TABIA HIZI MPAKA LINI??

Bwana YESU asifiwe wapendwa....
Kumekuwa na vitabia vya kijinga sana katika nyumba za ibada. Hizi tabia zina kera sana na zina dhalilisha. Tabia hizi ni pamoja na:
1. Mtu kujipiga picha wakati ibada inaendelea. Wengine hupiga selfie wakati mahubiri au nyimbo za kusifu na kuabudu zina endelea.
2. Kupiga story na hasa umbea umbea wakati wa ibada.
3. Kuvaa mavazi ya ajabu ajabu na hasa wasichana kuvaa vinguo vifupi! Au kuvaa nguo zenye maandishi yanayo pingana na imani ya muhusika!
4. Kuchelewa kanisani, na hasa wasichana alafu unakuta kavaa kiatu ambacho kinapiga kelele, alafu anakatisha katikati ya kanisa ili akakae mbele!
5. Mwingine amekariri "kiti cha kukaa". Akikuta siku nyingine mtu mwingine amekalia kiti hicho inakuwa ugomvi!
6. Unakuta Mchungaji anahubiri, kisha ana kemea labda tabia ya Ulevi alafu mtu uliye kaa naye jirani anakutazama wewe alafu anakuuliza "hapo vipi kwenye katabia ka Ulevi "?.. Sijui anategemea umjibu nini na ili iweje!
7. Unakuta mwanamke ana mtoto mtundu au mtoto anaye lia lia ovyo ovyo, kisha anamuachia mtoto alie tu au asumbue wengine!
ZIPO tabia nyingi za aina hii lakini hizi ni mifano, kama nyingine unazijua ZITAJE..
Mtumishi Charles Francis.

Charles Francis aliyeweka vidole mashavuni.

Comments