TUBU ILI ZIJE NYAKATI ZA KUBURUDISHWA.

Na Peter Mabula, Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe mpendwa..
Ni siku nyingine tena nakukaribisha tujifunze Neno la MUNGU la uzima.

Matendo  3:19 '' Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;''

Agizo la kutubu sio la kujitungia Mwanadamu ila ni agizo la MUNGU.
Umuhimu wa kutubu ni mkubwa sana kwenye ulimwengu wa roho na kwenye ulimwengu wa mwili.
Maisha ya toba ni maisha ya kutubu dhambi na kuziacha.
Toba huleta mtazamo mpya kwa MUNGU.
Toba hubeba muonekano mpya kabisa kwa anayetubu.
Usije hata siku moja ukajihesabia haki  kwamba huna jambo la kutubia maanadamu unaishi duniani.

Yakobo 3:2 ''Maana twajikwaa sisi sote pia katika mambo mengi. Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, awezaye kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu.'' 


Inawezekana kabisa hujafanya dhambi lakini umefanya kosa maana kosa sio dhambi ila dhambi zote ni makosa(siku moja nitafafanua katika somo kamili kuhusu dhambi na makosa)
Inawezekana hujafanya dhambi lakini umenajisika kwa sababu fulani.
Unaweza usiwe na dhambi lakini unajisi wa ukoo au familia uko kwako. 
Tunaishi katika dunia iliyo na machukizo mengi hivyo japokuwa hatuyatendi machukizo hayo lakini kama sehemu ya  jamii yanaweza kutuadhiri pia kwa nanma moja au nyingine.
Kuna mambo ya kitaifa au kimazingira au kiukoo au kijamii yanaweza yakauondoa utukufu wa MUNGU kwako hivyo toba tu ndio inayoweza kuurudisha utukufu wa MUNGU kwako.
Utukufu wa MUNGU ni kuonekana kwa MUNGU kwako kupitia matendo makuu.

Warumi  3:23-26 '' kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa MUNGU; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika KRISTO YESU; ambaye MUNGU amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa. apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye YESU.''

Madhara mojawapo ya dhambi ni kuondoa utukufu wa MUNGU.
Lakini mwanadamu akiamua kutubu na kugeuka kupitia YESU KRISTO anasamehewa.
Kutubu ni muhimu sana hakika.
Kutubu Ni Kumruhusu MUNGU Akuangalie Kwa Jicho La Huruma Na Kukusaidia. 
Naomba kila mtu ajue hili kwamba wakati mwingine mabaya yanayotukabili ili yaondoke na kuja mema inahitajika toba ya kweli.
Inawezekana hujui kosa lako ni nini lakini hata kuutumia muda wako vibaya hadi adui akakuweza hilo ni kosa na linahitaji toba.
Mifano hai ni hii;
Watu Wengi Baada Ya Kuachwa, Kufukuzwa Kazi, Kuwa Na Migogoro Kwenye Ndoa, Kuugua Au Kuingia Katika Matatizo Hukimbilia Kulaumu Na Kujihesabia Haki Lakini Matatizo Yao Hayatoki Na Wanashindwa Kujua Wafanye Nini. 
Siri Kuu Na Ya Mwisho Iliyo Ya Muhimu Ni Maombi Ya Toba. Kama Huoni Umuhimu Wa Kutubu Basi Hakika Utakuwa Pia Huoni Umuhimu Wa Tatizo Lako Kuondoka. 
Ndugu, Kutubu Ni Kumruhusu MUNGU Akushindie. 
 Hata Kama Unajiona Ni Mtakatifu Lakini Kama Umeingia Matatizoni Na Hujui Chanzo Cha Tatizo Basi Tubu Maana Inawezekana Hukukaa Katika Nafasi Yako Ya Maombi Kama Mteule Wa KRISTO Ndio Maana Adui Akapata Nafasi Kwako. Inawezekana Ulimwibia MUNGU Zaka Na Dhabihu, Inawezekana Ulidhulumu Au Uliiba. Tubu Ndugu Na Usitende Dhambi Tena.

 2 Petro 3:9 '' BWANA hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba. ''

 Kuna Watu Wamegeuza Makanisa Kama Vichaka Vyao Vya Kuficha Maovu Yao. 
Kuna Ambao Hata Huhubiri Madhabahuni Kama Njia Bora Ya Kuficha Uovu Wao. 
Kuna Ambao Huimba, Hujitoa Kipesa Na Ni Viongozi Wakubwa Makanisani Lakini Yote Hayo Ni Kichaka Cha Kuficha Uovu Wao. ROHO Wa MUNGU Amewaonya Mara Nyingi Sana Ila Bado Wameshupaza Shingo. 
Ndugu Zangu Hakuna Hatari Mbaya Kama Hiyo. 
Wakati Wa Kugeuka Na Kuacha Dhambi Ni Leo.

Mathayo 3:2 " Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."

 Unaisaliti Ndoa Yako Na Unaona Ni Sawa Tu. Lakini Napenda Kukuambia Kwamba Waliokuwa Wasaliti Wengi Leo Wako Kuzimu Matesoni Kwa Sababu Ya Usaliti Wao, Wameikosa Mbingu Mpya Kwa Sababu Ya Dhambi Ya Usaliti. 
Ndugu Zangu Saa Ya Kutubu Na Kugeuka Ni Leo Na Sio Kesho.

Zaburi 34:14 ''Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.''

 Ni Muhimu Sana Kuacha Dhambi Za Sirini Maana Mwisho Wa Dhambi Ni Jehanamu Na Sio Mbinguni. 
Kuokoka Ni Leo Wala Sio Kesho Maana Kuna Wengine Waliitarajia Kesho Yao Ndipo Waokoke Lakini Hasara Ni Kwamba Kabla Ya Hiyo Kesho Watu Hao Walikuwa Wameshaondoka Duniani. 
Kwa Maamuzi Ya Kuokoka Leo Ni Muhimu Kuliko Kesho.

Isaya 55:6-7 '' Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie BWANA, Naye atamrehemu; Na arejee kwa MUNGU wetu, Naye atamsamehe kabisa.''

Kama kuna jambo muhimu unalohitaji basi ni kufundishwa toba ya msamaha.
 Kuna Watu Wanataka Injili Za Mikate Na Samaki Tu Ila Hawataki Injili Ya Wokovu Wa KRISTO Inayowataka Kuacha Dhambi. BWANA YESU Anasema Tubuni Maana Ufalme Wa MUNGU Umekaribia.
Baraka zipo tu na zitakuja lakini uhusiano na MUNGU ndilo la muhimu zaidi kwetu.
dhambi hufuta uhusiano wetu na MUNGU lakini toba ya kweli huurejesha uhusiano wetu na MUNGU.

Marko 1:15 ''Wakati umetimia, na ufalme wa MUNGU umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. ''

 Una mambo mengi ya kutubu kwayo ndugu.
Mfano MUNGU Akiiangalia Imani Yako Ataikuta Imesimamia Kwenye Nini?. 
Kuna Watu Imani Zao Zimesimamia Kwenye Vyakula, Kuna Watu Imani Zao Zinasimamia Kwenye Baraka. 
Kuna Watu Imani Zao Zimesimamia Kwenye Siku, Kuna Watu Imani Zao Zimesimamia Kwa Mwanzilishi Wa Dhehebu, Kuna Watu Imani Zao Zinasimamia Kwa Mchungaji Au Askofu Wao. Lakini Napenda Kukuambia Kwamba Watu Muhimu Zaidi Ni Wale Ambao Imani Yao Imesimama Katika KRISTO Pekee. Hawa Wanaupendeza Na Kuubarikiwi Moyo Wa MUNGU.

1 Petro 3:10-12 '' Kwa maana, Atakaye kupenda maisha, Na kuona siku njema, Auzuie ulimi wake usinene mabaya, Na midomo yake isiseme hila. Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana. Kwa kuwa macho ya BWANA huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya. '' 

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments