ILI KANISA LA KRISTO LIKAMILIKE LINAHITAJI YAFUATAYO.

Na Peter M Mabula. Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

ILI KANISA LA KRISTO LIKAMILIKE LINAHITAJI YAFUATAYO.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Maana mojawapo ya Kanisa ni jumuiya ya wamwaminio YESU KRISTO kama Mwokozi wao kisha wanaishi maisha matakatifu.

Yohana 1:12-13 ''Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU.''


Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Kuwe na MUNGU(1 Timotheo 3:15)
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Kuwe na YESU KRISTO(Waefeso 1:20-23)
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Kuwe na ROHO MTAKATIFU(Warumi 8:16)
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Kuwe na Neno la MUNGU yaani Biblia takatifu(Zaburi 12:6)
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Kuwe na huduma tano za ROHO MTAKATIFU.

Waefeso 4:11-12 ''Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa KRISTO ujengwe;''

Huduma tano za ROHO MTAKATIFU kwa kanisa zinahusu Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji Na Walimu.
Hizo huduma tano ni lazima zifanye kazi katika kanisa la KRISTO ili kuwakamilisha watakatifu.
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Kuwe na huduma tano za ROHO MTAKATIFU.
Ili kanisa la KRISTO likamilike ni lazima kuwe na Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu.
Ili Kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Karama Tisa Za ROHO MTAKATIFU Zifanye Kazi.

1 Kor 12:4-11 '' Basi pana tofauti za karama; bali ROHO ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na BWANA ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali MUNGU ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa ROHO kwa kufaidiana. Maana mtu mmoja kwa ROHO apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo ROHO yeye yule; mwingine imani katika ROHO yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika ROHO yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha; lakini kazi hizi zote huzitenda ROHO huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.''

Ili Kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima Matunda Tisa Ya ROHO MTAKATIFU Yafanye Kazi Kwenye Kanisa. 

Wagalatia 5:22-25 '' Lakini tunda la ROHO ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa KRISTO YESU wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Tukiishi kwa ROHO, na tuenende kwa ROHO.''

Point Kuu Ni Kwamba Ili Kanisa La KRISTO Likamilike Lazima Awepo ROHO MTAKATIFU Na Karama Zake, Na Matunda Yake Na Huduma Zake. Tukidumu katika utumishi tutaona faida kuu.
Kuna Vitu Hata Hatutakiwi Tuviombee Kwa MUNGU Bali Kama Tukimtumikia Tu KRISTO Vitu Hivyo Vinakuja.

Jambo jingine hakika unakuwa kiroho ndipo utakuwa kanisa hai la MUNGU aliye hai.
Kila Siku Angalia Hali Yako Ya Kiroho Inaendaje.
Je Unashuka Kiroho Au Unapanda?
Kama Unashuka Ni Kwa Sababu Ya Jambo Gani?
Kwanini Usiliache Jambo Hilo?.
Kama Unapanda Kiroho Ongeza Juhudi Maana Unafanya Vyema. Kumbuka Vyanzo Vikuu Vya Mtu Kukua Kiroho Ni Utakatifu, Maombi Na Kujifunza Neno La MUNGU.
Na Vyanzo Vikuu Vya Mtu Kushuka Kiroho Ni Dhambi, Kuacha Ibada Na Kuendekeza Mambo Ya Kidunia.

Wakolosai 3:16 '' Neno la KRISTO na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia MUNGU kwa neema mioyoni mwenu.''

Inawezekana Wewe Zamani Ulikuwa Mtoto Mchanga Kiroho. Baadae BWANA Akakusaidia Ukakuwa Ukawa Mtoto Mdogo Kiroho.
Kwa Neema Ya MUNGU Baadae Ukakuwa Ukawa Mtoto Kiroho. Haikuishia Hapo Maana Ulikazana Katika Fundisho La KRISTO Ukakuwa Ukawa Kijana Kiroho. Kwa Juhudi Yako Kwa BWANA YESU Hatimaye Umekuwa Umefikia Kiwango Cha Mzazi Wa Kiroho, Yaani Kupitia Ulichofundishwa Kanisani Kwenye Fundisho La KRISTO Sasa Na Wewe Umewazaa Wengi Kiroho Baada Ya Wao Kuokoka Kupitia Fundisho Lako.
Je Wewe Unayesoma Ujumbe Huu Uko Kiwango Gani Kiroho?
Je Ni Mtoto Mchanga, Mtoto Mdogo, Mtoto, Kijana Au Mzazi?
Je Au Umepungua Kiroho Kutoka Kijana Na Sasa Umekuwa Mtoto?
Ndugu, Ongeza Juhudi Katika Kazi Ya MUNGU Na Utakatifu Ili Ukue Zaidi Kiroho.
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima kukua kiroho na sio kudumaa kiroho.

1 Petro 2:2 '' Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;''

Usikubali Kuwa Mtumwa Wa Kitu Kinachoonekana Kwa Macho. Kile Unachokiona Kwa Macho Ndicho shetani Hutumia Ili Kukukamata Ndio Maana Nasema Hivi; Usikubali Kuwa Mtumwa Wa Vitu Vinavyoonekana Kwa Macho.
Tamani kukua kiroho ili iwe msaada kwako kutokuyumbisha na mambo ya dunia.
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima kanisa liwe mbali na dhambi.
Jambo jingine kujua ni hili Hakuna Kitu Kisichokuwa Na Malipo. Dhambi Ina Malipo Na Utakatifu Una Malipo. Aliyechagua Dhambi Atalipwa Na Aliyechagua Utakatifu Atalipwa. Kila Kitu Kina Malipo. Anayefanya Dhambi Asitarajie Kulipwa Mema.
Hivyo jitahidi sana kuishi maisha mataktifu ndipo ukuaji wako wa kiroho utatimizwa.
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima lijitenge mbali na dhambi.
Nataka ujue na hili kwamba Unabii Na Mafunuo Kutoka Kwa MUNGU Vipo Sana, Lakini Wateule Wa KRISTO Tuweni Macho Maana Wakati Mwingine Unabii Kutoka Kwa Shetani Unakuwa Mwingi Sana Pia, Mafunuo Ya Kipepo Yamejazana.
Wengi Wanadanganya Kwa Lengo La Kujitafutia Kipato.
Soma sana Neno la MUNGU na litafakari ili upate ufahamu wa kupamanua jambo la MUNGU na jambo lisilo la MUNGU.
Ndugu, nimuhimu pia kujua kwamba Kulipindisha Neno La MUNGU Ni Kujiweka Hatiani Hata Kama Ujiona Ni Mtakatifu Kama Malaika Watakatifu.
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima litii Neno la MUNGU kama anavyotaka MUNGU na sio kama wanavyotaka wanadamu.
Neno la MUNGU linabaki kuwa Neno la MUNGU tu.
Hatuwezi kulibadili Neno la MUNGU tukafanikiwa. Siku Hizi Wafanyabiashara Wa Injili Ni Wengi Sana.
Ndugu Mtumishi, Ni Hatari Sana Kuigeuza Injili Ya KRISTO Kuwa Biashara. Mpaka Wakupe Hela Ndipo Uwaombee, Waliotoa Pesa Kubwa Ndio Unawaombea Mapema. Unakosea Sana Ndugu.
Ili kanisa La KRISTO Likamilike Ni Lazima liwe na KRISTO YESU na limtii.
Kumkataa KRISTO Ni Kumchagua Shetani.

Waefeso 4:22-24 ''mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. ''

BWANA YESU Amekaribia Kurudi. Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments