USIKUMBATIE DHAMBI BALI IACHE.

Na Peter Mabula, Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU la Msaada.
Kama kuna kitu mwanadamu anatakiwa kukiogopa basi ni dhambi, maana hiyo inaweza kuuondoa uhusiano mzuri kati Mwanadamu na MUNGU  Muumba wake.
Ndio maana Neno la Leo linasema ''usikumbatie dhambi'' 

1 Yohana 3:4-10 ''Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi. Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake. Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki; atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi. Kila mtu aliyezaliwa na MUNGU hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na MUNGU. Katika hili watoto wa MUNGU ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na MUNGU, wala yeye asiyempenda ndugu yake. '' 

 Maana ya dhambi ni uasi kwa MUNGU.
Dhambi ni kutenda tendo ambalo ni machukizo kwa MUNGU.
Dhambi ni kuwaza jambo ambalo ni machukizo kwa MUNGU.
Dhambi ina dawa moja tu ambapo katika andiko hapo juu Biblia inasema YESU KRISTO alidhihilishwa ili aziondoe dhambi.
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi.
Kupitia YESU KRISTO pekee ndipo mwanadamu anaweza kusamehewa dhambi, kama akiamua kutubu na kumpokea YESU.
Dhambi inaweza kufutika kama mwanadamu akiamua kutubu kwa BWANA YESU maana yeye husamehe dhambi.
Sio wote hupenda hutubu ila anayetubu kwa kuamua kutoka moyoni kisha anabadilisha mfumo wake wa maisha kutoka maisha ya dhambi na kuanza kuishi maisha matakatifu katika KRISTO anaokoka.
Watenda dhambi wasio tubu ni muhimu wakatubu maana  hakuna uzima wa milele kwa wadhambi ambao hawakutubu.
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi

Dhambi Moja Tu Ya Siku Moja Tu Inaweza Kukuletea Madhara Makubwa Kwako. 
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Dhambi Moja Tu Ya Siku Moja Tu Inaweze Ikazaa Jehanamu. 
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Dhambi Ya Uzinzi Moja Tu Ya Siku Moja Tu Inaweza Kukufanya Ukabeba Mimba na magonjwa ya zinaa Na Kufuta Mipango Yako Mizuri Ya Maisha Yako.
Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Dhambi Moja Tu Ya Siku Moja Tu Ya Adamu Na Eva Ilizaa Kifo Kwa Wanadamu Wote Hadi Leo. 

Warumi 5:12 ''Kwa hiyo, kama kwa mtu mmoja(Adamu) dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;''

Kupitia Adamu na Hawa dhambi iliingia duniani.
Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Dhambi Moja Tu Ya Wizi Wa Siku Moja Tu Inaweza Ikazaa Kilema Cha Maisha. 
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Dhambi Moja Tu Ya Uongo Inaweza Ikapelekea Wengine Wakafungwa Jela Kwa Sababu Umewasingizia.
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Dhambi Moja Tu Ya Uasherati Wa Siku Moja Inaweza Kukuletea Ukimwi Na Kifo Cha Kabla Ya Wakati.
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Dhambi Moja Tu Ya Rushwa Ya Siku Moja Tu Inaweza Kusababishwa Watu Wengine Wakaumia Na Kuteseka.
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
 Dhambi Moja Tu Uchonganishi Wa Siku Moja Tu Inaweza Ikavunja Ndoa Ya Wapendanao.
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Dhambi Moja Tu Ya Uchawi Wa Siku Moja Tu Inaweza Ikapelekea Ukachomwa Moto Na Wenye Hasira Kali na kupoteza maisha.
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi

 Nakuomba Epuka Dhambi, Ogopa Dhambi, Ikimbie Dhambi, usikumbatie dhambi  Na Usifanye Dhambi Tena. Tubu Na Mtii KRISTO Na Neno Lake(Biblia).

Warumi 6:23 '' Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya MUNGU ni uzima wa milele katika KRISTO YESU  Bwana wetu.''

 Watu wengi wanasumbuliwa sana na dhambi.
Tatizo tu wanaogopa kuwaeleza wachungaji wao ili wawapatanishe na MUNGU kupitia sala ya toba na fundisho la kuwabadilisha, kutoka katika matendo ya dhambi na kuanza kutenda mema.
Ndugu jitahidi sana kushudhulikia dhambi inayokutesa ili uiache, maana dhambi huwa haifutiki kwa kuiangalia bali kwa kutubu na kubadilisha  mfumo  wa maisha kutoka maisha ya dhambi na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Kushughulikia Chanzo Cha Tatizo Ni Muhimu Zaidi kabla ya  Kushughulikia Tatizo Lenyewe.

