SIRI YA USHINDI YA WATEULE WA MUNGU.

Na Peter Mabula, Mtenda kazi katika shamba la BWANA.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la uzima.

Warumi 8:36 '' Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.'' 

 Hakika MUNGU ametupenda na kwa yeye tunashinda na zaidi ya kushinda.
 Adui ana mipango mibaya kwa kanisa siku zote  lakini habari njema ni kwamba tunashinda na zaidi ya kushindi kwa sababu ya YESU KRISTO aliyetupenda.
=Kupitia maombi yetu tunashinda.
=Kupitia utakatifu tunashinda.
=Kupitia utoaji wetu kwa MUNGU tunashinda.

Hakika tunashinda na zaidi ya kushinda maana tuko na KRISTO aliyetupenda tangu zamani.
je umewahi kujiuliza kwamba, Kama Kila Mipango Ya Adui Dhidi Yako mteule  Ingekuwa Inatimia Hakika usingekuwepo Duniani. Adui Wanaweza Wakapanga Mabaya 7 Kwa Ajili Yeko  Lakini Mabaya 5 Katika Hayo Hayatatupata Na Mabaya 2 Yaliyobaki Yaliyo Mabaya Zaidi Huwarudia Wao Waliotuma Maana Damu Ya YESU KRISTO Ni Ukuta Mkubwa Sana Unaotukinga Na Kila Mishale Ya Adui Dhidi Yetu, Na Maombi Yetu Na Utakatifu Ndivyo Humfanya MUNGU Wetu Kufuta Mabaya Hayo Na Mengine Kuwarudishia Waliotuma Ili Wawe Na Adabu Na Wajue Kwamba Sisi Ni Sanduku La Agano La MUNGU. 
Ndani Ya Sanduku La Agano Kuna Sheria Ya MUNGU, Neno La MUNGU Na Nguvu Za MUNGU. 
Najisikia Raha Kuokoka Maana Ukiokoka Unakuwa Sanduku La Agano La MUNGU. 
Ashukuriwe MUNGU Wa Mbinguni Kwa Kutuletea Uzima Na Ushindi Kupitia Damu Ya YESU KRISTO Na Jina La YESU KRISTO.

Zaburi 60:12 '' Kwa msaada wa MUNGU tutatenda makuu, Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.'' 


Hakika MUNGU atawakanyaga watesi wetu ila kama tu tuomba kupitia jina la YESU KRISTO.
Siri kuu za ushindi wa watu wa MUNGU ni maombi, utakatifu na utoaji.
Kama umeona hushindi nakuomba zingatia hayo matatu hakika utashinda.

Mathayo 7:7-11 ''Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana BABA yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao? ''
   Ndugu zangu naomba nitoe maangalizo haya;
Watu Wengi Huharibu Siku Zao Za Maisha Kwa Jinsi Wanavyoianza Siku Kwa Njia Isiyofaa Na Kwa Jinsi Wanavyoimaliza Siku Kwa Njia Isiyofaa. Wewe Huwa Unaianzaje Siku Yako? 
Na Je Huwa Unaimalizaje Siku Yako?
Ni muhimu kuianza siku yako na MUNGU kwa maombi na maliza siku yako kwa maombi.
Anza siku yako na utakatifu na imalize siku yako na utakatifu.
Anza siku yako ukiwa na BWANA YESU na maliza siku yako ukiwa na BWANA YESU.

