USISIKILIZE HABARI MBAYA:

Na Mtume na Nabii Josephat Mwingira.

Ikimbie Habari MBAYA yeyote inayotaka kuingia kwako, Kimbia any Negative thought ndani ya Maisha yako. Kwa Mfano Mtu akija akikuambia “Mwenzio Mimi niliolewaga na sasa Nimeachika, yaani yule Mwanaume alikuwa mbaya kweli kweli, Yaani Wanaume wala sio watu wazuri”…….Kimbia mara moja, Muage uende USISIKILIZE, USIRUHUSU Negative Mind ndani yako, USIRUHUSU Uharibifu ndani yako. Mfano labda ni Mwanafunzi mwenzio anakuja na kukuambia “Yaani Somo la Hesabu au somo la Sayansi ni Gumu sana, yaani Siliwezi kabisa, na Wala silitaki, yaani ukifanya tu una fail (unashindwa), yaani wewe wala usisome”……KATAA UHARIBIFU, Usiendelee KUSIKILIZA, Mwambie rafiki KWAHERI, Nina Haraka naenda KUJISOMEA. Mfano anaweza kuja Rafiki yako au Mfanyakazi mwenzio akaanza kukuambia "Yaani huyu Mwenye Kampuni Simpendi, yaani anajifanya Anapesa, Yaani Mimi namchukia, Yaani yeye muda wote ni Kufanya Kazi tu, yaani Simpendi kweli".......Mwanangu KIMBIA, MUAGE MARA MOJA Wala USIENDELEE wala KUTAKA KUENDELEA KUSIKILIZA Hizo HABARI MBAYA, huyo Mwenye Kampuni ndiye Anayesababisha Aende Chooni, ndiye anayesababisha Asomeshe Watoto wake, Alishe nyumbani, Aaamke Asubuhi na kwenda Kazini, KATAA KUSIKILIZA UHARIBIFU Usije Ukaingia Ndani yako. 

Mfano pia Anaweza kuja Mtu akaanza kukuambia “Yaani Askofu yule mbaya, yaani Mi simpendi, Anajifanya kila kitu anajua, anajifanya ana Hekima, anajifanya yaani Yeye ni Kiongozi wa kila kitu, Yaani Mimi namchukia, yaani hata akiagiza kitu Mimi huwa Sifanyi, Mimi huwa Nagoma kisirisiri, yaani Mimi simpendi”……..Mwanangu USISHIRIKI Hiyo dhambi, IKIMBIE hiyo dhambi ISIINGIE ndani yako nawe Ukapotea kama alivyokwishapotea huyo, USIRUHUSU huo Uharibifu kukujia na Kukuharibu, KIMBIA Kabisa, Mwambie KWAHERI, Acha NIKASOME Neno Nikapate NGUVU YA MUNGU, KIMBIA.
USIRUHUSU KUSIKILIZA Uharibifu Wowote ndani yako, USIRUHUSU KUINGIZA Habari Mbaya ndani yako, USIRUHUSU KUPOKEA Habari mbaya katika Masikio yako HAYAKUUMBWA kwa ajili ya Habari Mbaya YALIUMBWA kwa Ajili ya KUPOKEA, KUSIKILIZA HABARI NJEMA, Usiruhusu Dhambi iingie Ndani na Ikutafune.
USIRUHUSU.

 

Comments