Mathayo 3:2 '' Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''

Dhambi imekuwa na madhara makubwa hata kwa baadhi ya watumishi ambao huamua kufanya dhambi kwa siri.
Hiyo ni hasara na ni hatari sana maana baada ya kifo ni hukumu. 
Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
 Huduma Nyingi Zimedumaa Kwa Sababu Ya Dhambi Ya Siri. Dhambi Ya Siri Inatafuna Idara Ndani Ya Kanisa. Unakuta Mama Mchungaji Anafanya Yake Na Kuua Kabisa Huduma Ya Mume Wake Mwenye Upako Na Maono Mazuri.  
Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
Unakuta Mwanakwaya Mmoja Anayetegemewa Sana Ni Mzinzi Na Anaua Huduma Nzima Ya Kwaya Kanisani. 
Kwa Sababu Mwanakwaya Huyo Anafanya Dhambi Zake Kwa Siri Sana Hujiona Ni Mtakatifu Tu, Anadhani Ataenda Mbinguni Kwa Sababu Ana Ka Sauti Kazuri Na Hushangiliwa Kila Wiki Kwenye Ibada. 
Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
 Unakuta Mmoja Wa Wazee Wa Kanisa Ni Mdhambi Mkubwa Na Kusababisha Mipango Yote Ya Kanisa Kuharibika, Na Huyu Mzee Wa Kanisa Kwenye Vikao Vikuu Vya Kanisa Kazi Yake Ni Kupinga Kila Mpango Mzuri Unaopendekezwa Na Wenzake. Dhambi Za Siri Zinaumiza Sana Huduma. 
Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
 Ndugu, Ni Wakati Wa Kutubu Na Kuacha Dhambi Za Siri. Kumbuka Baada Ya Kifo Chako Ni Hukumu. 
Dhambi zote kwa MUNGU zinajulikana na hakuna jambo la siri ambalo MUNGU halioni.
MUNGU anasema;
 ''Wala hawafikiri mioyoni mwao ya kwamba naukumbuka uovu wao wote; sasa matendo yao wenyewe yamewazunguka pande zote; yako mbele za uso wangu.-Hosea 7:2 ''

 Kuna Watu Hufanya Dhambi Kwa Siri Sana Na Kujiona Wako Sawa Tu. 
Ndugu, Ni Heri Kufanya Dhambi Zako Hadharani Tu Na Watu Wote Wakujue Kwamba Wewe Ni Mzinzi Au Mwizi Au Dhambi Yeyote Na Kwamba Umemchagua Shetani Na Sio MUNGU. Hakuna Haja Ya Kufanya Dhambi Kwa Siri Wakati Dhambi Ni Dhambi Tu Hata Kama Umeifanya Kwa Siri Au  Hadharani. Malipo Ya Dhambi Ni Jehanamu Tu Haijalishi Ulifanya Dhambi Kwa Siri Au Hadharani. Dawa Ya Dhambi Ni Kuacha Dhambi Na Sio Kufanya Dhambi Kwa Siri Ukidhani Dhambi Hizo Hazihesabiwi Kama Ni Dhambi.
 Ndugu usikubali kukumbatia dhambi
 Ndugu, BWANA YESU Yuaja Na Akija Atamlipa Kila Mtu Sawasawa Na Matendo Yake Yakiwemo Matendo Ya Siri Yote.
BWANA YESU anasema '' Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.-Ufunuo 22:12'' 

 Naamini kabisa kuna kitu umejifunza, lakini lengo la kwanza la MUNGU ni wewe uokoke. Kama unaishi maisha ya dhambi ndugu nakuomba tubu na okoka.
Kama hujampokea YESU nakuomba umpokee leo na uanze kuanzia leo kuishi maisha matakatifu ya wokovu.
Kama wewe ni mtu wa kanisani lakini maisha yako yamejaa dhambi nakuomba okoka upya na amua kumpendeza MUNGU kuanzia leo.
Kama wewe umegeuza kanisa kama kichaka chako cha kuficha uovu wako , nakusihi sana umche MUNGU maana kuna ziwa la moto kwa waovu, lakini pia kuna uzima wa milele kwa wateule wa KRISTO wanaoishi maisha matakatifu.
MUNGU wangu akubariki sana na akupe
ufahamu wa kumjua yeye na Neno lake, akupe
ufahamu wa kuliishi kusudi lake jema kwako.
ubarikiwe sana pia kwa kujifunza masomo
yangu.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments