KWANINI YESU KRISTO? NI KWA SABABU YA UZIMA WA MILELE

Na Peter Mabula, Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Siku moja mchana nilisikia sauti ikiniambia ''KWANINI YESU KRISTO? ''
Nikataka kujibu lakini kabla sijajibu ile ile sauti ikaniambia kwamba ''NI KWA SABABU YA UZIMA WA MILELE''
Nilitiwa nguvu sana kwa sauti hiyo ya live niliyoisikia, kwa sababu kila ninachoambiwa na ROHO wa MUNGU huwa nakiandika basi niliandika haraka haraka ujumbe ule na kuendelea kuutafakari kwamba ''Kwanini YESU KRISTO? Ni kwa sababu ya uzima wa milele.''

1 Yohana 2:21-25 ''Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli.  Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa YESU ni KRISTO? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye BABA na MWANA.  Kila amkanaye MWANA, hanaye BABA; amkiriye MWANA anaye BABA pia. Ninyi basi, hilo mlilolisikia tangu mwanzo na likae ndani yenu. Ikiwa hilo mlilolisikia tangu mwanzo linakaa ndani yenu, ninyi nanyi mtakaa ndani ya MWANA, na ndani ya BABA. Na hii ndiyo ahadi aliyotuahidia, yaani, uzima wa milele.'' 

Tukimtaja YESU KRISTO tunakuwa tunamtaja aliye pekee anayeweza kuwapeleka wanadamu uzima wa milele.
Tukimpokea YESU KRISTO tunakuwa tumepokea uzima wa milele ambao uko tayari kwa ajili yetu kama tu tukidumu katika utakatifu wake KRISTO.
Linapotajwa jina la YESU maana yake hapo panatajwa uzima.
Ndio maana uponyaji hutokea baada ya jina la YESU KRISTO kutajwa.

Ona mfano huu wa nguvu za jina la YESU KRISTO;
''Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu MUNGU. Watu wote wakamwona akienda, akimsifu MUNGU. Wakamtambua, ya kuwa yeye ndiye aliyekuwa akiketi na kuomba sadaka penye mlango Mzuri wa hekalu; wakajaa ushangao wakastaajabia mambo yale yaliyompata-Matendo 3:6-10''

Kumjua YESU KRISTO ni ufunuo.
na huwezi kumjua vizuri YESU KRISTO ukiwa nje na yeye.
Ingia ndani ya YESU kwanza ndipo utamjua YESU kwa usahihi.
Unaweza Ukakusanya Majibu Mengi Juu Ya YESU Lakini Katika Majibu Yako Hayo Yote Kusiwepo Jibu Sahihi. 
Okoka Kwanza Ndipo Ujifunze Mafundisho Sahihi Kanisani Ndipo Utamjua BWANA YESU Mwenye Uzima Wa Milele Kwa Wote Wanaomtii Na Kutii Neno Lake.
 Huwezi Kuwa Mkristo Kama Huna KRISTO Ndani Yako.
 Kama Huna KRISTO Ndani Yako Wewe Sio Mkristo Labda Mkristu Tu.

 Japokuwa Mbinguni Ni Mbali Sana Lakini Kuna Watu Watafika Huko Kirahisi Sana Kwa Sababu Tu Wamemtii YESU KRISTO Na Injili Yake Ya Uzima.
Matendo 4:12 ''Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.''

 Kumbe ni kwa jina la YESU tu tunaokolewa.
Kuokoka ni kuchagua uzima wa milele ambao uko katika KRISTO pekee.
Kuishi maisha matakatifu ndani ya KRISTO ni kuubeba uzima wa milele.
Kuishi maisha ya matakatifu ya wokovu ni kama kutanguliza mwili wako uzima wa milele.


 Anayetaka Kumfuata YESU Anatakiwa Kumfuata YESU Siku Zote. Usimfuate BWANA YESU Kwa Sababu Una Shida Na Matatizo Bali Mfuate BWANA YESU Kwa Sababu Unautaka Uzima Wa Milele.

 Kumchagua YESU KRISTO Ni Kulichagua Fungu Lililo Jema. Kumchagua YESU KRISTO Ni Kuuchagua Uzima Wa Milele.

