JINSI MAPEPO YANAVYOMSHIKA MTU KWA KUKOSA NENO LA MUNGU

Na Mtumishi Geoffrey Mwanza.

Bwana Yesu atukuzwe sana?
Kuna mtu aliniuliza:
"Pastor ni vipi mapepo yanavyowashika watu wa Mungu?"
Majibu yangu kwa mwenye swali hili:
Nilimwambia kuwa mapepo yanatumia njia zifuatazo kuwashika watu wa Mungu:

1.Kupitia kutoa sadaka: 

Watu wengi hupenda kutoatoa sadaka mahali popote waendapo bila kujua ni madhabahu ya Mungu au ni ya shetani.
Kama madhabahu yale sio ya Mungu unapata umetoa sadaka na kujiunganisha na ibada ile.Miungu ile itakusajili na unakuwa member pale.

2.Kupitia kutenda dhambi: 

Mtu anapotenda dhambi utukufu wa Mungu unamwondokea huku anakosa immunity ya kuzuia mapepo kumwingia.Mapepo yatapata urahisi wa kupenya ndani yake kwani atakuwa kama boma lisilo na fence.

3.Kupitia kuyatii mafundisho ya uongo:

Unapohubiriwa na kushawishiwa uongo heti Biblia inasema ufanye dhambi na utubu baadaye, utapata kukaluwa na mapepo maana hauna Neno la kweli la Mungu na hakika shetani atakumeza.

4.Kuyafuga mapepo: 

Kuna watu kwa kujua au kutokujua watapewa mapepo wayafuge ili yawe walinzi wao,kwa biashara,kwa kukamilisha kesi,kupata watoto na kisha washtukia wanafunzi wanapiga duru shuleni mapepo yakisema wewe ndio baba/mama yao.

5.Upagani (being a pegan)

Upagani ni hali ya mtu kuwa yeye hana imani kwa dini yoyote kwani haamini kuwa kuna Mungu au kuna shetani.
Maana kutoamini kwake si tisho kwa shetani,mapepo yanapomuona yanapata mahali pazuri pa kuishi kwani no kama jumba lisilo na mwenyewe.

Mapepo haya yaweza kuwa kwa mfano wa hirizi za kujifunga viunoni,madawa ya kumwaga kwa biashara,mchanga wa kumimina kwa nyumba yako nk.

Epuka njia hizi zote na uokoke kwani Bwana Yesu ameniweka kwa Hapa  nikufungue macho.
ISAYA 42:6-7 "Utawafungua macho vipofu na kuwaweka huru wote waliofungwa na waliokaa gizani utawapa nuru"
Ubarikiwe na kama umeokoka zidi kukaza imani yako kwa Bwana Yesu na kama hujaokoka okoka sasa hivi.
MUNGU akubariki sana.
By Pastor Geoffrey Mwanza 
Tupigie simu kwa ushauri zaidi:
THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES
Geoffreymwanza@yahoo.com
+254724 656 653

Comments