SIKU UZIA AKIFA UTAMUONA MUNGU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.

Isaya 6:1 ''Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.''

Mwaka ambao Mfalme Uzia alikufa Nabii Isaya alimuona MUNGU.
Kuna hali zingine mpaka uzia wako aondoke ndipo urtamuona MUNGU katika matendo makuu.
Ni kweli kila jambo lina wakati wake(Mhubiri 3:1) lakini kuna vizuizi fulani hadi viondoke kwako ndipo utaona ushindi.
Najua kabisa wakati wa kuipokea baraka yako ni sana lakini inabidi uzia aondoke kwako ndipo utamuona BWANA.
Uzia wako ni nani?
Uzia wako mpaka aondoke ndipo utamuona BWANA katika matendo makuu katika huduma yako, Uchumba wako,ndoa yako, uchumi wako, biashara yako, masomo yako n.k.

Siku Uzia wako akiondoka ndipo utamuona MUNGU.
Uzia wako anaweza kusababisha usiwe huru hadi aondoke ndipo utakuwa huru.

Siku Uzia wako akiondoka ndipo utamuona BWANA.

Zaburi 34:8-9 '' Onjeni mwone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini. Mcheni BWANA, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu. ''


Kuna watu wamejaa akina uzia lakini siku uzia akiondoka ndipo utamuona MUNGU kwa viwango vingine.
Sio lazima ubarikiwe leo ndugu ila siku Uzia wako akiondoka ndipo utamuona BWANA kwa baraka atakayokupa.
Uzia anaweza kuwa kizuizi chako kinachokutesa kwa muda mrefu sana maishani mwako.
Inawezekana kabisa roho ya kiburi ndio Uzia wako, Siku Uzia huyo akifa ndipo utamuona BWANA.
Inawezekana kabisa tabia yako ya Uzinzi ndio uzia wako anayekuzuia usiolewe au usibarikiwe kama wengine. Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA akikutendea muujiza.
Inawezekana mizimu ya ukoo wenu ndio uzia anayezuia usimuone MUNGU akikubariki, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA.


Ayubu 42:5 ''Nilikuwa nimesikia habari zako(MUNGU), kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona.''


Inawezekana kabisa kuna mtu katika ulimwengu wa roho wa giza amekalia cheo chako katika ulimwengu wa roho, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA
Inawezekana kabisa huyo mchawi anayefuatilia familia yako ndiye Uzia, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA
Inawezekana kabisa huyo anayekuzuia kumtumikia BWANA YESU ndio Uzia wako, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA
Inawezekana kabisa huyo rafiki yako unayemweza siri zako kila siku ndio Uzia wako, Inawezekana kabisa ndugu yako mchawi ndio uzia wako, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA
Inawezekana kabisa mfumo fulani mbaya katika uongozi wa kanisa lenu ndio uzia wako, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA.
Inawezekana kabisa tabia yako ya kukataa kuokoka ndio uzia wako, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA
Inawezekana kabisa Adui yako fulani wa sirini ndiyo uzia wako, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA
Inawezekana kabisa kanisa la kimwili unaloabudu ndio uzia wako, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA
Inawezekana kabisa kazi yako mbaya ndio uzia wako, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA
Siku akiondoka huyo uzia ndipo utamwona BWANA.
Uzia ndio kizuizi cha wewe kumwona MUNGU ila siku uzia akiondoa ndipo utamuona MUNGU.
Uzia anakuzuia hivyo kwa maombi yako kwa BWANA YESU anatakiwa huyo uzia aondoke ndipo utamuona BWANA kwa viwango vingine.


Yohana 11:4-5 '' YESU akajibu akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana mnayoyasikia na kuyaona; vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.Naye heri awaye yote asiyechukizwa nami.''


Ana heri ambaye hachukizwi na BWANA YESU.
Inawezekana kabisa huyo mkuu wa giza wa mtaaani kwenu ndiye Uzia, Siku huyo uzia akiondoka ndipo utamuona BWANA.
Kumuona BWANA ni kuona uzima.
Kumuona BWANA ni kuona ushindi mkuu.
Kumuona BWANA ni kumuona mwenye baraka zako, uzima wako na ulinzi wako na mali zako.

Nabii Isaya baada tu ya kufa kwa mfalime Uzia ndipo alimuona BWANA.
Siku akifa huyo mchawi anayekuzusumbua au akihama ndipo utamuona BWANA.
Siku ukiacha dhambi ndipo utaziona baraka za MUNGU maishani mwako, dhambi anaweza kuwa ndio uzia wako anayekuzuia usimuone MUNGU kwa matenddo makuu atakayokutendea.
Ninataka nichapishe vitabu ila napungukiwa Pesa hivyo kwa yeyote atakayependa kusapoti injili kwa kuwezesha vitabu hivyo 2000 vya kwanza kuchapishwa karibu, unaweza kuwasiliana na mimi inbox au kwa email au kwa tigo pesa, namba yangu ni 0714252292, Namba hiyo huwa iko kila mwisho wa kila somo langu. Ubarikiwe kwa hilo.

Ndugu uliyesoma ujumbe huu ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments