ATOA MAUZO YA DVD YAKE YOTE YA KWANZA KWA YATIMA.

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Loyce Nducha


Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Loyce Nducha atimiza ahadi yake ya kufikia watoto yatima ambao teali aliazimia moyoni kutoa pesa zitakazo patikana kwenye mauzo yote ya DVD na kujikuta kwenye uhuru wa kile alichokiita kuwa ni kufunguka kutoka kwenye kifungo cha nadhili ambayo ni mzigo wa huduma aliyobeba kwa watoto yatima, akizungumza na Efamline Loyce alisema katika kumtumikia Mungu kuna haja ya kujua wajibu wa kiutumishi na kusimamia ukweli wa lengo la utendaji katika kazi ya Mungu bila kusita au kuogopa vita ya kufikia kusudi.
Alisema mara nyingi amekuwa akitafuta namna ya kumfikia mwenye uhitaji na sasa anaona huo ndiyo mwanzo wake wa safari itakayomgarimu kufikiri na uomba kutimiza kusudi hilo ili kuwa sehemu ya kuwa kielelezo kwa vitendo.
Huu ni mwanzo wa safari ya kuwafikia wenye uhitaji ma wasiyo na uwezo kama yatima na wajane.
Alisema hili si la akili yake tu! bali ni pamoja na Mungu mwenyewe kumuwezesha kufikia kusudi na mwanzo wa safari ya huduma yake kwa jamii.

Comments