MAOMBI YA KUSAMBARATISHA VIKAO VYA WANAOKUJADILI KWA MABAYA.



 Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze kisha tuombe.


Isaya 54:15 '' Tazama, yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.''

Neno la MUNGU linaonyesha kwamba wakati mwingine huwa kuna wanaokusanyika kwa ajili yako katika ulimwengu wa roho wa giza, Lakini ukiomba katika KRISTO YESU Hakika utashinda.
Kila kitu kwako huwa hakifanyiki kwa ghafla tu bali huwa kuna mipango na mikakati iliyofanywa kwa ajili yako, mipango hiyo hufanyika katika vikao vya mawakala wa shetani, lakini ashukuriwe MUNGU kwa YESU KRISTO maaa leo tunasambaratisha vikao vyote vya wanaotujadili kwa mabaya.
Kazini kwako unaweza kuona viongozi wako wanakujadili ili wakufukuze kazi au wakusimamishe au wakushushe cheo. Kwenye kikao hicho utawaona wanadamau lakini naomba nikuambie kwamba hakuna jambo hata moja unaloliona katika ulimwengu wa mwili kama tu jambo hilo halikuanzia katika ulimwengu wa roho.
Vitu vyote vinavyokutokea katika maisha yako huwa vinaanzia katika ulimwengu wa roho ndipo vinakuja kutimia katika ulimwengu wa mwili.
Unaweza ukawaona wanadamu wanakujadili kwa mabaya kazini kwako kumbe katikati yao liko jini linalowaelekeza cha kuongea na cha kuamua juu yako.
Unaweza ukashangaa tu kwamba unashushwa cheo au kufukuzwa wakati wewe ndio hufanya kazi vizuri na kwa uaminifu lakini wanaofanya kazi kwa ulegevu ndio unawaona wanapandishwa vyeo, siri iko katika ulimwengu wa roho.
Kama huwezi kushinda katika ulimwengu wa roho na katika ulimwengu wa mwili huwezi kushinda pia.
Ashukuriwe MUNGU maana Neno lake linasema '' yamkini watakusanyana; lakini si kwa shauri langu. Watu wo wote watakaokusanyana juu yako wataanguka kwa ajili yako.''

 
Uchumba wako unaweza ukajadiliwa na wachawi na kama utashindwa kuwadhibiti hakika uchumba huo utavunjika na kukuachia maumivu makubwa.
Ni mara nyingi sana MUNGU husema na wewe kwa ndoto na maono ili kukujulisha kile wanachokupangia adui zako lakini wengi hudharau ndoto hizo ambazo baadae zikitimia kujuta na kusema kumbe ile ndoto ilikuwa kweli.
Ndoa yako kwenye kikao cha wachawi wanaweza wakapitisha maamuzi ya kwamba lazima ndoa hiyo iwe na migogoro kila siku.
Kujua huleta ushindi. Leo umejua haya ili ujue pia jinsi ya kupambana kiroho na ushinde.
Kwenye ndoto unaweza ukaona kabisa msimamo wa maadui zako lakini wengi huwa hawajui jinsi ya kupambana kimaombi, wengi hukimbilia kuwaambia watu kwamba wawaombee lakini watu hao husahau maana ni mambo ambayo hayana uzito kwao.
Ndugu nakuomba pambana mwenyewe kwa jina la YESU KRISTO na ushindi wako ni mkubwa sana baada ya kuyajua haya.
Pia nakuomba kila mara na kila siku omba ukiharibu vikao vya wote wanaokujadili katika ulimwengu wa roho wa giza.
Ukikivuruga kikao cha mashetani wanaokujadili hakika walichokusudia kwako ndio kitakuwa kimeishia hapo.
Kwa maombi ya leo hata vikao vya wachawi vya mwezi ujao au mwakani unaweza kuvisambaratisha.
Ukiwa ni mtu unayeishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO na ukawa muombaji hakika utakuwa mtu hatari katika ulimwengu wa roho. Wakati mwingine mawakala wa shetani kila wakitaka kukujadili tu watajikuta wanasahau au viti vinawaka moto na wanaarisha kikao hicho.
Nadhani umewahi kuona baadhi ya ajenda katika vikao zikiarishwa na kupangiwa siku nyingine kwa sababu tu ya uzito wa ajenda hizo. Kwa mwanamaombi halisi anayemcha MUNGU katika KRISTO ajenda zote zinazokuhusu wewe adui zako wanaweza kujikuta wanaahilisha kila mara hadi miaka inapita hakuna kilichokupata.

