THE VOICE NA WENGINE WENGI KUFANYA MAAJABU SIKU YA SALVATION DAY .

Kundi la The Voice, hawa watakuwepo katika Salvation Day kumtukuza MUNGU.
THE VOICE WATAFANYA MAAJABU YA AKAPELA SIKU YA SALVATION DAY PAMOJA NA Edna S. Kuja,Sifaeli Mwabuka,Jerome Magassa,Moses Salamba,Neema Ng'asha,Christopher Paul,George Haule, Buruno Kayenzi,Gift George,Neema Decoras pamoja na wengine wengi, bila kusahau kwaya na waimbaji watakao onyesha vipaji vyao ili Enzi Recods ikawalee kwa umoja na Salvation Day ambayo nao watakuwa watumishi pamoja nasi. Maandalizi yanaenda vizuri vyombo vitakuwa vya nguvu, ma-producers wengi kama vile C9, Amyz,Beny Chaila watakuwepo, na Waandishi mbalimbali kutoka TBC,watakuwepo kuhakikisha ambaye hukufika ukajionee historia,na waalimu wa Mambo ya Sayansi ya maendeleo ya jamii na Ubunifu watakuwepo kufundisha namna itupasavyo kuamka tufanye kazi kwa kumwamini Mungu,ili hata kama hujaokoka siku hiyo njoo Uokoke,SENIOR TAX OFFICER wa TRA, Bwana Haule atakuwepo atapata nafasi ya kusema na watanzania kwa kina sana, hii isikupite, kutakuwepo wamiliki wa Makampuni yanayohusika na mambo ya Sanaa nao watasema jambo, tunataka tujenge Muziki wetu kwa ufanisi. Mambo yote yatafanyika lakini usisahau ya kwamba siku hiyo Albamu ya Rudi by Mr. Dayos itaachiwa Rasmi kufikia jamii zote kwa mfumo wa Audio CD.

Ndugu mpendwa nakuomba usipange kukosa siku hiyo tarehe 10 Mwezi huu.

Edna Kuja atakuwepo ni mmoja katika  waimbaji wengi watakaokuwepo Salvation Day Kumtukuza MUNGU.

Comments