Huu ni wakati wa kuhubiria watu injili ya kweli

Na Mtumishi Generali Geoffrey Mwanza,
The Global Evangelism Ministries (Kenya)
Bwana Yesu asifiwe?
Huu ni wakati wa kuhubiria watu injili ya kweli na ambayo watu wengi hawaipendi; bali ndiyo injili ya kweli na anayotaka MUNGU wa mbinguni.

Mimi sikuitwa na MUNGU kibahati; wala sikujilazimisha kutumika bali MUNGU alinipa neema yake niutangaze ukweli.Hata ukitaka kuondoa alichotia MUNGU ndani yangu; hebu jaribu kama utaweza!

Wengi hawapendi kukwambia ukweli ila leo iepe sasa nyundu hii ya kichwa nikutambue!
"MUNGU anataka uache dhambi na uyaishi maisha matakatifu ya wokovu ndani ya Bwana Yesu"
Kama kuna mtu amekudanganya kuwa utakuwa na maisha mazuri ukiwa dhambini; nenda umwambie hata yeye kuwa MUNGU anamtaka aokoke!

Kama una pastor wako anayekudanganya kuwa "Utabarikiwa" na huku upo dhambini; nenda umwambie hata naye aokoke au akufe.
Kama una nabii yako ambaye hakuonyi uachane na uasherati huku kila akikuona anakwambia kuwa utabarikiwa nenda umwambie akimbie haraka kwanza aokoke kabla kitabu kifungwe.
Kama kuna mtu anakudanganya heti hatuendi mbinguni kesho na bado kuna muda wa kutubu; nikamatie yeye uniletee tumfundishe Neno sahihi la MUNGU maana huyo amepotea.

Utaendelea kutoa sadaka zako nono na mafungu ya kumi na kujenga makanisa bila kuacha dhambi ukidhani utasaidika kwenda mbinguni; tikiti ya mbinguni ni kuokoka na kuacha dhambi kisha uendelee na kutoa dhabihu zako.
Pengine umesikia Neno hilo na umeanza kujihukumu kwa uovu unaotenda; kisha ungetaka kuokoka nipigie simu:
Generali Geoffrey Mwanza
The Global Evangelism Ministries (Kenya)
+254 724 656 653
geoffreymwanza@yahoo.com

Comments