KUIBUKA GHAFLA KWA NABII ELIYA MTISHBI KATIKA ISRAELI

Na Mtumishi Geoffrey Mwanza Wambua

Bwana Yesu asifiwe?
Somo hili ambalo nimeliweka mtandaoni nataka ukajifunze kitu kitakachokusaidia maishani mwako.
Ukiangalia katika historian ya nchi ya Israeli,kulishuka ugawanyikaji wa falme, historia ya makabila kumi ya kazikazini huku ikiwa ni kuchukiza MUNGU kwa umwakigaji wa damu na mateso.
Falme zilizofuata zilizidi kila mmoja na ukaidi na ibada ya sanamu (shetani) mfalme wa kwanza akiwa Yeroboamu mwana wa Nebati.(1Falme 14:9, mwanawe Omri akatawala baadaya kifo chake (1Falme 16:25 kisha baadaye akafa na mwanawe Ahabu akatawala mahala lake (1Falme 16:30)
Licha ya kutomtii MUNGU; MUNGU alikuwa tayari kuwaonyesha huruma take kama wangemfuata kwa kweli.
Ilikuwa ni kazi ya Eliya kuregesha ibada ya kweli kwani Israeli nzima ilikuwa imeshawishiwa na Yezebeli ambaye alikuwa mkewe mfalme Ahabu na alikuwa binti Ethbaali mfalme wa wasidoni (watu waliomwabudu baali)
Baada ya kumwoa Yezebeli, Ahabu alibadilika sana na kuwa mwabudu sanamu kwa kushawishiwa na mkewe.Hivo nchi nzima ya Israeli ikawa waabudu sanamu hii (baali).(1 Falme 16:31)
Yezebeli ni jina linalomaanisha "Safi" au "kujipodoa" na mwanamke ambaye alikuwa na asilia ya sidoni na wasidoni na wamisri walikuwa na asilia moja kwani wanawake wao walijipaka rangi ya midomo (lipstick) ambayo ilikuwa ni mawasiliano ya mwanamke kahaba akiambia waume kuwa yuko tayari kwa ngono.
Leo wadada wetu wanajipaka rangi hizi pasipokujua zilimaanishaje.
Ibada hii ya baali ilikuwa ikihusisha vitendo vya ngono na kutoa watoto sadaka na ikawa machukizo kwa MUNGU.
MUNGU alikuwa amewaagiza waisraeli kama watamwasi basi atawaletea mapigo kama ukame ndipo anamtuma Eliya ghafla kama umeme atabiri ukame Israeli kwa sababu ya kumwasi.
Kumbukumbu 11:16-17 "Jihadharini mioyo yenu isichanganywe mkaiabudu miungu mingine nayo hasira ya Bwana ikashuka nakuzifunga mbingu mkakosa mvua"
Pia tazama 1 Falme 8:35-36 "Mvua isiponyesha sababu wametenda dhambi; wakikuomba msamaha maana wamekutenda dhambi uwasikie na kuwasamehe"
Kwa ajili ya uasi huu MUNGU alikuwa azifunge mbingu miaka mitatu na miezi sita ili watu hawa wageukie MUNGU na kumwacha baali.
Luka 4:25 " Lakini sikilizeni kweli kulikuwa na wajane wengi Israeli nyakati za Eliya MUNGU alipozifunga mbingu kwa muda wa miaka mitatu na miezi sits kukawa na njaa katika nchi yote"
Jina Eliya ni jina la kiebrania linalomaanisha "Yehova ni MUNGU wa kweli"


