MAOMBI YA KUZIBOMOA MADHABAHU ZA KIPEPO ZOTE.


Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.

Bwana YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze  maombi ya ushindi mkuu.
Kuna madhabahu nyingi za kishetani na hizo madhabahu zimewashikilia watu, familia, mtaa, mji au ukoo N.k
Madhabahu  ya kipepo ni mahali pa kutolea kafara za kipepo ili kukuharibia wewe au kuharibu kitu chako chochote.
Madhabahu za kishetani ni mahali wanapofanyia matambiko kwa ajili yako au familia yako au ukoo wako au uzaa wako au biashara yako au kitu chako chochote.
Tangu zamani MUNGU aliwataka wateule wake wazibomoe madhabahu za shetani zote maana madahabahu za shetani kwanza ni machukizo kwa MUNGU na pili madhabahu hizo zikiachwa zitakuwa tanzi mbaya kwa wateule wa MUNGU, Na zitakuwa miiba mikali mbvavuni mwao.
Waisraeli kama wateule wa MUNGU walitakiwa kuzibomoa na kuziharibu madhabahu zote za shetani lakini walipoziacha MUNGU kupitia Malaika wake alisema Maneno haya;
'' nanyi msifanye agano lo lote na hawa wenyeji wa nchi hii; zipomosheni nchi madhabahu zao; lakini hamkuisikia sauti yangu; je! Mmefanya haya kwa sababu gani?  Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni tanzi kwenu.-Waamuzi 2:2-3''

Wana wa Israeli kama wateule wa MUNGU walitakiwa na MUNGU wazibomoe na kuziharibu madhabahu zote za kipepo.
Wao walibomoa kwa jinsi ya kimwili lakini sisi katika agano jipya tunazibomoa kiroho kwa njia ya maombi kupitia jina kuu la YESU KRISTO.
Leo omba Maombi ya kubomoa Madhabahu za kishetani zote zinazokufuatilia au kukutesa katika maisha yako.
Ukisoma kitabu cha Waamuzi 6 Kuanzia Mstari 11 utaona jinsi ambavyo kulikuwa na madhabahu ya kishetani katika familia ya Yoashi na hiyo hiyo ilikuwa ndio madhabahu ya kishetani ya mji huo, Ngoja nikupe maandiko machache kutoka katika Sura hiyo ya waamuzi 6.
Waamuzi 6:25,28
''Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Mtwae ng'ombe wa baba yako, yaani ng'ombe wa pili, wa miaka saba, ukaiangushe MADHABAHU YA BAALI, ALIYONAYO BABA YAKO, ukaikate Ashera ile iliyo karibu nayo;
Hata WATU WA MJI walipoondoka asubuhi na mapema, tazama, madhabahu ya Baali imebomolewa, na ile Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na yule ng'ombe wa pili ametolewa sadaka juu ya ile madhabahu iliyojengwa''

Katika eneo la kina Gideoni kulikuwa na madhabahu ya kishetani ya familia iliyokuwa katika nyumba ya baba yake Gideoni na pia hiyo hiyo ilitumika kama madhabahu ya mji ndio maana wakazi wa mji walianza kumtafuta Gideon aliyeobomoa madhabahu hiyo kwa agizo la MUNGU.
Ndugu, Kuna madhabahu nyingi za kishetani zinazoweza kukushikiria wewe kama hutajua umuhimu wa kuomba ili kujikomboa.
Kuna Madhabahu za kishetani za familia.
Kuna Madhabahu za kishetani za ukoo.
Kuna Madhabahu za kishetani za jamii.

Kuna Madhabahu za kishetani za mji uliopo.
Kuna Madhabahu za kishetani za nchi.

Mfano, Mji unaweza ukakukataa na usiweze kufanikiwa ukiwa katika mji huo, hadi utakapofanikiwa kuvunja Madhabahu za kishetani za mji huo.

Yeremia 1:10A ''angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ''
Leo omba ukivunja Madhabahu za kishetani.
Leo omba ukiharibu Madhabahu zote za kishetani.
Leo omba ukibomoa Madhabahu zote za kishetani.
Leo omba ukiangamiza Madhabahu zote za kishetani.

Unaweza ukafungua biashara katika mtaa Fulani au kijiji Fulani ambapo ndani ya kijiji hicho kuna mganga wa kienyeji ambaye hutaka ukajipendekeze kwake ndipo utafanikiwa. Huyo mganga ni kuhani katika madhabahu ya kishetani.
 Ndugu usipomwita Bwana YESU kwenye biashara yako hakika mganga atakuzuilia mafanikio yako, hadi utakapoivunja Madhabahu yake ya kishetani kwa Maombi ndipo utafanikiwa na kustawi kibiashara.
Ni muhimu sana kila uendako uwe kwanza unavunja Madhabahu za kishetani katika eneo hilo.

Leo omba ukivunja Madhabahu zote za waganga na wachawi, vunja Madhabahu zote za ardhi, vunja Madhabahu zote za manuizi ya kipepo na makafara ya kishetani.
 Ni rahisi sana kushinda kupitia jina la YESU KRISTO Mfalme wa uzima.  
Ndugu tumika kama silaha ya MUNGU ya kuwaharibu mawakala wa shetani wote wenye madhabahu za kishetani katika maeneo yako yote.
 Yeremia 51:20-22 '' Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; na kwa wewe nitamvunja-vunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunja-vunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; na kwa wewe nitawavunja-vunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunja-vunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunja-vunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; ''

Ndugu, Utayaweza yote kwa YESU Mwokozi wako tu na sio vinginevyo.
Utawashinda wote wa kishetani ukiwa na YESU tu.
Mtii YESU kupitia Neno lake na omba kwa imani na utakatifu.
Kama wachawi hawajawahi kukukimbia basi wakati huu mmoja watakukimbia na hata kukutazama hawataweza.
Kama waganga wanakuchezea mchezo wa kukufilisi, wakati huu watashangaa Madhabahu zao zikiwadondokea na nguvu zao zikifutika kwa jina la YESU KRISTO Mwamba wa milele.

Kama kuna madhabahu zimeofunga ndoa yako na kuleta vita isiyoisha. Leo ukiwa na nia safi ndani yako na utakatifu sahihi katika KRISTO YESU nakuomba haribu madhabahu hizo za kishetani na zitaharibika.
Ni muhimu sana kuzibomoa madhabahu za kishetani maana madhabahu ya kishetani haiogopi bunduki wala degree yako bali inaogopa Damu ya YESU KRISTO tu.
Ndio maana ni muhimu sana kuomba maombi ya kuzibomoa madhabahu zote za shetani zilizokuzunguka.
Unaweza ukawa na elimu nzuri lakini kila siku wachawi wanakukaba usiku, ukiivunja madhabahu yao kwa jina la YESU hakika hutawaona tena wakikusumbua.
Unaweza ukawa na ulinzi wako wa mbwa na bunduki lakini majinamizi yanakuwa yanakukaba kila siku, ndio maana nasema kwamba madhabahu za kishetani haziogopi chochote ila damu ya YESU KRISTO tu. 
 Kumb 7:5  ''Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.''

Omba leo katika jina la YESU KRISTO ukivunja na kubomoa madhabahu zote za kishetani katika maeneo yako na maisha yako.
Madhabahu za kishetani zinaweza kuangamiza uchumi wako, kipato chako, afya yako, ndoa yako na chochote chako. Ndio maana ni muhimu sana kuomba maombi ya kuharibu madhabahu zote za kishetani zinazokufuatilia.
Madhabahu za kishetani ukiziaacha zitakufanya uwe mkia kimaisha na sio kichwa, zitakufanya mama mke akuchukue hadi akuite shetani bila hata kosa.
Madhabahu ya shetani ni mahali ambapo shetani anazungumzia maneno kinyume chako mtu wa MUNGU.
Madhabahu ya kishetani madhumuni yake ni kukufanya ushindwe, uabike, uadhirike. Inakuzuia kuendelea mbele na inakuzuia usiwe na ufahamu mzuri.
Madhabahu ya kishetani inaweza kuzuia maono yako na kukuzuia kufanikiwa.
Madhabahu ya kishetani ni lazima uiteketeze kwa jina la YESU KRISTO pekee.
Katika madhabahu ya kishetani hutoka magonjwa yasiyo na tiba na ni yale magonjwa ambayo vipimo vya hospitali havionyeshi kama mtu anaumwa wakati katika hali halisi anaumwa tena amezidiwa kabisa.
Ponda kwa jina la YESU madhabahu zote za kishetani zinazofuatilia maisha yako.
Yohana 14:13-14 Bwana YESU anasema ''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili BABA atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.''

Vyanzo vya madhabahu za kishetani ni.
1. Roho ya kumuasi MUNGU
1Sam 15:23 '' Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.''

2. Kutegemea Mila na desturi za kipepo za jamii au familia au ukoo.
Maombolezo 5:7 ''Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao. ''

Vunja Madhabahu za kishetani zote zinazokufatilia, vunja kwa jina la YESU KRISTO.
MUNGU BABA yuko tayari kukushindia kupitia maombi yako.
Warumi 16:20 ''Naye MUNGU wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu YESU KRISTO na iwe pamoja nanyi. [Amina.] ''
Ni muhimu sana kuzibomoa Madhabahu za kishetani katika mazingira yako.
Bomoa Madhabahu hizo kwa jina la YESU KRISTO.
Usipozivunja Madhabahu za kipepo kuna vitu vitakusumbua kuvishinda maana hujabomoa Madhabahu iliyobeba jambo baya hilo.
Madhabahu ya kipepo inaweza kubeba laana yako, hivyo vunja Madhabahu zote za kishetani.
Madhabahu ya kipepo inaweza kubeba magonjwa na umasikini, hivyo zibomoe Madhabahu zote za kishetani katika maeneo yako.
 Yakobo 4:7 ''Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. ''
Maombi haya naomba yamsaidie muombaji mchanga ili kuliendea hitaji lake sahihi.
Kwa wazoefu wa kuomba naomba tumia maandiko niliyoyatumia ndani ya somo hili ili kuliendea hitaji lako.
Kikubwa baada ya maombi haya ni utakatifu katika wokovu wa KRISTO YESU na mtii MUNGU.
Katika maandiko ya Waamuzi 6:25 na 28 tuliyoyatumia tunamuona Gideon akitoa sadaka katika madhabahu ya MUNGU baada ya kuibomoa madhabahu ya shetani.
Hata wewe baada ya kuibomoa madhabahu ya shetani basi Nenda kamtolee MUNGU sadaka nzuri kwenye madhabahu hai ya MUNGU kupitia watumishi wake waaminifu.
Kumbuka wachawi walikufunga kwa sadaka za kafara hivyo na wewe jifungue kwa Damu ya YESU KRISTO na Mtolee MUNGU sadaka maana sadaka iliyotoka kwa Moyo ina kazi nyingi sana na nzuri mbele za MUNGU.

MAOMBI YA KUBOMOA MADHABAHU ZOTE ZA KISHETANI KWENYE MAENEO YAKO.

YAHWEH wewe ni MUNGU na hakuna aliye kama wewe.
Ninakushukuru MUNGU wangu kwa kunilinda na kunipa Neema yako kuu kupitia YESU KRISTO.
Neno lako linakutambulisha katika Zaburi 83:18 kwamba uko juu ya yote na juu ya vyote.
Neno lako linakutambulisha pia katika Yeremia 10:6 kwamba Hakuna popote aliye kama wewe ee BWANA Mungu wangu na jina lako ni kuu katika uweza.
Ninakushukuru na kukusifu daima MUNGU wangu na muumbaji wangu. BWANA nakuomba leo uumbe uzima katika maisha yangu, ndoa yangu, biashara yangu, masomo yangu, kazi yangu, watoto wangu, afya yangu na kwenye vitu vyangu vyote.
Katika jina la YESU KRISTO ninabomoa madhabahu zote za kishetani katika maisha yangu yote.
Naibomoa na kuiangamiza madhabahu ya pombe,  iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiangamiza madhabahu ya magonjwa,  iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiharibu madhabahu ya madeni, iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiangamiza madhabahu ya kushindwa maisha, iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiangamiza madhabahu ya mafarakano kwenye ndoa, iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiangamiza madhabahu ya uchawi katika ukoo wangu, iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiangamiza madhabahu ya Uganga iliyo katika mtaa wangu, iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiangamiza madhabahu ya kukataliwa kwangu,
iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.

Naibomoa na kuiteketeza madhabahu ya kufukuzwa kazi,  iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiteketeza madhabahu iliyonifunga kiroho, iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiteketeza madhabahu iliyonifanya nikataliwe na kudharauliwa, iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Naibomoa na kuiangamiza madhabahu ya kishetani iliyoifunga biashara yangu, iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Kila madhabahu ya kishetani na kokote iliko kwenye eneo langu na maisha yangu naibomoa na kuiangamiza  kwa jina la YESU KRISTO,  iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Popote ilipo madhabahu ya kishetani katika ukoo wangu na kwa ndugu zangu wote naibomoa na kuiangamiza kwa jina la YESU KRISTO,  iondoke katika familia yangu na maisha yangu, iondoke kwa Damu ya YESU KRISTO na kwa jina la YESU KRISTO.
Asante MUNGU Baba maana umenishindia na sasa sitakamatwa tena na madhabahu za kishetani.
Najivua kutoka madhabahu zote za shetani.
Hata kama ndani ya mwili wangu iko madhabahu ya kipepo naibomoa na kuiangamiza kwa jina la YESU KRISTO.
Majini wote wanaotumwa ili kuniharibia kuanzia sasa watakosa pa kutua katika maisha yangu na moto wa jina la YESU wataukuta daima na huo moto utawala kwa jina la YESU KRISTO.
Katika jina la YESU KRISTO nimeomba na kupokea ushindi mkuu.
Amen Amen.

Ndugu, sasa wewe ni mshindi na mtii MUNGU siku zote.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana.

Comments