SALVATION DAY IMEKARIBIA, NI TAREHE 10/7/2016


Baada ya Kimya kilefu sasa mwimbaji wa Salvation Music aamua kuwaunganisha waimbaji na wachungaji wafanye kazi ya Mungu kwa umoja,pamoja na lawama zinazosemekana kuwa waimbaji wengi hupenda pesa kwenye kutoa huduma ya bure wamejikuta wakitumbukia kwenye misingi mibovu,kitu ambacho mwimbaji huyo ameamua kuanzisha huduma ya Siku ya Wokovu (Salvation Day) ambayo ni huduma ya kufikia jamii na kuipa mafundisho ya Neno la Mungu ambalo ndilo kusudi kuuu la Mungu ili kila mwana Damu apate toba na kuupokea Wokovu,kadri siku zinavyo kwenda ndivyo shauku ya wengi inavyokaribia kukutana na Mungu siku ya Tarehe kumi mwezi wa saba ambapo waimbaji watafurika na makanisa mbalimbali na wachungaji na maasikofu kumuita Mungu ashuke kwa Nguvu zake kuponya na kuharibu makazi ya shetani ndani ya wenye dhambi na vifungo.

 KATIKA SIKU YA SALVATION DAY
MEMA YOTE YALIYOKUFA MAISHANI MWAKO YATAFUFULIWA KWA JINA LA YESU.
Shetani hana jipya kwa Mungu.
Tarehe kumi mwezi wa saba ni siku ya kuponda kazi za kuzimu na kuinuliwa kwa jina la Yesu kwa Utukufu wa Mungu, uliyemezwa na mashetani siku ya Wokovu ikawe uhuru kwako, kwa wewe mwenye Mungu mwambie mwenzio kuwa hii ni siku ya maajabu ya Mungu wa Kweli.Tatafanya mambo ambayo huwezi kuamini hata ukiambiwa.
Habakuki 1:5


 Kama ni Mungu basi muombe siku hii usikose kufika kujionea yatakayofanyika ndani ya Ibada hii maalum ya kuweka Wakfu huduma ya Salvation Day (Siku ya Wokovu) ambayo itafanyika pale Mbagala siku ya tarehe 10/7/2016 waimbaji wengi watakuwepo na vipovitu vingi vya tofauti, Maombi na maombezi ndiyo dhima kuu nikumwabudu Mungu na kumuita ashuke na kuokoa pamoja na kuponya. usikose.

 Salvation Day iwe siku yako ya kufurahi na kumshukuru Mungu kwa maana fadhili zake kwetu hazikomi,wapo waimbaji wengi watakuwepo wengine hawajawekwa hapo kama Moses Salamba na Neema Decoras Calvary Brothers, Betheli Kwaya, Eben Ezer kwaya, Elliya Alex, Zacharia Kenyatta na wengine wengi.

Mwimbaji Nguli wa Nyimbo za Injili Steven Dayos

Comments