 Katika Maisha Yako Mtu Wa Kwanza Kumuona Kwa Macho Yako Na Kumfahamu Ni Nani? Bartimayo Yeye Katika Maisha Yake Mtu Wa Kwanza Kumuona Na Kumfahamu Ni BWANA YESU Baada Ya Kumponya. 
Kumuona BWANA YESU Ni Uzima.

Warumi 6:23 '' Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU BWANA wetu.''

Ukurasa Wa Wanaotakiwa Kuokoka Duniani Bado Umefunguliwa. Kuna Siku Ukurasa Huo Utafungwa Na Wakati Ukurasa Huo Unafungwa Utafunguliwa Ukurasa Mwingine Wa Hukumu.
 Ndugu Zangu Kuokoka Ni Leo.
 BWANA YESU Anaokoa Leo, Ukimpokea Leo Unaokoka.

Warumi 10:17 ''Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la KRISTO.''

Imani ya kweli  na ya uzima wa milele ni moja tu, ni imani ya kumpokea BWANA YESU pekee kama Mkombozi wako.
Mtaji wa Mkristo ni imani.
Imani ni uhakika wa mambo yajayo.

Tunapokea Wokovu wa KRISTO kwa imani.

 Kumpokea YESU ni kupokea nguvu za kimbingu za ulinzi na uzima.
Kuna Watu Huwatupia Watu Wengine Maneno Mabaya. 
Kuna Watu Hutupiwa Maneno Mazito Ili Wateseke. 
Ndugu, Je Umewahi Kuyapangua Maneno Mabaya Uliyotupiwa Na Watesi Wako? Damu Ya YESU KRISTO Ina Uwezo Pekee Wa Kufuta Maneno Mabaya Yote Haijalishi Aliyatamka Ni Nani. 
Damu Ya YESU KRISTO Ina Uwezo Pekee Wa Kufuta Laana Zote Haijalishi Laana Hizo Kazitamka Anayemiliki Majini 700 Na Ana Hirizi 200 Mwilini Mwake.
Kuna faida kuu ya ya milele ndani ya jina la YESU KRISTO.

 Tazama yuaja Mwana Wa Adamu.
Kila jicho litamuona Mwokozi YESU.
Kila ulimi utakiri YESU KRISTO ni BWANA.
Ni saa ya wokovu sasa.

Ufunuo 1:7-8 '' Tazama, yuaja na mawingu; na kila jicho litamwona, na hao waliomchoma; na kabila zote za dunia wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana MUNGU, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.''


 Huwezi Kukutana Na BWANA YESU Ana Kwa Ana Ukabaki Vile Vile. Kupitia Kumpokea YESU Kama BWANA Na Mwokozi Wa Maisha Yako Hakika Utakutana Naye Na Atakupa Uzima Sasa Na Uzima Wa Milele, Changamka Ndugu Kama Uko Mbali Na Wokovu.

  Jambo jingine la kujua ni kwamba Kwa Sasa BWANA YESU Ni Mwokozi Lakini Siku Inakuja Ambapo BWANA YESU Atakuwa Hakimu Ili Kuwatenga Waliomtii Na Wadhambi. Waliomtii Na Kulitii Neno Lake Wataenda Uzima Wa Milele, Na Waliomkataa(wadhambi) Wataenda Jehanamu. 

 Isaya 13:9 ''Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.''

Dunia Nzima Leo Inasubiria Kuja Kwa BWANA YESU Lakini Wengine Wanasahau Kwamba Atakuja Kama Hakimu, Kwa Msaada Zaidi Leo Soma Mathayo 24 Yote. 
Ukitaka BWANA YESU Awe Mwokozi Wako Basi Okoka Kwa Kumpokea Ukiwa Hai Na Kuanza Kuishi Maisha Matakatifu, Lakini Kama Unamkataa Na Wokovu Wake Na Unaendelea Na Dhambi Hakika Subiria Kumuona BWANA YESU Akija Kama Hakimu. Ni Heri Kila Mmoja Wetu Leo Amkimbilie BWANA YESU Kwa Kuokoka. 
Biblia inasema ''Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. 1 Yohana 1:9  ''
 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments