LAANA YA NGONO NA MTU WA UKOO.

Na Mtumishi Geoffrey Mwanza

Bwana Yesu asifiwe?

MWANZO 19:30-38 "Loti/Lutu aliogopa kuishi Soari kisha akauhama mji huo yeye pamoja na binti zake wawili.Wakaenda kuishi pangoni milimani.
Binti yake mkubwa akamwambia dadake mdogo "Tazama baba yetu ni mzee na hakuna mwanamume nchini wa kutuoa tupate watoto.Tumlevye baba yetu ili tulale naye atuzalie watoto."
Usiku huo wakamlevya baba yao divai na binti mkubwa akalala naye na kupata mimba........
Yule binti wa kwanza akajifungua mtoto na kumwita jina lake "Moabu" na ndiye baba wa wamoabu hata leo.

Ninaongea na watu kumi na wawili ambao walipouona ujumbe huu wameshtuka maana wamehusika kukifanya kitendo hiki kiovu na cha laana na wazazi wao,Dada zao,ndugu zao,mama zao,babu na hats nyanya au na watu WA ukoo wao.
Tazama uone kuwa baada ya binti hawa wote kulala na baba yao walizaa wana wa laana.Maisha ya binti hawa yakawa yamelaaniwa,ukoo wa wana wao ukalaaniwa na ikawa hata hakuna cha kufaulu kwa ukoo huo.
Hivyo ndivyo familia yenu ilivyo maana mambo kama haya yalitendeka na hata leo ndoa hauna na umeamua kufanya ukahaba ukingojea kaburi kwani umekosa matumaini.
Haijalishi mtu wa ukoo wako aliyekufanyia kitendo hiki alikubaka,mlikubaliana ila Mungu amenitokea usiku wa mida ya saa nane nikupe mwelekeo wa kuifuta laana hii kwani maisha yako hayawezi kuwa mazuri kabla ya maombi.
RUTHU 1:1-5 Biblia inasema baada ya njaa kuu kuikumba Bethlehem,Elimeleki na mkewe Ruthu waliamia nchi ya Moabu maana ndiko kulikuwa na chakula.
Walipofika nchi ile Elimeleki na wanawe wawili Kilioni na Mahloni walikufa vifo vya ujanani kwa sababu ya ile laana iliyokuwa imesababishwa na binti za Lutu kuzaa na baba yao kwani nchi nzima ya Moabu ililaaniwa ikawa hata uingie pale na kitu kizuri kitaharibika au kife.Laana ni mbaya.
Ndugu huenda mke uliyeoa alilala na babaye,huenda mumeo alilala na mtu wa ukoo wao,pengine kuna mmoja kati ya uzao wao pengine babaye/mamaye.Tambua hawezi kukwambia wewe.Itabidi uombe maombi ya kumnasua kwa laana ile.
Watoto wengine baba zao ni wajomba zao,huenda pia mumeo ashawahi kutana kimwili na mamako mzazi.
Mungu amenituma kwako kwani ameona kilio chako.Umejaribu kutaka kuelezea watu wakusaidie ila unakiona kitendo chenyewe kina aibu kusema na watu watakuona mjinga.

Nimetumwa kwako na Mungu nikakwongoze katika maombi yakukuweka huru.


Utaomba maombi haya kisha unaweza kutenga wakati wako mwafaka ukaomba tena kwani huu ni mfano tu:

Kumbuka maombi haya ni muhimu sana kwa kila mmoja maana huenda kuna mtu wa nyumba yenu aliyeutenda uovu huu.Hata kama wewe hukuutenda lakini yaombe uokoe ndugu zako/watoto wako na watu wenu wote.

MAOMBI YA KUTUBU/KUFUTA LAANA KWA KITENDO CHA NGONO NA MTU WA UKOO WENU.

"Baba wa Mbinguni katika Jina la Yesu Kristo ninakushukuru kwa kunipa kuiona siku ya leo na kunipa uzima kila kuchao.
Ninakushukuru Bwana Yesu maana una mpango mzuri juu ya maisha yangu.
Neno lako (Yeremia 29:11) unasema yakwamba unaniwazia mema.Asante sana Yehova Mungu wangu.
Ninakushukuru maana Baba hauko mbali nami Bwana kama vile usemavyo kuwa wewe ni Mungu wa karibu si wa mbali.(Yeremia 23:23)
Isaya 59:1-2 unasema yakwamba dhambi zetu ndizo zimetutenga na uso wako na unazidi kusema kuwa nikuje tuojiane hata kama dhambi zangu ni nyekundu kama madoa utaniosha na kunisamehea na kuwa mweupe kama pamba(Isaya 1:18).Nisamehe Bwana Yesu kwa ajili yangu na ukoo wangu.
Tazama Bwana Yesu naja kwako unisamehe kitendo cha ngono nilichokitenda/walichokitenda watu wangu na mtu fulani wa ukoo wangu (mtamke jina lake) na ambacho kilisababisha dhambi na laana juu yangu na nyumba yangu.
Nilikutenda uovu,Yesu nisamehe na unitakase kwa damu yako na kwa Jina la Yesu Kristo.
Kila kitendo cha ngono kilichotendwa na watu wa nyumba yetu,mume/mke/watoto/ndugu/dada na mtu yeyote wa ukoo nimetubu leo na kuoshwa kwa damu ya Yesu katika Jina la Yesu Kristo.
Uovu huu umezuia baraka zetu.
Nyanya/babu/mama/baba yangu alihusika kwa dhambi hii.Yesu msamehe na utuondolee laana hii katika Jina la Yesu Kristo.
Yohana 14:14 unasema kuwa na lolote tutakaloliomba kwa Jina la Yesu tutapewa,leo nimeomba msamaha na nimesamehewa na Yesu Katika Jina la Yesu Kristo.
Ninafuta kila laana za kiukoo zinazotuandama kwetu kupitia ngono ya ukoo kwa damu ya Yesu na katika Jina la Yesu Kristo.
Kuanzia sasa tumesamehewa na tuko huru katika Jina la Yesu Kristo.
Najifunika Mimi pamoja na ukoo wetu kwa damu ya Yesu Kristo.Tutabakia guru kutoka sasa kama lisemavyo Neno lako (Yohana 8:36) katika Jina la Yesu Kristo nimeomba na imetendeka.
AMEN.

Tupigie simu kwa ushauri zaidi.
"THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES
Geoffreymwanza@yahoo.com
+254724 656 653.

Comments