Baada ya Eliya ambaye alikuwa akivaa joho refu la manyoya lililoning'inia mabegani na mshipi wa ngozi kiunoni;
2Wafalme 1:8 "Wao wakamjibu, alikuwa amevaa vazi la manyoya na mshipi wa ngozi kiunoni; mfalme akasema huyo ni Eliya kutoka Tishbi"
Eliya alitabiri ukame katika nchi nzima ya Israeli kwa maana walikuwa wamemtupa MUNGU wa kweli na kuiendea miungu ya kigeni aliyokuwa ameonya Yehova MUNGU (Kutoka 20:1-5)
Watu wote Israeli walikuwa wameiendea miungu hii ambayo ilikuwa ikitenda maajabu na miujiza mikubwa waksmwacha Yehova aliyekuwa amewatoa Misri utumwani.
Leo watu wengi sana wamemwasi MUNGU wa kweli na ndiyo maana wanalia katika maisha yao wakisema wamerogwa; kumbe si kurogwa unahitaji tu uifuate ibada ya kweli kwa MUNGU wa kweli.
Kisha Eliya akatabiri ukame :
1Wafalme 17:1 "Basi Eliya nabii wa MUNGU kutoka Tishbi huko Giliadi akamwambia mfalme Ahabu "Kwa jina la Yehova MUNGU ninayemtumikia nakuapia kwamba hakutakuwa na mvua wala umande hadi nitakapotoa amri"
Eliya alipotabiri hivyo tu akawa anatafutwa na Ahabu na mkewe Yezebeli wamuue kwani alikuwa ameiletea Israeli nzima ukame.Ndipo MUNGU alipomwelekeza Yordani kujificha katika kijito cha Kerithi.
Mstari wa 3 "Ondoka ukajifiche kijito cha Kerithi mashariki mwa Yordani utakunywa maji ya kijito hicho nami nitawaamuru kunguru wakulishe huko"
Bwana MUNGU anafanya maajabu kwa kumtumia kunguru kumlisha Eliya kwani kunguru walikuwa ndege waliotambulika kama wachafu kwa Eliya kulingana na maandiko. (Walawi 11:15)
Pili kunguru ni ndege wapenda nyama na mikate na kipindi hiki cha ukame wangekula chakula hiki chote ila wanakuwa wajumbe wa kutumwa chakula.
MUNGU alitaka kuonyesha kuwa hata watu wanaoonekana wenye dhambi leo wanaweza kubadilishwa kwa damu ya Yesu na kuwa wajumbe wa injili. (Walawi 20:22-26)
Hats ndio maana unaona Eliya akiambiwa na MUNGU aende mjini Serepta uliokuweko SIDONI ile ile alitotoka Yezebeli mlete madhara haya yote akalishwe na mwanamke mjane na masikini.
Elisha angemshangaa MUNGU akimtuma kwa ngome kuu ya ibada ya baali akalishwe namaskini mjane.
Si MUNGU angemtuma kwa matajiri wa SIDONI?!
La hasha alimtaka mjane maskini huyu apokee ukombozi kutokana na mile kidogo alichokitoa kwa Eliya nabii wa MUNGU.

1 Wafalme 17:9 "Ondoka uende Serepta ilioko SIDONI na ukae huko kwani nimeamrisha mwanamke mjane akulishe"
Tazame jinsi mjane huyu anavyofananishwa na kunguru (mstari wa nne).
Amri hii ya MUNGU kumtuma nabii wake katika nyumba ya watu wa mataifa aliyetoka nchi moja na Yezebeli ilikuwa ya kushangaza machoni pa Eliya.
Mama mjane huyu alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wamefinyiliwa ambao MUNGU aliwapendelea kuwapa sheria ya wokovu na kuona wanaishi pamoja na watu wake.
Mwanamke huyu anaonyesha imani ya ajabu kwa kujinyima pamoja na mwanaye ili ampe mtumishi wa MUNGU kile kidogo sana alichokuwa nacho.
Ona jinsi Eliya anavyomwambia mara baada ya kuonana:
Mstari wa 10 "Niletee maji ninywe"
Kumbuka nchi nzima ina ukame na maji ni bidhaa adimu sana kupatikana kisha nabii huyu wa MUNGU anaitisha maji!
Mstari wa 11 "Yule mwanamke alipokuwa anaondoka Eliya akamwita na kumwambia "Niletee na kipande cha mkate pia"
Nabii Eliya kwanza hajaanza na kumwambia mwanamke kuwa MUNGU ameniambia kuwa amekuamuru unilishe; bali anaanza kwa kumpa kazi ngumu ya kumpa maji ya kunywa na kabla aende anaongezea kuwa aletewe mkate pia.
Utii na imani ya maskini mjane huyu ilimletea baraka; Ingawa alikuwa na kisababu cha kujitetea kwa kumwambia Eliya kuwa yeye ni maskini na nimjane; bali alitii alichosema nabii pekee wa Yehova aliyebaki Israeli.
Utii na imani yako kwa watumishi wa KWELI wa MUNGU wa KWELI utakupa kufanikiwa kwa baada ya mjane kumlisha mtu wa MUNGU, yeye akuteswa na ukame kama waisraeli waliokuwa wakiteswa na njaa kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.
MUNGU anataka kukutumia wewe ambaye unaonekana mdhaifu; mwenye madeni; usio na kazi au ndoa kuonyesha wanaojiona wakuu kuliko were; matajiri kuliko wewe, wasomi kuliko we we kwamba ana uwezo wa kukubadilisha.
Wewe uliyezalia kwenu na haujaolewa, wewe uliyeolewa na ukafukuzwa kwa ndoa; wewe unayechumbiwa ukiachwa bila sababu; MUNGU amenituma kama Eliya nikuletee habari njema kuwa ni wakati wako wa kuingia kwa ndoa safi.
MUNGU amenichipua ghafla kama umeme nisimame kama Eliya kwani wengi wa manabii zake wameiacha njia ya MUNGU na kuindea baali (Illuminati) na mienendo inayomchukiza Yehova MUNGU .
Wazazi wako wametenda uovu mbele za MUNGU nitakuongoza kwa maombi ili ujimasue na ukame huu ulio juu yako.
Waisraeli walipigwa na ukame na wslipotambua kiini cha shida yao walitubu na kusamehewa kisha ukame ukaondoka.

Hakuna hata mmoja katika taifa nzima la Israeli ambaye aliiona ghadhabu ya Yehova MUNGU isipokuwa nabii huyu shupavu wa MUNGU Eliya kutoka Tishbi.
Ingawaje Biblia inasema kuwa walikuwako manabii wengi wa Yehova ila malkia Yezebeli alikuwa amewaua kwa upanga huku Obadia msimamizi wa mfalme Ahabu akiwaficha baadhi ya manabii wa MUNGU katika pango hamsini hamsini.
1Wafalme 18:13 "Je, huna habari kwamba Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa MUNGU mimi niliwachukua manabii mia moja wa MUNGU nikawaficha hamsini hamsini pangoni nikiwa nawapatia chakula na maji?"
Mpango wa MUNGU kumlete ghafla nabii Eliya katika taifa la Israeli ulikuwa ni kumaliza ibada mbaya ya baali.
Baali alikuwa ni kama Illuminati ya leo ambayo watu wengi leo wamejiunga nayo kwa manufaa yao wenyewe.
Baali alikuwa ni kama majini ya leo ambao wengi leo wameyafuga kwa manifaa yao wenyewe.
Baali alikuwa ni kama uchawi wa kienyeji ambao wengi leo wanautumia kwa manufaa yao wenyewe.
Baali alikuwa ni kama uasherati/ uzinzi wa leo ambapo watu wengi sana wamejiunga nao pasipokutaka kubadilika wamwabudu MUNGU wa kweli Yehova.
Taifa hili la MUNGU lilikuw limemgeuka na kumwacha MUNGU wa kweli Yehova na kukosautii kwake na ndipo angawaje MUNGU angekuwa na rehema kwao kama wangemrudia; alikuwa tayari kuwasamehea.
Kuna kizazi cha watumishi wa MUNGU leo ambacho MUNGU amekiibusha ili kije kiiokoe miji fulani iliyomwacha MUNGU .
Kuna kizazi cha watumishi wa MUNGU leo kimetumwa kubadilisha vijiji fulani vilivyomwasi MUNGU wa kweli.
Kuna kizazi cha watumishi wa MUNGU ambacho kimeibushwa ghafla na MUNGU kiokoe taifa liliko katika maangamivu makuu kwa kumwacha MUNGU wa kweli na kuabudu mapepo.
Kuna kizazi cha watumishi wa MUNGU ambacho kimeibushwa na MUNGU ghafla kuwaficha watumishi wa MUNGU ambao mwabudu shetani Yezebeli ameapa kuwamaliza.
Kumbukumbu 12:30 "Jiadharini msijiingize mtegoni kwa kuyafuata baada ya kuangamizwa.Msijisumbue kwa kujua miungu yao mkisema mataifa haya yaliabuduje miungu yao? Ili nasi tuabudu hivyo?
Mtu wa MUNGU ninao ujumbe kwako ambao MUNGU amenituma kabla ya majanga kukupata.Kama utatii utaishi; usipotii utaangamia.
Mrudie MUNGU wako leo maana ni wa rehema na ukimrudia na kutubu dhambi zako atakusikia na kukusamehea wewe ni mwanaye.
2 Nyakati 7:14 "Kama watu wangu wanaoitanishwa na jina langu wakijinyenyekeza mbele zangu wakiomba, watubu na kuziacha dhambi zao nitawasi


Kwa msaada wa ushauri na maombi;
Geoffrey Mwanza Wambua,
The Global Evangelism Ministries (Kenya)
+254 724 656 653
geoffreymwanza@yahoo.com

Comments