MAOMBI YA KUHARIBU UCHAWI NA USHIRIKINA.

Na Mtumishi Peter Mabula.

Bwana YESU KRISTO Mwokozi asifiwe.
 Najua wewe ni muombaji na mara zote huwa unaombea mambo mengi tu.
 Wiki iliyopita kwenye mkesha nilipata ufunuo juu ya kuomba ukiwawawekea mipaka maadui zako katika ulimwengu wa roho. Nilishangaa sauti hiyo ya ufunuo, maombi ya kuwawekea mipaka maadui kwenye ulimwengu wa roho yatakuja siku moja hapa hapa kwenye page yangu.
Leo nataka tuombe tukiharibu uchawi na ushirikina wote.
 Neno ''uchawi'' maana yake ni ufundi wa kutumia dawa ili kuleta madhara kwa watu.
Je ni madhara gani umeyapata kutokana na kurogwa  biashara yako kurogwa ufahamu wako kurogwa maisha yako?

Neno ''Ushirikina' maana yake ni mambo ya uchawi na mizimu.
Uchawi na ushirikina ni vitu hatari katika ustawi wa watu wa MUNGU na ustawi wa kanisa.

 Leo tunaenda kuomba tukiongozwa na Neno la MUNGU.

Hesabu 23:23 '' Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli. Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda MUNGU!''

 Yakobo wa leo ni wewe na mimi tuliookoka tuko na jina la YESU KRISTO, tuko na Damu ya YESU KRISTO na tuko na ROHO MTAKATIFU.
Uchawi sio lolote wala chochote kwako mtu wa MUNGU.
Usiogope uchawi bali wachawi ndio watakuogopa wewe kwa maombi yako kupitia jina kuu kuliko yote  la YESU KRISTO, BWANA na MWOKOZI wetu.

Katika maombi yako leo ;
=Hamisha wachawi wote watoke katika eneo lako, mtaa wako, familia yako, ukoo wako, masomo yako, kazi yako na eneo lako, omba kwa jina la YESU KRISTO utaona ushindi mkuu sana.
=Kemea mapepo ya kichawi na ita damu ya YESU KRISTO iwe moto wa kuwaunguza mapepo wote wanaozungukia kazi yako, biashara yako.
=Haribu mapepo ya magonjwa yatoke katika familia yako na nyumba yako. Haribu mapepo ya ajali, balaa na mikosi yaondoke kwako kwa jina la YESU KRISTO.
=Vunja vunja makazi yote ya wachawi katika ulimwengu wa roho,  mapepo yanayokuibia yaponde kwa moto wa jina la YESU KRISTO na hakikisha unakuwa huru.

=Haribu kila mizimu na kazi zao zitoke katika ukoo wenu na familia yetu.
=Lipua kwa damu ya YESU KRISTO kila tv za kichawi na kamera za kichawi.
=Amuru moto wa damu ya YESU uwaharibu wote wanaolitaja jina lako katika madhabahu za kichawi na kiganga.

Ndugu omba.
BWANA YESU anasema

''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.-Yohana 14:13'' 

Maombi haya ni ya kukusaidia tu katika kuombea hitaji lako mwenyewe ambalo unalifahamu kwa kina. kupitia maombi haya naomba yakusaidie ili ukaombe zaidi ya hapa na naamini utaomba muda mrefu kupitia kujifunza. Kumbuka pia kuishi maisha matakatifu ya Wokovu katika KRISTO maana maombi bila utakatifu  ni msaada wa wiki moja kisha msaada huo unaondoka kwasababu ya wewe kutokuishi maisha matakatifu. utakatifu ni muhimu sana kwa kila mtu.

Maombi.
Ninakushukuru MUNGU BABA kwa uzima wako kwangu.
Nakushukuru kwa kunilinda na kunikinga na mabaya yote.
Niko mbele zako BWANA nikiomba uzima na ushindi wako katika jina la YESU KRISTO. Naukataa uchawi na ushirikina katika jina la YESU KRISTO.
Neno lako BWANA linasema hakuna uchawi juu ya Yakobo na hivyo naamini kabisa hakuna uchawi juu yangu, hakuna uchawi utakaofanikiwa katika maisha yangu kwa jina la YESU KRISTO.
Hakuna uchawi utakaofanikiwa katika kazi yangu, familia yangu na masomo yangu.
Niko kinyume na uchawi pamoja na wachawi wote. kwa mamlaka ya jina la YESU KRISTO ninaharibu uchawi wote uliotumwa kwangu na kwa familia yangu.
Kwa jina la YESU KRISTO ninawahamisha wachawi wote watoke katika nyumba yangu, familia yangu, mtaa wangu na ukoo wangu. nawahamisha kwa damu ya YESU KRSTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mapepo yote ni mawakala wa shetani hivyo kwa jina la YESU KRISTO ninawaondoa katika maisha yangu na kazi yangu, nawaunguza kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila uchawi wa magonjwa ninaufuta kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila uchawi wa kuleta balaa na ajali naukamata katika ulimwengu wa roho na kuutupa kuzimu, mipango hiyo ya giza haitakuwa kwangu kwa jina la YESU KRISTO na kwa moto wa damu ya YESU KRISTO.
Wachawi wote na mipango yao naifuta kwa damu ya YESU KRISTO.
Kila uchawi na mchawi naharibu kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Mlizoea kunitesa lakini kuanzia leo mnateketea wachawi wote na washirikina wote na mizimu wote, kwa jina la YESU KRISTO aliye hai.
Nakushukuru MUNGU wangu maana umenishindia.
Wachawi na uchawi wao umeharibika na hakuna laana ya mchawi itakayonipata,   kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Asante JEHOVAH MUNGU wangu maana wewe ndio mshindi wangu.
Nitakaa salama siku zote kwa jila la YESU KRISTO.
Asante BWANA maana imekuwa katika wewe.
Ni katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea.
Amen Amen.

Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
+255714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili


Comments

. said…
Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159

dawnacuna314@gmail.com