Isaya 1:19-20 ''Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.''
  Jambo jingine ni kwamba ;
Wabaya Sio Wote Lakini Wapo. 
Usikubali Kuwapa Siri Zako Watu Wote Lakini Pia Usiache Kumwambia Mwanamaombi Wa Kweli Atakayekuombea Ili Uvuke Salama.
Kwa sababu siri ya ushindi ya watu wa MUNGU ni maombi basi hakika ni muhimu mtu wa MUNGU kuwa muombaji.
Wakati mwingine unaweza ukasikia himizo la kufunga, ndugu, nakuomba funga ndugu.
Wakati mwingine unaweza kukumbana na vita vikali, ndugu, nakuomba shirikisha waombaji wengine maana ninachojua ni kwamba katika maombi kuna siri kuu ya ushindi ya wateule wa KRISTO.
BWANA YESU anasema '' Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya MWANA. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.-Yohana 14:13-14 ''


 Ni Kweli Kuna Wakati Wa Maadui Kuwa Wengi Sana, Lakini Ashukuriwe BWANA YESU Maana Pia Kuna Wakati Wa Adui Hao Kupigwa Na Kuharibiwa, Kuteketezwa Na Mahali Pao Hapataonekana Tena.

Warumi 16:20 ''Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.] ''

  Jambo jingine naomba tujue kwamba kuna wakati wa kupitia majaribu ambayo yakipita yanatupandisha viwango vya imani na viwango vya baraka pia.
Jaribu kama hilo  Unatakiwa Ulishinde. 
Hilo Jaribu Ni Saizi Yako Ndio Maana Limekuja Kwako. Lisingekuwa Saizi Yako Wala Lisingekuja Kwako, Lakini Kwa Sababu Jaribu Hili Ni Saizi Yako Ndio Maana Limekuja Kwako Lakini Biblia Inasema Inakupasa Ulishinde Jaribu Hilo. 

Yakobo 1:2-3 ''Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.'' 

Najua Hakuna Jaribu Lisilo Na Mlango Wa Kutokea. 
Kama Hujaona Mlango Wa Kutoka Kwenye Jaribu Hilo Hakika Ongeza Maombi Na Unyenyekevu Kwa BWANA YESU Ndipo Utaona Mlango Wa Kutokea Na Hakika Utatoka Salama Ukiwa Mshindi.
 Ni Kweli Kuna Wakati Wa Huzuni Kubwa Kwa Sababu Ya Yanayoonekana, Lakini Pia Ashukuriwe YAHWEH Maana Kuna Ushindi Mkuu Ambao Hutoka Katika Kutoonekana Na Kuwa Kuonekana.

Jambo jingine kujua ni kwamba Kama utakuwa na wasiwasi juu ya kupokea kile unachoomba kwa MUNGU hakika wasiwasi huo utasababisha nguvu za MUNGU zisifanye kazi yake vizuri.
Kama akili yako inaamini ukiomba kwa kitu A utapewa, sasa hicho A unacho na sasa maombi yako unaomba upate kitu B na C lakini huamini kama utapewa vitu hivyo. Je kwanini usiache kuomba vitu hivyo hadi Siku ukiamini kwamba hata hivyo BWANA anaweza kukupa?
Kutokumwamini MUNGU katika maombi kama atakujibu hitaji lako ni kupunguza kupokea hitaji hilo.

 Neno La MUNGU Huwa Halijikani. 
Wanaweza Wanadamu Wakalikana Neno La MUNGU Lakini Hiyo Hailiondoi Neno La MUNGU Katika Nafasi Yake Kwamba Ni Neno La MUNGU. 
Neno La MUNGU Huwa Ni Jepesi Sana Kama Ukiamua Kulitii Lakini Neno Hilo Linaweza Kuwa Mwiba Mkali Kwako Kama Hulitii. 
Ndugu, Litii Neno La MUNGU. 
Ndani Ya Neno La MUNGU Kuna Mpango Wa MUNGU Na Nguvu Za MUNGU. 
KRISTO Ni Neno Juu Ya Neno La MUNGU Ndio Maana Hapo Mwanzo Kulikuwako Na Neno, Na Kwa Neno Vyote Viliumbwa. Neno La MUNGU Ni Uzima. 
Mtii MUNGU Kupitia Kulitii Neno Lake Biblia
 Yakobo 4:7-10  ''Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni MUNGU, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa hamu. Jidhilini mbele za BWANA, naye atawakuza.'

Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments