UTHAMANI WA MWANAMKE



Scholar Mabula
Na mtumishi Peter Mabula.
 BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Jambo la kwanza naomba niseme kwako Mwanamke kwamba;
Mpango wa MUNGU kwako hauna mabadiliko.
=Hata kama adui atainuka kiasi gani lakini mpango wa MUNGU kwako hauna mabadiliko.
=Hata kama litainuka tatizo kubwa kiasi gani lakini naomba utambue kwamba mpango wa MUNGU kwako hauna mabadiliko.
=Hata kama litatokea tatizo la dunia nzima lakini kama MUNGU amekupangia jambo tambua tu kwamba katika jambo la MUNGU kwako hakuna mabadiliko.
Baki katika Kumwamini na kumuomba na kuishi katika maisha mataktifu maana hadi leo bado mpango wa MUNGU kwako uko pale pale.


Mithali 11:16A ''Mwanamke wa adabu huheshimiwa daima; ''

Heshima hutanguliwa na tabia yako.
Ili uheshimiwe ni lazima uwe na adabu.
Ili uheshimiwe ni lazima kwanza wewe mwenyewe ujiheshimu.
MUNGU hubariki wale wenye kumtii na kujiheshimu.
Scholar Mabula
Kwa wewe unamweshimu MUNGU na kumtii ni kwamba MUNGU Akisema atakubariki hakika atakubariki hataka kama utaona wengine wote wameshindwa kubarikiwa.
=Akisema utafunga ndoa, hakika itakuwa hivyo, usinung'unike bali omba katika utulivu huku ukimngoja BWANA Maana mpango wake kwako hauna mabadiliko.
=Akisema utapata kazi, ni hakika hata kama wenye elimu kubwa kuliko wewe wameshindwa.

BWANA YESU akubariki sana na songa mpele katika yeye siku zote.

Zaburi 68:11 '' BWANA analitoa neno lake; Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa; ''

Wanawake ni jeshi kubwa.
Wanawake wanaweza wakijiwezesha sio mpaka wawezeshwe.
Mwanamke anaweza kutimiza kusudi la MUNGU katika jambo lolote.
Hana aliweza kutimiza kusudi la MUNGU la kumleta Nabii Samwel.

Sehemu ya Maombi ya Hana yalikuwa haya;

 ''Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama MUNGU wetu. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; Washindanao na BWANA watapondwa kabisa; Toka mbinguni yeye atawapigia radi; BWANA ataihukumu miisho ya dunia; Naye atampa mfalme wake nguvu, Na kuitukuza pembe ya masihi wake. -1 Samweli 2:2,8-10''


Mwanamke ni wa thamani sana.

Mwanamke Abigairi kwa kuonyesha uthamani wa mwanamke alitimiza kusudi jema la kutokuangamia kwa familia yake yote

1 Samwel 25:32-34 ''Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe BWANA, MUNGU wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki; na ibarikiwe busara yako, na ubarikiwe wewe, uliyenizuia hivi leo nisimwage damu, wala kujilipiza kisasi kwa mkono wangu mwenyewe. Kwa kuwa ni kweli, aishivyo BWANA, MUNGU wa Israeli, aliyenizuia nisikudhuru, kwamba hungefanya haraka kuja kunilaki, hakika huyu Nabali asingaliachiwa hata mtoto mume mmoja, kutakapopambazuka asubuhi. ''
 
Mwanamke ni wa thamani sana mbele za MUNGU.

Mwanamke ana thamani sawa na mwanaume mbele za MUNGU.
-Mwanamke ni mkamilishaji.
-Mwanamke ni mjenzi wa balipobomoka.
-Mwanamke ni sababisho la mafanikio.

Nimejisikia furaha leo kuongea hayo juu ya wanawake.

Mwanamke anatakiwa awe mcha MUNGU halisi.
Mama aliyeokoka ni zawadi kwa familia yake.
Mama aliyeokoka ni chanzo cha familia yake yote kuokolewa na BWANA YESU.
Binti mchaMUNGU ni hazina njema kwa kanisa.
Binti mmoja mchaMUNGU na mwenye hofu ya MUNGU watu walipomuona tu kwa mbali walisema hivi juu yake.

''Kisha Boazi akamwuliza mtumishi aliyewasimamia wavunaji, Na huyu je! Ni msichana wa nani?-Ruthu 2:5''

Mwanamke kuwa na hofu ya MUNGU ni baraka kwake.
Tuko katika dunia iliyoharibika kwa mambo mbalimbali. MUNGU anawategemea watumishi wake wa kiume na wa kike katika kutengeneza. 
Kazi ya wateule wa MUNGU ni kumtumikia MUNGU.
Kuwa kielelezo cha matendo mema.
na kuhakikisha injili ya KRISTO inayookoa inasonga mbele.

Usikubali kuwa mwanamke tu bali hakikisha unakuwa Mwanamke mwema.
Hakikisha unakuwa mwanamke aliyeokoka.
Hakika unakuwa mwanamke anayemcha MUNGU na kumwabudu katika Roho na kweli siku zote.

Mithali 12:4 '' Mwanamke mwema ni taji ya mumewe; Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.''

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichako chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments