESU KRISTO.
Nakushukuru BWANA YESU kwa ajili ya damu yako ya agano  la milele ambapo kwa damu hiyo tunapata uzima, ushindi na ulinzi.
Sasa BWANA kwa jina la YESU KRISTO naita damu ya YESU ya agano ili iwe ukuta wa moto kunizingira mimi na familia yangu, adui aliyezoea kunionea usiku nikiwa nimelala sasa hataniona tena maana damu ya YESU KRISTO inanizunguka sasa pande zote, kwa jina la YESU KRISTO naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kunizunguka mimi na biashara yangu ili waharibifu wasinione kamwe kwa jina la YESU KRISTO.  naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kuizingira nyumba yangu na wazazi wangu na watoto wangu na ndugu zangu katika  jina la YESU KRISTO.  naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kulinda uchumba wangu pamoja na mchumba wangu,  naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kuzunguka mimba yangu na mtoto aliye ndani  katika  jina la YESU KRISTO.  naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuzizunguka pesa zangu zilizo benki au dukani  katika  jina la YESU KRISTO.  naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuizingira ndoa yangu ili adui anayepanga kuiangamiza hataiona tena maana imefunikwa kwa damu ya YESU KRISTO  katika  jina la YESU KRISTO.
 naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kunizingira pande zote, kunizingira mimi na mali zangu zote, shetani hataniona mimi wala mali zangu kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
 naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kulinda nyumba yangu na walio ndani yake  katika  jina la YESU KRISTO. 
 naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto  kulinda kanisa letu na mchungaji wetu  katika  jina la YESU KRISTO.
 naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili kuwalinda watumishi wa BWANA YESU wote walio katika nchi yangu  katika  jina la YESU KRISTO.
 naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto kila kona ya maisha yangu  katika  jina la YESU KRISTO.
 naita damu ya YESU KRISTO ili iwe ukuta wa moto ili adui yeyote akija kwangu aangamie kwa jina la YESU KRISTO  katika  jina la YESU KRISTO.
Nakushukuru BWANA maana umejibu maombi yangu.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na ninapokea ushindi sasa Amen Amen.

Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments