USHUHUDA WA MAISHA YA RAFIKI YANGU MMOJA ALIYENITUMIA ILI NIMUOMBEE.



Mtumishi nakusalimu katika jina la BWANA wetu YESU Kristo.
Mimi mkazi wa Mbezi jijini Dar es alaam
Mara nyingi nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mafundisho yako kupitia huu ukurasa wako wa facebook. kiukweli nimejifunza baadhi ya mambo katika maisha ya ulimwengu wa kiroho.

Mtumishi naomba nikuandikie historia ya maisha yangu kuanzia nilipozaliwa, nilikopitia na mpaka sasa hapa nilipo..
kuna matatizo mengi sana yamejitokeza katika maisha yangu lakini naamini baada ya kusoma utaangalia ni jinsi gani naweza kuendelea mbele kutokana na uwezo mwenyezi MUNGU aliouweka juu yako.

Mwaka 1992 nilizaliwa mkoani Tanga.
Baba yangu alikutana na Mama yangu Jijini Dar es alaam katika harakati za kibiashara. lakini wazazi wangu hawajawahi kuoana wala kuishi pamoja.
kipindi mama yangu yupo na mimba alikuwa akiishi na baba yake Tanga.
lakini baba yake alipogundua ile hali alimfukuza mama yangu.. kwa mujibu wa mama yangu alihangaika sana ndipo akapata msaada wa kuishi na mama mmoja kule tanga sehemu hiyo iliitwa bonde. aliishi na mama huyo mpaka alipojifungua.
yule mama hakuwa na uwezo lakini alijitoa tu kiubinadamu.

Nilipozaliwa mama yake mama yaani bibi yangu alisikia habari ya kuwa mama amenizaa na amefukuzwa kwa baba yake anaishi kwa kusaidiwa ndipo akamtuma mtu aje atuchukue.
kwa mujibu wa mama yangu.
tulikuja Dar es salaam kwa bibi wiki 1 tu baada ya mimi kuzaliwa. tuliishi kwa bibi tabata ambapo miaka hiyo alikuwa akifanya biashara ya uuzaji wa Gongo.
Baada ya mwezi mmoja kitovu changu kilikatika na Bibi akakichukua lakini mpaka leo hatujui kama alienda kukitupa au alikokipeleka.
Tuliishi na bibi ndipo mama alienda kumtafuta baba yangu alipo. alimpata na alikuja kuniona kwa mara ya kwanza. ndipo akaenda kuwachukuwa ndugu zake waje kunifahamu. lakini cha ajabu baadhi ya ndugu walinikataa wakisema mimi sio mtoto wa yule baba na amebambikiwa. kitendo kile kilimfanya baba aamini maneno yale na akakataa kuja kwa takribani miezi 3 .

lakini baadaye alikuja akaomba msamaha na akakubaliwa na bibi pamoja na mama yangu.. tuliishi pale huku akiwa anasaidia baadhi ya matumizi.
Lakini haikuchukuwa hata muda, mwaka mmoja baadae bibi yangu alifariki ndipo maisha magumu yalianza upya.
Bibi ndiye aliekuwa mhimili wetu mjini pale. lakini alikuwa amepanga na kipindi hicho mama yangu hakuwa na kazi yakumuingizia kipato.

Ndipo kaka zake mama walipoamua kutuchukua na kwenda kuishi nao kwenye chumba kimoja. kilichokuwepo maeneo ya magomeni. tuliishi kwa muda wa miezi 8 ndipo mama yangu alipopata kibarua cha kufanya usafi katika chuo dar technical kilchopo posta. ikabidi mimi anipeleke kwa baba yangu rasmi kwa sababu kipindi hicho sikuwa na mtu wakunilea zaidi ya mama.
lakini kipindi kile baba hakuwa ameoa kwa hiyo ikabidi anipeleke wilayani Lushoto kwa mama yake. yaani bibi angu mzaa baba. nilikuwa na umri wa miaka 2.
Ndipo nikaanza kuishi na bibi angu pamoja na babu yangu. nilisoma huko Tanga kuanzia darasa la 1 mpaka la 7. nilifaulu kwenda sekondari . mwaka 2011 nilimaliza sekondari lakini sikifaulu kutokana na maksi zangu kutoruhusu kuendelea,
baba yangu alikasirika sana. lakini sikuwa na namna.

Mtumishi tangia nimalize kidato cha nne nimekuwa mtu wakutofanikiwa nimesoma vyuo viwili katika kujaribu kujiendeleza lakini naashia katikati simalizi. nimepata ajira zaidi ya mbili lakini naacha baada ya miezi kadhaa bila sababu za msingi
mtumishi nateseka na dunia sina ramani yoyote kimaisha kila ninalopanga halitimii na mbaya zaidi nimekuwa adui mkubwa sana wa wanawake kila kukicha nagombana nao. .

Cha ajabu upande wa mama yangu wamezaliwa wanaume 3 na wanawake 3 lakini kwa wanawake hakuna aliyeolewa hata mmoja zaidi ya kuishi na wanaume na kuachika.
na kwa wanaume wawili hawajaoa na mmoja anaishi na mwanamke tena bila ndoa. . cha ajabu zaidi maisha yao ni magumu sana ukiwaona utawaonea hata huruma. hakuna aliefanikiwa

kwa upande wa baba yangu huku maisha yao kidogo mazuri kwani wameoa na kuolewa lakini cha ajabu waliovuka kwenda kidato cha 5 ni wawili tu. wote wamekwama kidato cha 4.
Mchungaji nilipokuwa nahoji mama yangu aliniambia ukweli kwamba baba alienilea na kuishi naye si baba yangu mzazi bali alikutana naye kimwili akiwa na mimba ya mwezi 1 tayari. lakini mpaka sasa uyo baba yangu mzazi sijui aliko na huyu ninayeishi naye hajui hili lakini nimelificha moyoni mwangu kwa sababu nimeishi naye tangia nipo na umri wa miaka 2 mpaka sasa.
Mchungaji nisaidie kimaombezi.
Ubarikiwe Mchungaji.


Majibu yangu mimi Peter Mabula.

MUNGU wa mbinguni akubariki sana.
mimi nitakuombea na vifungo vyote vitakoma, baraka mpya itafuata na ushindi wa ajabu utauona.
story yako naomba niitumie ili watu wengi zaidi wajifunze kitu na wakuombee lakini sitataja jina lako .
MUNGU wa mbinguni akubariki sana.

Comments