YATAMBUE MADHARA YATOKANAYO NA MTU KUFANYA UASHERATI NA JINSI YA KUTOKA KATIKA MADHARA HAYO.


Mwl.na Mwnj . Emmanuel Kamalamo

REDEEMED GOSPEL CHURCH (KITUO CHA MAKIMBILIO)
KIBAHA-PWANI.
TEL.+255712-660766/+255758-103103
E-MAIL: ekamalamo@gmail. com

Bwana Yesu asifiwe!
Natumaini hujambo na u mzima wa afya nafsi mwili na roho.
Namshukuru Mungu kila wakati anaipaye uzima huu niliyo nao ndani ya Kristo Yesu.

Karibu tujifunze pamoja somo hili ambalo Mungu ameweka "MOYONI MWANGU" nami sina budi kukushirikisha; na ninaamini utapata kitu cha kusaidia katika somo ambacho kitakutoa mahali ulipo kwenda mahali.
Roho Mtakatifu awe nawe unapojifunza somo hili katika Jina la Yesu Kristo Amen

Tunapokutana na matokeo "MABAYA" katika maisha yetu kama usipojua chanzo chake kimetoka wapi ni vugumu kuvuka katika maeneo mbali mbali ambayo yameshikiliwa nat vyanzo vyake.
Soma na Mimi kile kitabu cha Warumi 12:1-2 neno la Mungu linasema..."Basi, ndugu zangu nawashihi, kwa, huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, tkatifu, ya kumpwndeza Mungu, ndiyo ibada yenu maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu ,mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kupendeza, na ukamilifu."
Ukiisoma mistari kuna kitu nataka ukione ambacho Roho Mtakatifu anataka ukione; nacho ni "MWILI WAKO ULIO DHABIHU"
Kwa hiyo kama mwili wako ni dhabihu ujue ni "SADAKA KWA BWANA" ambayo hutolewa katika madhabahu ya Bwana.
Kama Mungu anauangalia "MWILI" wako kwa jicho la sadaka kwake ujue ni sadaka iliyo hai.
Ndiyo maana maandiko yanasema..."...HAI, TAKATIFU, YA KUPENDEZA" Takatifu maana yakee (kilichotengwa kwa kusudi maalumu) kwa hiyo, mwili wako unathamani kwa Bwana.
ooooh! Bwana Yesu asifiwee....!

Mwili wa Mtu aliyeokoka unatazamwa na Mungu kwa jicho la Mwili uliyo "DHABIHU AU SADAKA" ambao unahitajika kutumiwa na Mungu.
Ndiyo maana tunaambiwa..."WALA MSIIFUATISHE NAMNA YA DUNIA HII..." kama mkristo. usipojua jambo hili la si rahisi kuupa uthamani mwili wako katika viwango vya utakatifu mbele za Bwana.

MADHARA YANAYOTOKEA KWA MTU KUUTOA MWILI KWA KUIFUATA DUNIA
Jambo la I.
KUPATA SHIDA YA KUACHWA AU KUACHA WAKATI UCHUMBA.
Roho Mtakatifu aliponifunulia jambo hili nilipata maswali mengi sana, na kujiuliza je ni msaada upi wa mtu kutoka katika tatizo hilo? Lakini Roho Mtakatifu akikupa jambo ujue anakupa na njia ya kutatua tatizo hilo.
Sasa si kila anayeachwa au kumwacha mtu kwenye kipindi cha UCHUMBA anaweza kuwa katika tatizo hili la asha ! wapo ambao wanaachishwa na Mungu mwenyewe kwa kuwaokoa na watu wasiosahihi. Lakini wapo wanaoachishwa au kuacha kwa sababu ya AGANO LA UASHERATI lililofanyika ndani yake bado linanena.
Maandiko yanatwambia katika kitabu kile cha 1 Wakorintho 6:16-17 nasema..."Au hajui yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye ? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja. Sasa angalilia ule mstari wa unaofuata anavyosema..."LAKINI YEYE ALIYEUNGWA NA BWANA NI ROHO NAYE"
Sasa nataka uangalie jambo hili, unapofanya "UASHERATI" kwa mara ya kwanza ujue umeingia katika "AGANO" na Agano ni jambo linafungwa na watu wawili, na lazima kuwepo na "DAMU" kama alama ya kulithibitisha Agano hilo.
Wasomaji wa Biblia nadhani mnayakumbuka maneno ya Yesu wakati wa chakula cha mwisho wakati alipokaribia kuteswa, alikuwa yeye na wanafunzi wake alisema hivi...."KIKOMBE HIKI NI AGANO JIPYA KATIKA DAMU YANGU.." Katika chakula kulikuwepo MKATE NA DAVAI. MKATE-Ulisimamia Mwili wa Yesu ; DIVAI-Ilisimamia Damu ya Yesu. Swali? kwa nini MWILI haukutajwa kama ishara ya kuufanya AGANO, lakini DAMU ikatajwa kufanya Agano.
Ukitaka kujua Damu inafanya Agano kawaulize wagaga wa kienyeji watakwambia Damu inapokelewa kwa Miungu kama ishara ya kufanya Agano.

Najaribu kukupa mifano hii ili ujue kwamba mtu anapofanya UASHERATI na kama binti ni BIKIRA anapokutana na kijana lazima DAMU imwagike; na inapomwagika tayari katika ulimwengu wa roho hao wameunganishwa tayari, na kwasababu liko katika DHAMBI shetani analifuatalia hilo Agano,maana si WAWILI tena maandiko yanasema...."Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja? Maana ,Wale wawili watakuwa mwili mmoja" (1 Wakoritho 6:16)
Ndiyo maana unaweza kumuona kaka au Dada ana mchumba wake unashangaa wanavurugana na kuachana; na mara nyingine sababu hakuna na ipo si ya kuwatenganisaha. Kwa namna ya kibinadamu unaweza kufikiri ni ile sbabu usijue NI AGANO la Dada au Kaka halimruhusu kutoka kuolewa na mwingine ,hivyo Shetani ataachalia sababu zozote ili mladi usitoke kwenye Agano. Kama natania muulize msichana aliyetolewa bikira je anaweza kumsahau kilahisi aliyemtoa hiyo bikira ? Kama hakupata ufunuo wa namna hii atapata shida maana atakuwa anamkumbuka yule kaka ,kwa nini amkumbuke? alimwaga DAMU,NA IKIWAFUNGA AGANO.
Hivyo shetani hutumia sheria ya Agano ili kumfunga mtu, lakini usipojua kutoka katika Agano hilo utapata shida sana.

Ulishawahi kujiuliza kwa nini wanaopenda kuuza miili yao hawataki kuolewa ,na wakiolewa hawawezi kudumu kwenye ndoa? Ni kwa sababu wamefanya MAAGANO na wanaume wengi; hivyo hawezi kutoka katika MUUNGANO wa hao wakaka mbalimbali.
Fikilia kijana wa kiume umetembea na wadada saba, je hujui kwamba umeunganishwa katika roho na hao wadada? Kwa hiyo kuoa kwako kunaweza kukupa shida kama usipojua namna ya kutoka katika maagano hayo.

FUATANA NAMI KATIKA SOMO HILI NAWE UTABARIKIWA.
KAMA HUJAOKOKA OKOKA SASA BAADA YA KUFA NI HUKUMU (Waebrania 9:27)
MUNGU AKUBARIKI
ekamalamo@gmail. com

Comments