Maadui zako katika ulimwengu wa roho wa giza hukaa vikao ili kukujadili na kukuwekea mikakatai ya kukuharibia au kukuangamiza.
Maadui zako hukaa vikao ili kukujadili unaendeleaje kiroho.
Maadui zako hujadili watakuharibiaje uchumi wako, kazi yako au biashara yako.
Hukusanyikana katika vikao ili kuhakikisha mipango yako haiendi.
Maadui zako wanaweza kukaa vikao ili kupanga mikakati ya kukuharibia muujiza wako, uchumba wako au ndoa yako au baraka yako.
Maadui zako wanaweza kukaa vikao kwa ajili ya kuchunguza asili ya nguvu zako na ili wafanye mpango wa kuhakikisha nguvu zako za kiroho zinaondoka kwako.
Hebu ona kikao hiki kilichokuwa kinamjadili Samsoni ili wajue asili ya nguvu zake ili wapate kumwangamiza.


Waamuzi 16:5 '' Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja. '

Wafilisti kama maadui wa samsoni walikaa kikao na Delila mkewe Samson ili tu kujua asili ya nguvu za samson, kwenye kikao hicho walipanga hadi kiwango cha pesa ili tu kumpa Delila kama atawafanikisha mpango wao.
Hata wewe mmoja wa rafiki zako wa karibu au ndugu yako anaweza akaitwa katika kikao cha wabaya wako ili wajue jambo fulani kuhusu wewe ili wakumalize kwa urahisi.

Wachawi wanaweza kukaa kikao kwa ajili yako ili kuhakikisha hufanikiwi.
Kuna mtu anaweza kwenda kwa waganga kwa ajili yako, huko kwa mganga atakaa kikao na mganga ili kukujadili kwa lengo la kukudhuru au kukuharibia.
Unaweza kuwa ni mwanafunzi mwenye akili nzuri lakini adui yako anakwenda kwa waganga na kufanya kikao ili kuharibu ufahamu wako. Leo sambaratisha vikao vyao.
Inawezekana jina lako hupelekwa kwenye vikao vya mashetani kila mara.
Dalili moja wapo ya mtu jina lake kutajwa kwenye madhabahu za giza ni kusisimka nywele au mwili wote ghafla bila tatizo, wakati mwingine kutajwa kwa jina la mtu katika madhabahu za wachawi hukosa amani ghafla moyoni mwake. Ndugu yangu ukiona vitu kama hivyo omba kwa imani kwa jina la YESU KRISTO ili kuharibu vikao vyote vya wanakujadili kwa hila, wasambaratishe kwa damu ya YESU na kwa moto wa ROHO MTAKATIFU, liite jina la YESU na utashinda. kataa kila kusudi baya dhidi yako.
Haribu vikao vya wanaoijadili biashara yako kwa hila.
Vunja vikao vyote vya wachawi wanaoijadili afya yako. Kuna watu wanaumwa ukimwi lakini ni ukimwi wa kutengeneza na mashetani tu, ndugu ni muhimu sana kuharibu vikao vyote vya wanaokujadili kwa mabaya.
Inawezekana kabisa wanapanga ufe au wanapanga upooze.
Inawezekana kabisa wanapanga uzeeke bila kuolewa.
Inawezekana kabisa wanapanga kwenye vikao vyao vya giza kwamba kila mwaka uwe unafiwa tu.
Inawezekabisa wanaiwekea mipaka familia yenu ili mtu akifanikiwa tu kidogo afe.
Leo vunja vikao vyote vya wanaokujadili.
MUNGU akubariki sana kama unanielewa pia naomba mimi Peter Mabula nikushirikishe jambo moja hili ambalo limekuwa ndani yangu kwa muda mrefu. Nataka niwe nachapisha vitabu vitatu kila mwaka, nimeandaa masomo mengi sana na namshukuru ROHO MTAKATIFU ambaye hunipa masomo kila leo, niliyowahi kuandika mitandaoni ni sehemu tu ndogo ya masomo hayo japokuwa hadi kufika leo nimeshaandika masomo 502 ambayo nimeyaandaa kwa miaka 4.Naomba ndugu yangu unichangie mchango wa hiari wa kiwango chochote ili kufanikisha kuchapisha vitabu 2000 tu vya kuanzia ambapo nitaandaa kitabu cha maombi yenye nguvu na kitabu kingine cha ujana, uchumba na harakati za kuelekea ndoa na ndoa. Maelfu ya watu watasaidiwa na vitabu hivyo na kwa tendo hilo utakuwa umehubiri injili ya BWANA YESU pamoja na mimi na kwa MUNGU kuna thawabu kwa ajili yako maana umeipeleka injili. Ukiweza kunichangia hakika MUNGU wa mbinguni akubariki sana. Namba ya kunichangia ni hiyo moja ya tigo ambayo ni 0714252292 jina PETER MABULA, tuma kutokea mtandao wowote nitaipata pesa hiyo, namba hiyo pia huwa mwisho wa kila somo langu na ukiangalia kwenye blog yangu ya maisha ya ushindi unaweza ukafungua label juu mwanzo eneo lenye rangi ya njano na utaona masomo yangu yote zaidi ya 500 na kila somo mwisho wake ipo hiyo namba. Kama uko nje ya nchi unaweza kutafuta inbox au kwa email ili tuelekezane jinsi utakavyotuma, na kama utapenda kunitumia kwa Bank nitafute pia inbox nitakutumia account namba na utanitumia. Pia ukitaka maelezo zaidi kabla ya kutuma unaweza kunipigia kwanza kwa namba hiyo hiyo na MUNGU akubariki sana.
Asante kwa kunielewa na leo omba sasa ukiharibu vikao vyote vya mawakala wa shetani dhidi yako.
Haribu vikao vyote vya shetani vinavyokujadili.
Haribu silaha zote za shetani zilizopitishwa kwenye vikao vya kichawi na kiganga.
Vunja kila ulimi na kinywa kilichokujadili kwa hila.
Vunja vikao vyote vya maadui zako wa sirini.
Vunja vioo vyote vya wachawi unavyoonekana wewe kwao.
Haribu TV zote za kichawi na kamera za kichawi zinazokumulika na kukuona.

