KUNENEWA NA MUNGU WA MBINGUNI



Na Mtumishi Geoffrey Mwanza.
Bwana Yesu asifiwe?

Karibu kwa somo la leo na ninaamini utabarikiwa na Yesu Kristo aliyenituma.Leo tunaenda kujifunza somo jipya lenye kichwa:
KUNENEWA NA MUNGU WA MBINGUNI
Mtu anapoomba huwa ananena na Mungu akiwakilisha mahitaji.Ili maombi yako yafanikiwe ni lazima uombe kupitia kwa Jina la Yesu pekee.
Unapomaliza kuomba utabakia kumgojea Mungu akujibu maombi yako.Mungu atakunenea ili kukupa majibu yako.

Ili ufikie hatua ya kuenewa na Mungu ni lazima uwe na mambo fulani:
-Uwe mwombezi

-Uzidishe utakatifu kwa Mungu
-Uwe msomaji wa Neno la Mungu
-Ujitenge na vikao vya uovu/dhambi
-Nyakati zote uwe tayari kunenewa na Mungu.

Mungu hunena na watu wake nyakati zote mahali popote bali siku ya ibada Kanisani Mungu anaweza kukunenea zaidi.
Mungu anaweza kukunenea ukiwa njiani kuelekea Kanisani,ukiwa Kanisani,ukitoka Kanisani hata ukiwa nyumbani baada ya ibada.
Mungu anaweza kutumia wanyama,wendawazimu,ndege kwani hata sauti ya paka dirishani kwako wakati wa usiku yaweza kuwa ni njia ya Mungu kukuamsha uombe.
Watu wengine hudhani tu sauti ya paka dirishani ni pepo limetumwa kwao huku wakikemea na kusema "shindwa! shindwa katika jina la Yesu kumbe maana wewe si mwombezi ukatofautisha sauti ya Mungu na ya shetani.

Kumbuka kisa cha kunguru aliyetumwa kwa Eliya kumlisha.Ingekuwa ni wewe na uone kunguru karibu nawe utakemea ukisema:
"Shindwa jini Khadija na buibui zako nyeusi"
na baadaye utakuwa umepoteza nyama na mkate aloletewa nabii Eliya.

Eliya alikuwa mwombezi na alijua maana ya yule kunguru ni mjumbe wa Mungu.
Dada unaomba Mungu akupe ndoa,kijana mzuri na aliyeokoka akitumwa na Mungu kwako wamwangalia kwa dharau maana hana kazi/anabangaiza huku ukisema si umbavu wako kwani umbavu wako ni mtu ako na gari.

Panya,kunguni hata kukosa kazi ndani ya nyumba yako yaweza kuwa ni njia ya Mungu kukunenea ili uombe ukikemea roho ya kutofanikiwa/umaskini.
Vita kwa ndoa,kukosa kazi yaweza kuwa si mapepo ni njia ya Mungu kukunenea ukae kwa maombi,au utoe sadaka fulani mambo yako yafumbuke.
Sio vita pekee hata kubarikiwa na mali nyingi kwaweza kuwa njia ya Mungu kuongea nawe uwasaidie maskini/wajane/mayatima ila wewe waona ni ujanja wako.Usipotii sauti ya Mungu mali yako itaisha ushangae ndipo utaanza kupigia mchungaji simu mara wasema shetani kakuvamia,kumbe wewe ndio shetani tu.
Kaa katika maombi ubainishe sauti ya Mungu na ya shetani.
Mungu hutumia njia nane tofauti ili kuongea na watu wake. Mwanadamu hutumia maombi kuongea na Mungu kisha Mungu atayajibu maombi haya kwa njia zingine.

Njia hizi ni pamoja na:
1.Malaika
2.Sauti ya wazo
3.Watumishi wa Mungu
4.Kupitia Neno lake
5.Kupitia ndoto
6.Kupitia ishara
7.Kupitia maono
8.Kupitia mazingira

Mungu anaweza kutumia njia hizi zote au akatumia mojawapo yake ili kukunenea.Haitategemea na wewe unataka atumie ndoto au watumishi,itategemea njia anayotaka yeye mwenyewe kwani waweza tarajia ndoto naye kaleta mazingira.

1.MALAIKA
Malaika ni viumbe ambao Mungu amewaumba ili kupeleka/kuleta ujumbe anapowatuma.

Nyakati zingine Mungu anaweza kumtumia mtu unayemjua kama malaika ili akuletee habari fulani.
Ni vizuri sana kuwa macho kuijua sauti ya Mungu kwani nyakai zingine malaika anaweza kutumwa kwako na ukakosa kujua kama ni malaika wa Mungu ukamfukuza huku ukijiondolea ujumbe wako kutoka kwa Yehova.
Mfano:
MWANZO 18:1-15 na 19:1-11 Mungu aliwatuma malaika kwa Abrahamu kwenda kuthibitisha agano la kuzaliwa kwa lsaka kisha wakaelekea Sodoma kumpelekea Lutu habari za kuondoka Sodoma kwani ghadhabu ya Mungu ilikuwa juu ya Sodoma na nchi ile ilikuwa iangamizwe.

WAAMUZI 6:11-Malaika wa Mungu amtokea Gidioni na kumpa habari za kuikomboa Israeli mikononi mwa Midiani.
LUKA 1:26-37-Malaika Gabrieli amtokea Maria mamake Yesu na kumpa habari za kuzaliwa kwa Yesu mwanaye.
MATENDO 12:7-11-Malaika wa Mungu amtokea Petro akiwa gerezani.
Malaika wameonyeshwa katika sehemu nyingi sana ila tu nimenukuu baadhi ya sehemu chache maana Biblia ni kubwa.
Mtu anapokuwa mwombezi sana atapata ufahamu wa juu kwani malaika ikitumwa kwakona Mungu na ukose kufahamu kuwa ni malaika wa Mungu utakosa ujumbe wako muhimu kwani hata ujumbe huu waweza kuwa Mungu amenituma kama malaika kwako.
Huyo jirani yako usiyemwongelesha aweza kuwa ndiye malaika aliyetumwa na Yehova kwako,enda kuanzia Leo mkasameheane kwani kukosana ni machukizo mbele za Yehova.
Mungu wangu Yehova akubariki na kama hujaokoka tubu kuanzia leo na umwelekea Bwana Yesu ili uupate uzima wa milele.
Nimetumwa kwako na Mungu kama malaika nikakwambie kuwa ni wakati wako a kumgeukia Mungu na kumkaribia kwani mtu asiye na wokovu yuko mbali na Mungu muumba wake.
MUNGU akubariki sana.
By Pastor Geoffrey Mwanza. 
Tupigie simu kwa ushauri zaidi:
THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES
Geoffreymwanza@yahoo.com
+254724 656 653

Comments