VUMILIA MAGUMU UNAYOPITIA HUKU UKIOMBA.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
MUNGU anakupenda sana na anakuwazia mema sana.
Isaya 55:8-10 ''Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula; ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma. ''

MUNGU anakuwazia mema sana.
MUNGU anaweza kukutendea mema sana ila uwe tu ndani ya kusudi  lake na katika muda alioupanga yeye na sio wewe. 
Ni ngumu sana kuwa ndani ya kusudi la MUNGU kama uko nje ya Wokovu wa KRISTO.
Ni ngumu sana kuwa ndani ya kusudi la MUNGU kama huna ROHO MTAKATIFU.
Ni ngumu sana kuwa ndani ya kusudi la MUNGU juu ya maisha yako kama huishi maisha matakatifu  ya Wokovu wa KRISTO.
Ni vigumu sana kuwa ndani ya kusudi la MUNGU kama huna muda wa kumuomba  MUNGU na kumshirikisha katika mahitaji yako.
MUNGU Anaweza Akakaa Nje Ya Mipango Yako Kama Hukumshirikisha.  Ni Heri Kumshirikisha MUNGU Kwa Maombi Na Utakatifu Katika Mipango Yako.
Ni kweli MUNGU anakuwazia mema lakini hakikisha unamtii na unalitii Neno lake ndipo utafanikiwa.
Vumilia wakati mgumu wa sasa huku ukiomba sana maana kesho haitakuwa kama leo, kesho ina ushindi wako na baraka yako kutoka kwa BWANA YESU.
Ni muhimu sana kuwa muombaji lakini pia ni muhimu sana kuomba kwa imani.
Inawezekana kabisa unaomba kwa imani lakini Imani yako haiko vizuri hata kama unaamini kile unachoomba.
Naomba utambue jambo hili kwamba;
Ili Kuiweka Vizuri Imani Yako Jifunze Kusamehe.
Mathayo 6:14-15 ''Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na BABA yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala BABA yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.''

Kuna baadhi ya watu wakipitia magumu kidogo tu humwacha BWANA YESU, Hiyo ni hatari sana.
Tunapaswa Kumtumikia KRISTO Katika Imani Thabiti. Imani Uliyoipokea Katika KRISTO Ni Ya Gharama Sana Hivyo Unatakiwa Kuilinda Sana.
Magumu ya sasa usikubali yakakuondoa katika wokovu wa BWANA YESU.
 Vumilia wakati mgumu wa sasa huku ukiomba sana maana kesho haitakuwa kama leo, kesho ina ushindi wako na baraka yako kutoka kwa BWANA YESU.
  ''BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.-Nahumu 1:7''

Mkristo Aliyekomaa Kiroho Kusikia Mabaya Kwake Ni Jambo La Kawaida Sana. Kadri Unavyovumilia Magumu Ndivyo Unavyokua Kiroho.
 Magumu ya sasa usikubali yakakuondolea utakatifu wako.
Magumu ya sasa usikubali yakaiua huduma yako njema kwa MUNGU.
Vumilia wakati mgumu wa sasa huku ukiomba sana maana kesho haitakuwa kama leo, kesho ina ushindi wako na baraka yako kutoka kwa BWANA YESU.

''MUNGU kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.-Zaburi 46:1-3''

Ni kweli wakati huu uko katika majaribu magumu kabisa lakini naomba ujue kwamba Kwenye baadhi ya majaribu MUNGU Hakuruhusu Upite Katika Jaribu Nje Ya Uwezo Wako, Lakini Hata Hilo Jaribu Dogo La Uwezo Wako Linaweza Kukuangusha Kama Humtii MUNGU.
 Vumilia wakati mgumu wa sasa huku ukiomba sana maana kesho haitakuwa kama leo, kesho ina ushindi wako na baraka yako kutoka kwa BWANA YESU.

Yakobo 1:12 '' Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, BWANA aliyowaahidia wampendao.'' 
 
Jaribu lako hilo lisikuangushe hata ukamwacha YESU.
Jaribu lako hilo lisikufanye uwe mtu wa mwilini tu badala ya rohoni.
Yaone Majaribu Kuwa Majaribio Tu Ya Kukupandisha Kiimani.
Lakini kuna majaribu ambayo watu wengine wanaweza kuyaleta kwako, Biblia inasema juu yako kwamba;
 Maana Majaribu/Makwazo  Hayana Budi Kuja Ila Ole Wake Anayeleta Majaribu Hayo. 
Luka 17:1-4 ''....  Makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake! Ingemfaa zaidi mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha mmojawapo wa wadogo hawa. Jilindeni; kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe. Na kama akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe. '' 

Ndugu, Kama Umeangukia Kwenye Majaribu Nakuomba Endelea Na Utakatifu Na Maombi, Lione Jaribu Hilo Kuwa Jaribio Tu Ambalo Likimalizika Utapanda Kiimani, Utapanda Viwango Kiroho Na Utapanda Kwenye Suala La Baraka.
 Vumilia wakati mgumu wa sasa huku ukiomba sana maana kesho haitakuwa kama leo, kesho ina ushindi wako na baraka yako kutoka kwa BWANA YESU.
.Hata Kama Unapitia Katika Magumu Kiasi Gani, Napenda Kukuambia Ndugu Kwamba Hakuna Magumu Yasiyo Na Mwisho. Ukidumu Katika Utakatifu, Maombi Na Utulivu Mbele Za BWANA Hakika Kesho Yako Njema Inakuja Na Itafika Tu.
 Wewe Ni Mbegu Iliyobarikiwa. Jitunze Sana Ili Uje Umzalie MUNGU Matunda Ya Utumishi Wako Katika Injili.
  Ni Muhimu pia kujua kwamba ili ufike uendako yaani katika baraka za MUNGU ni lazima uwe Mwaminifu kwa MUNGU.
Ni lazima uwe na uvumilivu katika baadhi ya mambo maana kuna mengine unaweza ukayahitaji sana kutoka kwa MUNGU lakini wakati wake hayo sio sasa hivyo vumilia huku ukiomba.
Wapende watu wote maana upendo ni kipimo cha ukamilifu.

''Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa MUNGU, na kila apendaye amezaliwa na MUNGU, naye anamjua MUNGU. Yeye asiyependa, hakumjua MUNGU, kwa maana MUNGU ni upendo.-1 Yohana 4:7-8''

Jambo jingine kuzingatia ni kuisikia na kuielewa sauti ya MUNGU inayozungumza na wewe.
Ni Bora Sana Kuisikia Sauti Ya MUNGU Na Kuitii.
 Inawezekana kabisa umekalia tu kusema MUNGU amekusahau.
Wewe unayesema MUNGU amekuacha au amekusahau naomba tu ujue kwamba MUNGU hajakuacha wala hajakusahau, kama MUNGU angekuacha au angekusahau hakika usingekuwepo duniani.

Naomba pia ujue kwamba Kila anayejishughulisha na ufalme wa MUNGU kupitia YESU KRISTO lazima tu kuna muda wa kuudhiwa, lakini atakayevumilia mpaka mwisho anao uzima wa milele.

Mathayo 24:13 '' Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka.''

Ndugu uliyesoma ujumbe huu ubarikiwe sana.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili.

Comments