MUNGU BABA anasema
 ''Mkono wako na uinuliwe juu ya adui zako, na adui zako wote wakauliwe mbali.-Mika 5:9 ''

MAOMBI YA KUSAMBARATISHA VIKAO VYA WANAOKUJADILI KIPEPO.

YAHWEH MUNGU uliye hai ninakushukuru na kukuabudu BWANA. Asante kwa uzima wako kwangu na asante kwa nafasi hii ya kuomba mbele zako maombi muhimu ya kuniletea ushindi wangu leo. Nakushukuru MUNGU wangu kwa ufunuo huu wa leo.
Niko mbele zako MUNGU wangu nikivunja vikao vyote vya siri wanavyokaa maadui zangu ili kunijadili.
Nasambaratisha vikao vyote vya watu wabaya wanaoijadili kazi yangu na biashara yangu. Niko kinyume na vikao vyote vya wachawi dhidi yangu na navifuta leo na kuvisambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao vyote washirikina wanaokaa kwa ajili yangu,Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao vyote vya watu walioniendea kwa waganga wa kienyeji, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao vyote vya wasionitakia mema, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao vyote vya wachawi wanaotaka kuharibu uchumba wangu/ndoa yangu, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao vyote vya wanadamu wanaotumika kipepo dhidi yangu, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha kila aina ya vikao vya siri vya giza, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao mapepo vilivyokaa baharini au porini, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao vyote vya wachawi vya mchana na usiku, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha kila vikao vinavyopanga kunifelisha, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Nasambaritisha vikao vyote vya kupanga ajali na mikosi na balaa, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambatisha mchawi na uchawi wake, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
nambaratisha mganga wa kienyeji na uganga wake, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambatisha mshirikina na ushirikina wake, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha mkuu wa giza na giza lake, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao vyote vya kunipangia kuumwa, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nsambaratisha vikao vyote vya kuniletea misiba, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasambaratisha vikao vyote vya giza vya kuniletea madeni, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Nasamabatisha vikao vyote vya kuniletea ajali na balaa, Nasambaratisha kwa damu ya YESU KRISTO na kwa ajina la YESU KRISTO.
Asante MUNGU BABA mwenyezi kwa kunipa ushindi leo.
Asante BWANA YESU maana damu yako na jina lako vimenishindia.
Asante ROHO MTAKATIFU maana katika wewe nimeshinda.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi.
Amen Amen.


Ndugu uliyesoma ujumbe huu ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments