MTAKATIFU, MTAKATIFU, MTAKATIFU NI BWANA WA MAJESHI; DUNIA YOTE IMEJAA UTUKUFU WAKE.

Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe mpendwa upendwae sana na MUNGU.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.


Isaya 6:3 ''Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.''

MUNGU wetu ni mtakatifu.
MUNGU ameumba watakatifu wote.
MUNGU wetu ni mtakatifu wa watakatifu na anataka na sisi tuwe watakatifu.
kuiabudu miungu ni kuukimbia utakatifu halisi maana utakatifu wa kweli una MUNGU wa mbinguni tu.
MUNGU wetu yu juu ya yote.


Zaburi 83:18 ''Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye juu, juu ya nchi yote.''

Yeye MUNGU wetu yuko juu ya wote na juu ya vyote.
Yeye ana mamlaka yote na uwezo wote.
Hakuna anayeweza kushindana naye.
MUNGU wetu anaagiza leo kwamba inatupasa mimi na wewe tuwe watakatifu maana utakatifu ni tabia ya kiMUNGU.
Ni muhimu ndugu ukaishi maisha matakatifu.


Kutoka 15:11 ''Ee BWANA, katika miungu ni nani aliye kama wewe? Ni nani aliye kama wewe, mtukufu katika utakatifu, Mwenye kuogopwa katika sifa zako, mfanya maajabu? ''

JEHOVAH ni MUNGU mtakatifu na hachangamani na uovu.
Tukitaka tumbariki MUNGU wetu basi jambo la kwanza inatupasa tuwe watakatifu.
Utakatifu katika KRISTO ndio ufunguo wa uzima wa milele.
Utakatifu ndio msingi mkuu wa baraka zetu.


1 Petro 1:15-19 '' bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya KRISTO. ''

MUNGU ni mtakatifu na anataka siku zote na sisi tuwe watakatifu.
Utakatifu ni silaha kuu ya sisi kutembea na ulinzi wa MUNGU.
Mbinguni kuna watakatifu tu hivyo yatupasa tuwe watakatifu ili tufike huko.

Pasipo utakatifu haiwezekani kumuona MUNGU.

Waebrania 12:14 ''Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona BWANA asipokuwa nao; ''

Utakatifu ni vazi la mteule, ni vazi safi la kuvaa siku zote.
Mambo yako mengi yanaweza kwenda vibaya kwa sababu tu huishi maisha matakatifu.
Biashara yako inaweza kugoma kuleta faida kwako kwa sababu tu huishi maisha matakatifu.
Tukihitaji MUNGU atubariki basi tunatakiwa tuwe watakatifu daima.


Mathayo 5:8 ''Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona MUNGU.'' 

Utakatifu hauna kipande bali umekamilika.
Huwezi kuwa mtakatifu katika jambo moja kisha jambo jingine ukawa sio mtakatifu. hiyo haipo na haiwezekani.
Utakatifu ni wa muhimu sana katika maisha ya waenda mbinguni.
Utakatifu wa kweli unatoka kwa YAHWEH MUNGU wetu.
Utakatifu kwa mkristo ni jambo la lazima ili kuipalilia taji yake ya uzima.


Wakolosai 1:21-22 '' Na ninyi, mliokuwa hapo kwanza mmefarikishwa, tena adui katika nia zenu, kwa matendo yenu mabaya, amewapatanisha sasa;katika mwili wa nyama yake, kwa kufa kwake, ili awalete ninyi mbele zake, watakatifu, wasio na mawaa wala lawama; ''

Utakatifu kwa wanadamu chanzo chake ni KRISTO.
Hakuna mtu mtakatifu nje na KRISTO.
Utakatifu unanza kwa kumpokea YESU KRISTO kama Mwokozi wako.
Kumpokea YESU ndio mwanzo wa utakatifu wako.
Kuokoka ndio mwanzo wa kuabudu na ndio mwanzo wa kuwa mtakatifu.
MUNGU anapendezwa na watakatifu walioko duniani.

Ukitaka kukubaliwa na MUNGU basi anza leo kuishi maisha matakatifu.

2 Kor 7:1 ''Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha MUNGU. ''


Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.

Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments