JE UMEJIANDAA KUINGIA KATIKA NDOA?

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
BWANA YESU atukuzwe ndugu yangu.
Karibu tujifunze Neno la MUNGU.
Ndoa Nyingi Zimekufa Kwa Sababu Ya Wanandoa Kutokujiandaa Ili Kuingia Katika Ndoa. 
Je wewe umejiandaa kuingia katika ndoa?
Mithali 16:1 ''Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA.'' 
Kumbe maandalio   ya moyo ni ya mwanadamu ila tu jibu linalotokana na mombi ndilo hutoka kwa MUNGU.
Maandalizi ya kuingia katika ndoa ni ya mwanadamu.
Maandalizi ya ndoa yako unayaandaaje?
Kujiandaa maana yake ni kujiweka tayari.
Je umejiweka tayari kwa ajili ya kuingia katika ndoa?
Je uko katika umri sahihi kuingia katika ndoa?
Maisha ya ndoa ni lazima utambue kwamba hayatakuwa maisha ya kumtegemea mama au baba yako mzazi au mlezi.
Maisha ya ndoa yanakuhitaji wewe uamue vyema.
Kama kila jambo ukisikia ulikuwa unakimbia kumweleza baba yako wakati huu wa ndoa baba wala mama hawatakuwepo, ila utakuwepo wewe na mume wako au mke wako.
Kama mshauri wako alikuwa rafiki yako au shangazi yako, wakati huu mshauri wako namba moja atakuwa ni mke wako au mumeo.
Mwenzi wako wa ndoa huyo ndio msiri wako na rafiki yako wa kipekee.
Mke wako au mume wako ni zaidi ya ndugu hivyo huyo ni wa muhimu sana.
Je umejiandaaje kuingia katika ndoa?

Mwanzo 2:24 ''Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.'' 

Baada ya kuingia kwenye ndoa utatakiwa kuishi na mwenzi wako na sio wazazi wako.
Nyumbani kwenu utakuwa unakwenda tu kusalimia tena sio kwenda tu kienyeji bali utakuwa unaenda kwa kuruhusiwa na mwenzi wako wa ndoa.
Ndoa ni furaha sana na raha sana  ila pia unatakiwa kujiandaa kuishi maisha  ya ndoa.
Unatakiwa kuuandaa ufahamu wako kwa ajili ya ndoa.
Je umejiandaaje kuingia katika ndoa? 
Je umejiandaa kumpenda mkeo kama Neno la MUNGU linavyokuagiza?
 Wakolosai 3:19 '' Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.''

Sio kijana wewe ulizoea kuwasifia mabinti wa mitaani, wakati huu uko katika ndoa hivyo mabinti wa mitaani hawakuhusu tena hivyo wa kumsifia ni mke wako.
Kama binti ulizoea kuwaita vijana wa kanisani kwamba ni ma-handsome, wakati huu uko katika ndoa na handsome wako ni mmoja tu yaani mume wako.
Je umejiandaaje kuingia katika ndoa? 
Je umeandaa kitanda tu na shuka hata vyombo hakuna?
Je umeandaa tu kwa kununua Tv  kubwa huku kulala ni chini?
Je umeandaa tu vijiko viwili na sahani mbili? Wageni wakija umtafanyaje?
Je umejiandaa tu  suti huku ufahamu wako hujauandaa kuingia katika ndoa?
Je umejiandaa tu kujua kupika huku tabia mbaya hujaacha?
Je umejiandaaje kuingia katika ndoa?

Je mchumba uliyenaye ana umri sahihi wa kuingia katika ndoa?
Je uko tayari kwa ajili ya majukumu mapya ambayo ni ndoa?
Kabla ya kuingia katika ndoa kunahitajika maandalizi ya kina.
Maandalizi Namba Moja Ya Kuingia Katika Ndoa Ni Kuishi Maisha Matakatifu Na Kumwabudu MUNGU BABA Katika ROHO Na Kweli. Ubarikiwe Kama Umenielewa kwa hilo.
Kaa ndani ya KRISTO siku zote za kabla ya ndoa na baada ya kuingia katika ndoa.

''Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea.-Yohana 15:4-6 ''


Je uko tayari katika kuingia katika ndoa?
Je Mazingira uiyopo yanafaa wewe kuingia katika ndoa takatifu isiyo na mawaa.
Je tabia zako ni njema hata upate mchumba mwema?
 Rebeka Alikutana Na Taarifa Ya Kuchumbiwa Kwake Akiwa Kisimani Kuchota Maji(Mwanzo 24:14-39).
 Binti Najua Hujui Ni Wapi Unaweza Kupata Taarifa Za Kupata Mchumba Lakini Kujiachia Achia Kwako Kunaweza Kukukosesha Baraka Ya Mchumba Au Mume. Jiulize, Kama Rebeka Angekutwa Pale Kisimani Kavaa Kimini Na Nguo Za Kuacha Matiti Nje Angepata Mchumba? Hakika Asingepata Mchumba. 
Maisha Ya Kujiachia Achia Huku Ukiwa Na Kauli Za Kebehi Na Matusi Vinaweza Kukusababishia Usipate Mchumba, Na Kukuacha Siku Zote Ukisema Una Laana Ya Kutokuolewa Kumbe Wewe Ndio Hiyo Laana. Nasukumwa Sana Kuandika Haya Wakati Huu Maana Najua Kuna Mtu Atapona Na Mwaka Mmoja Ujao Atakuwa Katika Ndoa Yake Njema Tayari.



Je umejiandaaje kuingia katika ndoa? 
 Kama wewe una mcha MUNGU hakika MUNGU na yeye atakupa wewe mke/Mume Mcha MUNGU kama wewe.
Wagalatia 6:7 '' Msidanganyike, MUNGU hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. ''

  Je umejiandaaje kuingia katika ndoa? 
 Mtu Anayejiandaa Kuoa Au Kuolewa Anatakiwa Awe Safi Kimwili Na Kiroho. Kama Ni Mchafu Unaweza Kuishia Kuchumbiwa Tu Na Sio Kuolewa. Kama Ni Mchafu Unaweza Kuishia Kuchumbia Tu Lakini Sio Kuoa Maana Uchumba Utavunjika Kwa Sababu Yako Ya Uchafu Rohoni Na Mwilini.

 Je umejiandaaje kuingia katika ndoa?
Ukiwa Na Shingo Ngumu Watu Hawatataka Kuishi Na Wewe Kama Mke Au Mume. Kama Unatafuta Mchumba Naomba Ulijue Na Hilo. Unakuta Kijana Kila Siku Unaambiwa Acha Dhambi Na Ishi Maisha Matakatifu. Wewe Mwenye Shingo Ngumu Utaendelea Tu Na Uovu Wako Na Kwa Mabinti Wenye Akili Wala Hawatataka Kuolewa Na Wewe. Unakuta Binti Unavaa Kikahaba Daily. Kijana Mwenye Akili Hatatamani Kukuchumbia Hata Siku Moja.
 Je umejiandaaje kuingia katika ndoa? 
Ukiingia katika ndoa ni jambo jema sana ila Neno la MUNGU linakushauri likisema;
'' Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe-Waefeso 5:28.''

 Ewe kijana unayetaka kuoa au wewe binti unayetaka kuolewa; Je huwa unatendea kazi Neno la nani ili kufanikiwa kuingia katika ndoa?
1 Je huwa unatendea kazi Neno la MUNGU?
2 Je Huwa unatendea kazi Neno lako la tamaa ya kuoa/kuolewa?
3. Je huwa unatendea kazi maneno ya marafiki zako wasio kutakia mema?
4. Je. Huwa unatendea kazi maneno ya mchumba wako yanayokuondoa katika kusudi la MUNGU?

Najua kila mtu anaweza akanijibu kwamba anatendea kazi Neno la MUNGU wakati hata huwa kwenye Neno la MUNGU huwa haendi.
 Waefeso 6:14-17 ''Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa ROHO ambao ni neno la MUNGU;''


Inawezekana umeingia kwenye uasherati na mtu fulani ndio maana sasa unataka kuolewa naye au kumuoa japokuwa yeye ni wakala wa shetani.
Ndugu,YESU KRISTO Ndiye Pekee Rafiki Wa Kweli Maana Atakuwa Na Wewe Hadi Ukamilifu Wa Dahari {Mathayo 28:20}. Ndugu Achana Na Hao Marafiki Wazinzi Na Ambao Urafiki Au Uhusiano Wenu Utaishi Tu Kaburini.

Kuna Kusikia Kwa Namna Nyingi Na Kuna Kusikia Kwa Maeneo Mengi. Kuna Sauti Nyingi Sana Lakini Muhimu Nakuomba Jifunze Kumsikia MUNGU Na Kumtii. Ni Muhimu Sana Kujifunza Kumsikia MUNGU Na Kumtii Ili Akuongoze Katika Maisha Yako, Katika Mipango Yako Na Katika Mahitaji Yako. Mfano Hai Ni Kwamba Isikilize Sauti Ya MUNGU Wewe Unayeomba Kupata Mchumba Maana Sauti Ya MUNGU Itakuongoza Katika Kumpata Mume Mwema Au Mke Mwema. Huo Ni Mfano Mmoja Katika Mingi Ya Faida Za Kuitii Sauti Ya MUNGU. Naomba Ujue Pia Kwamba Sauti Ya MUNGU Inaweza Kuwa Ya Baraka Kwako Au Sauti Ya MUNGU Inaweza Kuwa Upanga Kwako maana MUNGU anaweza kukukataza baadhi ya vitu uvipendavya sana. Muhimu Ifanyie Kazi Sauti Ya MUNGU Hata Kama Inakuondoa Katika Mambo Uliyoyazoea Maishani Mwako.

 Je umejiandaaje kuingia katika ndoa? 
Kuna watu walijiandaa vizuri kuingia katika ndoa ila ila shetani akaingia nao katika ndoa na kuwatesa.
 Unaweza ukatupiwa kitu kibaya kwenye zawadi za harusi yako. Ni muhimu kuvitakasa vitu vyako vyote ukivyopewa wakati wa harusi yako.
 Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili

Comments