UJUMBE WANGU KWAKO, WA KUFUNGA MWAKA 2015 NA KUFUNGUA MWAKA 2016

Na Mwl Nickson Mabena

Bwana Yesu asifiwe,
Nilikua natakafakari jioni ya leo, nione kama nitapata Ujumbe wa kukushirikisha kabla ya mwaka huu kuisha, namshukuru Mungu nimepata ujumbe, ukanifanya nipitie kwenye Maandiko ili nisome palipoandikwa!.
Neno linasema,
"Nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli." ISAYA 45:3
Katika vitu ambavyo shetani anapambana navyo, ni jinsi ya kuzuia watu wanaomjua Mungu wasifanikiwe,
Anapambana Waliomjua Yesu wasifanikiwe kwenye Maeneo mengi, likiwemo eneo muhimu sana, eneo la Uchumi!.
Zipo sababu za ki-Mungu zinazoweza kufanya mtu akachelewa kufanikiwa, lakini zipo za Kishetani Pia!.
Shetani anajua endapo ukifanikiwa, Utasapoti Kazi ya Mungu, na ufalme wake utanyanyaswa,
Kwa sababu hiyo, anaweza akakuruhusu ufanikiwe lakini Usiwe na Mpango wa kusapoti kazi ya Mungu!.
Mungu anampango wa kukufanikisha, angalia kwenye hilo andiko,
Mungu alikua anamwambia Koreshi, masihi wake, lakini alikua bado hajamjua Mungu,

Anasema atampa Hazina za Gizani, na mali zilizofichwa mahali pa siri,
Nisikilize Mtu wa Mungu, Vitu vyako, vipo, ila vipo gizani, vimefichwa Mahali pa siri,
Kazi, Ndoa, Masomo, pesa, Vipo, Inahitajika nguvu ya ziada, itakayomfanya Mungu anyooshe mkono wake avichukue mahali pa siri na akupatie!.
Pamoja na Ahadi hiyo, njia ya Kufanikiwa sio rahisi kama unavyotaka, ndio Maana Mungu alitangulia Kusema,
"Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma;" ISAYA 45:2
Si umeshaona hapo!?,
Tunapoenda kuanza Mwaka Mpya, Mungu aende mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza, na kuvunja kila Kikwazo Mbele yako..
Natamani Mwaka ujao ufanikiwe, ili Kazi ya Mungu isonge mbele, na wewe Pia, uishi kwa Amani na Furaha!.
Kama utaamua Kukaa na Mungu vizuri, Mungu yupo tayari kukupa hazina(vitu vya thamani) zako za gizani, na Mali zako zilizositirika!.
Yesu akupe kibari, Yesu akutunze, Yesu akufanikishe!,
Lakini, Utakapofanikiwa USIMSAHAU BWANA MUNGU WAKO!.
"Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. Angalia, utakapokua umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; na makundi yako ya ng'ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulichonacho kitakapoongezeka; basi hapo moyo usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utamwa;" KUMBUKUMBU 8:11-14
Na Huu ndio ujumbe wangu kwako,
Mungu akubariki!
HERI YA MWAKA MPYA WA 2016!.
By Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments