ONDOA 'TATTOO' NA CHALE MWILINI MWAKO

Na Mtumishi Geoffrey Mwanza.
Bwana Yesu apewe sifa?

Nina habari njema kwa watu wa Mungu ambao wamechorwa michoro mwilini mwao (tattoo) na pia chale za kukatwakatwa maana Mungu anasema waifute mara moja.

WALAWI 19:28 "Msijitie alama zozote mwilini mwenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata mwilini au kujichanja chale.Mimi Bwana Mungu nimesema"

Umeona Mungu amekataa hii michoro ni machukizo mbele zake kwa kuchorwa cobra,dragon,scorpion,eagle nk.
Kuna wengine pia wanachora ushetani huu kwa sehemu zao za siri jambo hili ni uovu mkuu mbele za Yehova Mungu enda uzifute kabisa mama,mzee,dada,ndugu umpendeze Mungu.
Waendao kwa waganga pia na kukatwakatwa chale mwilini ujue hayo ni machukizo mbele za Mungu.

Mstari wa 31 "Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi.Mimi Mungu nimesema"

Habari ndio hiyo mtu wangu.Kama umepangia kwenda kwa mganga/mchawi/mnajimu anza kupangua safari na umwendee mtumishi wa Mungu kisha umkabidhi Bwana Yesu maisha yako.
Ndugu,kwa mganga hakuna msaada waache kukudanganya wameanza kutupigia simu kisiri wakitaka maombi ya kuokoka kwani wameujua ukweli uko tu ndani ya Yesu.

Omba maombi ya kujinasua mikononi mwa wachawi na waganga na Bwana Yesu akakushindia kwa damu yake.

Toa,tupa au choma hiyo hirizi iliyo kiunoni na pia chochote ulichopewa kwa manganese kwani ndicho kizuizi cha maisha yako mazuri na ni sanamu ambayo Mungu anaikataa.
Barikiwa sana na Bwana Yesu.
By Pastor Geoffrey Mwanza. 

Tupigie simu kwa ushauri zaidi:
THE GLOBAL EVANGELISM MINISTRIES
Geoffreymwanza@yahoo.com
+254724 656 653

Comments

Anonymous said…
Wajin’’.- kichwa cha habari kingine mnatuhubilia injili kwani humu kanisani