HATA KATIKA HILI NAMSHUKURU SANA MUNGU WANGU.

Na Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
Bwana YESU atukuzwe ndugu yangu.
Namshukuru MUNGU Maana mwaka 2016 niliandaa masomo 141 naamini ndugu ulibarikiwa.
Kama kuna sehemu nilikukwaza nisamehe maana neno la MUNGU sio kila siku nikutie moyo tu bali wakati mwingine neno ni kali kuliko upanga.


Waebrania 4:12-13 ''Maana Neno la MUNGU li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu.''


Neno hai la MUNGU li hai na kama li hai ndio maana wakati mwingine linachoma, likikuchoma tengeneza njia zako ili umpendeze MUNGU.
Neno la MUNGU linayatambua mawazo yako na makusudi ya moyo wako, hivyo ukiona linakuonya mfano usiende kuiba, acha na litii neno la MUNGU maana linayatambua mawazo yako. Ukiona Neno la MUNGU linakukataza kuzini, acha dhambi hiyo maana unaweza kuikosa mbingu na unaweza kupata madhara kakubwa sana na magonjwa. 

Neno linajua mawazo ya moyo wako hivyo popote unaponaa Neno la MUNGU kama linataka kukuondoa katika mipango yako ya kipepo, ndugu litii Neno la MUNGU maana kulitii Neno la MUNGU ndiko kumtii MUNGU mwenyewe.
Mwaka 2016 sikufikia lengo langu ambalo nimeshajiwekea utaratibu kila mwaka la kuandaa masomo zaidi ya 200.
ROHO MTAKATIFU ana hazima maelfu za kutufundisha labda sisi tu tuwe na udhuru.
Miezi ya mwanzo ya mwaka 2016 nilikuwa kozi ya uongozi Zanzibar labda ndio maana sikutimiza lengo la kuandaa masomo zaidi ya 200 ambayo yamekuwa msaada kwa watu wengi sana.
Mwaka huu namuomba MUNGU nitimize lengo la kufidia mapungufu ya mwaka ulipita.
Wewe mteule wa KRISTO uliye muombaji nakusihi sana usiache kuniombea maana injili ya kweli inahitajika sana wakati huu kuliko hata huko nyuma.
Kuna wakati kibinadamu unaweza kuchoka lakini ROHO wa MUNGU anakupa masomo ya kufundisha.
Wakati mwingine adui hupiga vita hata vitendea kazi vya kuliandaa Neno la MUNGU.
Wakati mwingine vita ni kubwa na mara zote Bwana YESU ni mshindi na hunishindia.
Uchapishaji wa vitabu unaendelea na nakuomba sasa ukiguswa kunisapoti kwa mchango wako wowote nakuomba fanya hivyo na MUNGU atakubariki sana sana na kukujaza.

Mwaka 2016 somo la kwanza liliitwa ''HAKIKISHA UNAONGOZWA NA NENO LA MUNGU MAANA YA DUNIA YOTE YATAPITA.'' na somo la mwisho ni ''UMEMFUATA MWOKOZI YESU AU UMEFUATA DINI?''
Namshukuru sana MUNGU katika yote na baadae nitakufafanulia kile ambacho MUNGU ameniambia kufundisha mwaka huu kama kipaombele changu.


Asante kama umeelewa  ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana Na nakuomba nisaidie kushare kwa marafiki zako ili na wao wajifunze Neno la MUNGU.


Comments