JE! WEWE NI SIMONI MKIRENE, AU UNAMUHITAJI SIMONI MKIRENE?

Na Mtumishi Nickson Mabena

Bwana Yesu asifiwe sana, ninamshukuru sana Mungu aliyenipa nafasi hii ya kuandika ujumbe huu,
Pia, nawashukuru sana wote mnaonitia Moyo, Mnaoniombea, mnaonishauri na kunitakia mema, kwenye huduma yangu!!.
Najua kichwa cha ujumbe kinakuvutia kutaka kujua nimeandika nini ndani, ya somo,
Ninamwamini sana Roho Mtakatifu, kwamba atakuwezesha kuelewa, kile ninachaanisha!!.
Tuanze kumuangalia MTU anayeitwa SIMONI MKIRENE, wa KWENYE BIBLIA.
" *Wakamshurutisha mtu aliyekuwa akipita, akitoka mashamba, Simani Mkirene, baba yao Iskanda na Rufo, ili auchukue msalaba wake*" MARKO 15:21
Ili unielewe ninachomaanisha kwenye ujumbe huu, unatakiwa kuelewa kwanza ,
1.Simoni Mkirene ni nani?
2. Simoni Mkirene Alifanya nini?
3.Alichokifanya Simoni Mkirene, Unatakiwa kukifanya, au kufanyiwa?

1.SIMONI MKIRENE NI NANI?
Hapa nataka nikueleze tu, huyu kwa kifupi,
Simoni aliitwa Simoni Mkirene kwa sababu alizaliwa kwenye mji unaoitwa KIRENE (CYRENE), Nchini LIBYA.
Sawa na Mtu tumuite, Mtanzania, Mtemeke, Mgeita, n.k
Kwa maana hiyo, Simoni hakua MYAHUDI, alikua M-AFRIKA, alizaliwa AFRIKA!.
2.SIMONI MKIRENE ALIFANYA NINI?,
Wakati Yesu yupo kwenye wakati mgumu sana, alipobebeswa Msalaba, akielekea Goligotha, kwa ajili ya Mateso,
Yesu alipokua kwenye hatua ambayo, kwa jinsi ya kibinadamu, asingependa apitie,
SIMONI alikua anatoka zake Shamba, AKASHURUTISHWA KUBEBA MSALABA,
"Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shamba, wakamtwika msalaba, auchukue nyuma yake Yesu". LUKA 23:26
Alimsaidia Yesu kuubeba msalaba lakini kwa kulazimishwa!.
3.ALICHOKIFANYA SIMONI MKIRENE, UNATAKIWA KUKIFANYA AU KUFANYIWA?.
Hapa ndipo kwenye somo langu,
Yesu alikua MYAHUDI, na Simoni, alikua MUAFRIKA, ukiacha masuala ya SIMONI KUSHURUTISHWA, lakini kwa Desturi, ni ngumu kwa WAYAHUDI KUCHANGAMANA NA WATU WA MATAIFA,
Ingenoga zaidi, kama Yesu angesaidiwa na MYAHUDI MWENZAKE,
Lakini alisaidiwa na MUAFRIKA,

Maana yangu ni nini?,
Ni hivi,
Inawezekana kuna Mtu upo kwenye kipindi kigumu, kimaisha, kihuduma, kimahusiano, kijamii, kifamilia, kiuchumi, n.k,
Upo kipindi ambacho, kibinadamu, usingependa uupitie, kwa kifupi, unaelekea "goligotha yako",
Watu wa nyumbani/karibu/kanisani kwako yaani wayahudi wenzako, hakuna hata MMOJA anayejisumbua kukusaidia KUUBEBA MSALABA WAKO!,
Unamuhitaji SIMONI MKIRENE WAKO WA KUJA KUKUSAIDIA!,
Mtu ambaye inawezekana, SI WAKABILA YAKO, SI WA KANISA LAKO, SI WA KARIBU YAKO, aje kufanya huduma yake, ya kukusaidia kuubeba MSALABA!!
Ni Maombi yangu kwa MUNGU, Mtu huyo aje mwenyewe, sio lazima ASHURUTISHWE NA WATU,

Na wewe unatakiwa kumsubiri, inawezekana YUPO SHAMBA BADO, atakuja, ataletwa na Mungu mwenyewe!.
Upande wa pili, Inawezekana wew. Ndio Simoni Mkirene, kuna Mtu unatakiwa umsaidie kuubeba msalaba wake, yupo amechoka sana,
Inawezekana bado upo shamba, hujatambua HUDUMA YAKO,
Inawezekana una wazo la kusema, 'atasaidiwa na ndugu zake', au 'watu wa kanisa lake', nakwambia, usisubiri kushurutishwa, Nenda kafanya HUDUMA YAKO,
Kuna Mambo makubwa yatatokea, baada ya kumsaidia huyo!!.
Haijalishi anakufahamu, au hakufahamu, WEWE SIMAMA KWENYE NAFASI YA "SIMONI MKIRENE"
.....Naamini kuna kitu umekiona, kupitia ujumbe huu!.
MAMBO GANI YANAKWENDA KUONEKANA KWAKO, NA KWA FAMILIA YAKO, NA KWA ULIYEMSAIDIA??,
KABLA HUJAYAJUA YALIYOTOKEA, JIJIBU SWALI HILI, *JE! WEWE NI SIMONI MKIRENE, AU UNAMUHITAJI SIMONI MKIRENE?*
Tukutane, kwenye sehemu ya Pili ya Somo hili......
Naitwa Mwl Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments