Sio sawa kuwafananisha/kuwashindanisha/kuwalinganisha Watumishi wa Mungu

Na Mwl Nickson Mabena
Sio sawa kuwafananisha/kuwashindanisha/kuwalinganisha Watumishi wa Mungu,
Kila Mmoja ameitwa kwa kusudi lake, na kuna namna yake ya kutumika!!.
Wote wanaweza wakawa Wainjilisti, lakini wakatofautiana kwenye WITO, kwa hiyo watatofautiana na eneo la Kutumika,
Vivyo hivyo, wote wanaweza wakawa Wachungaji, lakini wasifanane kwenye namna ya Kutumika, ndio maana hupewa vitu vinavyotofautiana,
Hata Manabii, Waimbaji, na Mitume...
PAULO NA PETRO WOTE NI MITUME, LAKINI WALITOFAUTIANA
Biblia inasema,
WAGALATIA 2:
7 bali, kinyume cha hayo, walipoona ya kuwa nimekabidhiwa injili ya wasiotahiriwa, kama vile Petro ya waliotahiriwa:
8 (maana yeye aliyemwezesha Petro kuwa mtume wa waliotahiriwa ndiye aliyeniwezesha mimi kwenda kwa Mataifa);
9 tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;
USILAZIMISHE PAULO ATUMIKE KAMA PETRO, KISA WOTE NI MITUME..
Hata Mimi ni Mwalimu lakini sifanani na Walimu wengine...!!.
UKIIONA NEEMA NILIYOPEWA, USIACHE KUNIPA MKONO WA KUUME WA SHIRIKA!!!.
Bwana Yesu asifiwe sana...
Naitwa Mwalm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments