MAFUTA YA KUPAKA,VITAMBAA,MAJI,FAGIO NA CHUMVI NI UFUNUO MTUMISHI ANAOPEWA NA MUNGU

Na Mtumishi Geoffrey Mwanza.

Bwana Yesu asifiwe?
Karibu kwa somo la mafuta ya kupaka,vitambaa,chumvi na vitu vingine.Watu wengi wamenitaka nifundishe somo hili huku wakiniuliza kama ni halali kutumia vitu hivi.
Watu hawa wameniulizia ni wapi vitambaa,fagio na vitu vingine vimetumika katika Biblia?

Biblia imeonyesha MAFUTA ya kupaka katika:

Marko 6:13 - Wanafunzi wa Yesu waliombea wagonjwa wakawapaka mafuta na kupona.

Yakobo 5:14 -Akipatikana mgonjwa katikati ya kanisa aombewe kisha apakwe mafuta ili apone.

Isaya 10:27 -Nira ya shetani huvunjwa na kuharibiwa kwa kupakwa mafuta.

Kupakwa mafuta ni kupokea ROHO MTAKATIFU.
Kile cha muhimu zaidi si kuona vitambaa /chumvi/maji/fimbo/nguo nk vikikufungua, cha muhimu zaidi ni kuacha dhambi na kuokoka.
Lakini ni lazima tujue haimaanishi mafuta ni mafuta tu,mafuta yanayosemekana hapa ni ROHO MTAKATIFU wa Mungu.

Nataka nikwambie kuwa sio kila kitu mtumishi wa Mungu ambacho atakitumia kimeandikwa kwa Biblia ila vitu vingine huwa ni ufunuo wa nabii huyu anayekuombea anapewa na Roho wa Mungu atumie.
Sisi twataka tu kukiona kilichoandikwa Bibliani na huku tumeshindwa kutimiza vile vichache vilivyoandikwa.

Mfano:
Biblia inasema tuokoke na tunashindwa.
Je, kwa nini tusitimize kwanza haya Bwana Yesu anatutaka?
Wakati wa Nabii Elisha,Mungu alimpa Elisha ufunuo wa kumtuma Naamani kujitosa mtoni Yordani ndio apone ukoma.
Leo mtumishi akwambie ukajitose mtoni karibu na kwenu utakataa ukisema mtumishi yule ameiweka miungu yake mtoni huo na anatafta kukuua.

Wakati wa Bwana Yesu aliyetumia mate kutengeneza tope na kumpaka kipofu macho pia ni ufunuo.
Musa kuinua fimbo bahari ya Shamu njia ikapatikana pia ni ufunuo.Kuna mafunuo mengi ambao yanapatikana kwa Biblia.
Musa alipoiangusha fimbo yake kwa nyumba ya Farao na ikawa nyoka,wachawi wa Farao waliangusha fimbo zao pia zikawa vijoka ila ikawa nyoka ya Musa ikawameza vinyoka vya wachawi wa Farao.

Hata hivo pia manabii na walimu wa uongo hutumia mafunuo yao ya miungu kudanganya wakristo.

Sio mafunuo yote yanayotokana na Mungu wa mbinguni.
Ukiwa mwombezi na msomi wa Neno la Mungu utapata ufahamu wa kutofautisha mafunuo ya Mungu na yale shetani.

Ukipata mafuta/vitabaa/chumvi/mchanga/maji nk vinavyouzwa ujue hayatokani na Mungu wa mbinguni.
Kaa macho kwani sio miujiza yote inayotokana na Mungu na pia sio yote ya shetani.
Ubarikiwe na kama hujaokoka okoka sasa.
By Pastor Geoffrey Mwanza. 

Tupigie simu kwa ushauri zaidi:
THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES
Geoffreymwanza@yahoo.com
+254724 656 653

Comments