USHUHUDA WA KIJANA ALIYESHUKA KUZIMU KUTAKA FEDHA NA UMAARUFU

OMBENI ISRAELI AKISHUHUDIA KANISANI UFUFUO NA UZIMA KIGOMA.

Huu ni ushuhuda wa kijana mmoja aitwae OMBENI ISRAELI ambae alikuwa ni mwanamuziki mchanga alitamani kufahamika kama wasanii wengine maarufu ndipo alipo kutana na kijana mmoja aliyekuwa smart na mtanashati sana katika hoteli moja kila alipokuwa akikutana na kijana huyu alietafuta umaarufu alimpenda kwa usafi aliokuwa nao lakini kilichomvutia zaidi ni kwamba alikuwa anabadili magari ya kila namna pamoja na kuwa na wadada Warembo wengi.
Ndipo siku moja aliamua kumuuliza nini siri ya mafanikio yake, ndipo akamwambia "kijana uko tayari ujiunga na chama cha kikubwa?" kijana huyu kwa sababu alikuwa anahitaji umaarufu alimwambia niko tayari kwa lolote, ndipo akamwambia jtatu saa nne tukutane ili twende kwenye Ibada, Ilikuwa jijini Dar es salaam siku ilipofika walikutana na kumpa mavazi mekundu, alivaa suruali nyekundu, sharti nyekundu, saa na kofia nyekundu kijana huyu alijiona amependeza kuliko siku nyingine yoyote tangu azaliwe ilikiwa ni maandalizi ya kuelekea kanisani.
Baada ya hapo, alikuta kanisa limejaa kuliko kawaida na walipomuona walimfanyia sherehe kubwa akakaribishwa Madhabahuni na kupewa kiti kilichokuwa kimepambwa sana na makofi yakapigwa mara tatu, ndipo akasujudu na kukaribishwa karibu karibu mara tano. Ndipo akaanza kujieleza ametokea wapi na anahitaji nini, hapo akaambiwa hapa hakuna kitu kinacho shindikana lakini akaulizwa tena upo Tayari kwa lolote? aliulizwa swali hili kama mara Tano, alipokubali kuwa tayari kwa lolote ndipo akabadilishwa Jina na kuitwa (MORELIGHT).
Kijana anasema, "Ibada ilipoisha niliondoka na kupanda gari na kulipiwa nauli na mtu nisiyemjua ndipo niliambiwa Ijumaa tunatakiwa twende Yerusalemu mpya ila nikaambiwa nitafute mayai matano" haya, siku ilipofika wakaenda Baharini na kuanza kurusha yale mayai matano kama alivyoelekezwa, bahari ikajigawa na kufika sehemu ya kusaini na kula kiapo baada ya kusaini akaletewa karatasi iliyoandikwa kwamba kama kuna jambo litakukuta je uko tayari Issa akusaidie? Akaambiwa Issa maana yake ni Yesu, akasema sipo tayari. ndipo akaruhusiwa kuingia YERUSALEMU MPYA ambayo huku tunaita Kuzimu.
Basi akaona mageti saba, baada ya kuingia hadi geti la saba aliona giza nene mno na nyota inangaa kwa mbali sana baada ya kwenda mbele zaidi Kijana Ombeni anasema, "nilimuona nyoka mkubwa sana ambae sijawahi kumuona tangu nizaliwe,
Yule Joka akaniletea sahani nyeupe ndogo ambayo niliambiwa ukifaulu mtihani huu basi Utapata Pesa na kupata kibali Mbele za watu na utakuwa mtu kubwa sana duniani nikapewa na kakisu kadogo; akaniambia unaona nini ndani ya sinia nikamwambia ninaona Maji akaniambia nichome kisu ndani ya sinia, Wakati nataka kuchoma kwenye lile sinia nikamuona Mama Yangu ndipo nikastuka sana, nikasema siwezi ndipo nikaambiwa ulikuja mwenyewe akanilazimisha nichome nikamuona tena Baba Mdogo, nikamwambia siwezi ndipo wakaniambia sahau kama uliwahi kuishi duniani, ndipo lifti ikaja ikanichukua hadi kwa Lusifa yaani shetani akaniambia karibu na kuniambia Damu yako ni nzuri sana"

Je, Unataka kujua nini kiliendelea fuatana nasi na LIKE page hii.

Ushuhuda huu aliutoa Kanisa la Ufufuo

na Uzima Kigoma Mara baada ya kuombewa na Kufunguliwa. Kufika Ufufuo na Uzima tawi la Kigoma Mjini piga simu namba: 0768937938/0717162208

ufufuo na uzima kigoma

Comments