kalenda za kichawi-1

 
Na Askofu Mkuu Dk Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima.

 Baadhi ya watu wakristo wengi huenda kanisani kwao kwenda kanisani hawajui kwanini kuna kanisa huenda bila kujua wanaenda kufanya nini, kanisa lipo kwaajili ya kutatua mambo yaliyoshindikana kwa akili za kibinadamu, kanisa lipo kwaajili ya kutatua mambo yaliyoshindikana kutatuliwa kwa ferdha.Tumeona kuna ulimwengu wa kiroho na ulimwengu wa mwilini.
Tumesheherekea Christmas kama Yesu amezaliwa lakini hakuzaliwa miaka 2000 iliyopita kwasababu kama alizaliwa miaka hiyo na anaitwa Mungu basi kabla hajazaliwa Mungu hakuwepo. Yesu alikuwepo hata kabla hajazaliwa kimwili duniani.
Kila jambo baya au zuri linaloanza huanzia rohoni kwanza na baadaye hudhihirika kwenye ulimwengu wa mwilini. Kuna nguvu zinazomiliki kuongoza rohoni, Zipo nguvu za Mungu wa mbinguni na nguvu za shetani. Nguvu za Mungu wa mbingu na nchi ndizo tunazo ambazo zinatupa afya, nguvu, amani, ulinzi na mamlaka hapa duniani, shetani naye anazo nguvu ambazo ni za giza, nguvu zake ndizo zinazoleta magonjwa, uasi, chuki, uoga, vifo vya kutengeneza, kupitia watumishi wa shetani waganga wa kienyeji, washirikina, wachawi ambao huenda mpaka kuzimu kwenda kuchukua nguvu za shetanikuja kuzitumia kuharibu maisha ya watu.

Kuna kalenda za kiroho za kishetani ambazo zinasababisha matukio mabaya yote yanayotokea duniani. Ili ziitwe kalenda zinakuwa na siku, tarehe, mwezi na mwaka zmbazo ndizo zinakuwa kalenda kamili.
“Wale malaika wanne wakafunguliwa, waliokuwa wamewekwa tayari kwa ile saa na siku na mwezi na mwaka, ili kwamba waue theluthi ya wanadamu.” Ufunuo wa Yohana 9:15
Hapa wanaonekana malaika wanne ili waende kutenda mabaya, malaika hawa ni mapepo wanakuwa wameandaliwa kwaajili ya ile kalenda ya kishetani/kichawi. Imeandikwa Mashetani hawa wamefugwa mahali kwaajili ya siku fulani, tarehe fulani, mwezi na mwaka fulani kwaajili ya mtu ili apate ajali afe ama kwenye ajali ama kwenye moto.
Unakuta ile siku imefika na mapepeo haya yanaachiliwa. Unaweza kukuta familia flani inapatwa na magonjwa ya marakwa mara, familia flani huwa wanakufa wakifikia miaka fulani, unakuta ukoo flani watu wake hujinyonga mara kwa mara.
“Wakamwambia, wakisema, Vema, lakini tutakufunga sana, na kukutia katika mikono yao; lakini hakika hatutakuua. Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya, wakamchukua kutoka huko jabalini.Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo roho ya Bwana ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.” Waamuzi 15:13-14
Watu wanaofanya vita na wewe ni wale unaoishi nao, ndugu anaweza kukufunga kwenye familia kuna ndugu anafunga biashara, anafunga kazi, anafunga safari. Kwenye kila familia kuna mtu mmoja ambaye amewekwa na shetani kwaajili aya kuwashusha chini watoto na wakubwa, mara nyingi mtu wa aina hiyo yupo kwenye kila familia.
Usalitu upo, Mungu alisalitiwa na Ibilisi aliyekuwa malaika mzuri aweka uwepo mbinguni. Daudi alisalitiwa na Mwanae wa kumzaa Absalom, Musa alisalitiwa na dada yake Miriam, unaona ndugu ndio wanaoweza kukusaliti na kukufunga zaidi ya mtu ambaye hakujui..
“`kama huamini shetani hayupo hawezi kukuacha kwasababu huamini.”
Malaika hawa wanne imeandikwa wamefungwa kwenye mto Frati ambao upo hata leo, wamewekwa kwaajili ya kalenda ya siku fulani na tarehe fulani na mwezi flani na mwaka flani.
Kuna siku Saba tu ndani ya mwaka mzima ambazo ni Jumatatu hadi Jumapili ambazo zinajirudia na kufikia wiki, mwezi hadi mwaka mzima kupishana tarehe. Siku hizi ndizo mabaya hupangwa ili yatokee taehe moja ya siku hizi na mwenzi na mwaka flani. Tunafunga na kuomba ili kufuta kalenda zote za kishetani na matukio yake kwenye maisha yetu mwaka wote wa 2017 juu yetu na familia zetu kwa jina la Yesu.

Esta 3:8-14” Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme.
Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema.Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake.Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara.Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku ile ile.”
Tunaona Maandiko yanatuonyesha kumbe mpango wa uovu wa kalenda ya kichawi unaweza kuandaliwa ili utokee tahene na mwezi na mwaka flani, Imeandikwa tarehe ya kumi na tatu ili uje utimie tarehe kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili.
Maarifa ya Mungu ni ya muhimu sana.
Isaya 5:13 "Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.”

Hosea 4:6 “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako:”
Tumeona kumbe kuna kalenda ya kufishwa, kuuawa na mali zako kuchukuliwa,Biblia inatuonyesha zipotarehe za kalenda ya kichawi ili ufilisike, Mungu ameshatusaidia tayari ameshatupa mamlaka na nguvu lakini inatupasa kusimama na kushindana na kila hila ya adui dhidi ya maisha yetu. Kalenda za kichawi huwa zimehakikishwa, kalenda za kichawi huwa zimepangwa ili zitimie na lazima litimie kama hauko viruri.
Esta 8:1-17 “Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu.Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani.Tena Esta akasema na mfalme mara ya pili, akaanguka miguuni pake, akamsihi kwa machozi ayaondoe madhara ya Hamani, Mwagagi, na shauri alilowafanyia Wayahudi.Ndipo mfalme alipomnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu. Basi Esta akaondoka, akasimama mbele ya mfalme.Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, iandikwe kuzitangua barua za Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika majimbo yote ya mfalme.Kwa maana niwezeje kuyaona mabaya yatakayowajia watu wangu? Au niwezeje kuyatazama maangamizo ya jamaa zangu?Mfalme Ahasuero akawaambia malkia Esta na Mordekai, Myahudi, kusema, Tazama, nimekwisha kumpa Esta nyumba yake Hamani, naye mwenyewe wamekwisha kumtundika juu ya mti, kwa sababu aliwatia mikono Wayahudi.Basi waandikieni Wayahudi pia vyo vyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie muhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme hakuna awezaye kulitangua.Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na maakida na maliwali, na wakuu wa majimbo toka Bara Hindi mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao.Akaandika kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutia muhuri kwa pete ya mfalme, akazipeleka barua kwa matarishi, wamepanda farasi, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, ndio waliozalishwa katika zizi la mfalme.Katika barua hizo mfalme aliwaruhusu Wayahudi wakusanyike katika kila mji na kuzisimamia maisha zao, kuangamiza, na kuua, na kulifisha jeshi lote la watu na la jimbo watakaowaondokea, wao na wadogo wao na wanawake; na kuyachukua mali yao kuwa nyara;siku moja, katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote, na kwa Wayahudi, wawe tayari siku ile ile kujilipiza kisasi juu ya adui zao.Matarishi wakaondoka, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, huku wakihimizwa na kusukumizwa kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni.Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia.Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi.Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia.”
Esther na watu wake Wayahudi walikuwa wamepangiwa kalenda ya kishetani ili waangamizwe wote lakini walipigana mpaka mwisho Mungu akawasaidia wakaitengua,
Esta alisimama imara akaenda kwa Mfalme kuongea na Mfalme kuhusu ile barua juu yake na watu wake bila kuogopa, (Ukisimama bilauoga utapata kibali mbele ya watu wenye msaada wakukuvusha kwa jina la Yesu.) Barua ilishaandikwa ili wayahudi wauwawe lakini Esther alifanikiwa kwenda kumshawishi mfalme atengeneze waraka mwingine. Tunajifunza kalenda nyingi za mabaya huwa hazitatuliwi hadi upatikane waraka mwingine.
kalenda ya upande wa giza haiwezi kutanguka mpaka apatikane mfalme mwingine, Danieli naye alipangiwa mipango mibaya na walewale waliomtakia mabaya waliangamia kule walitaka angamie. Tunaye Mfalme Yesu ambaye leo hii ametupa waraka Biblia ili tuzitengue kalenda zote za kichawi za siku ya jumatatu na siku nyingine nay ale mabaya yaliyopangwa juu yetu yawapate walewale na tunawashinda kwa damu ya mwanakondoo Yesu Kristo.

(Simama kama askari wa Yesu Kristo uzifute kalenda zote na matukio ya kichawi juu yako na familia yake kwa jina la Yesu, shambulia mapepo na wachawi na waganga wa kienyeji kwa jina la Yesu)
Siku za jumatatu za maisha yako mwaka huu 2017 ziwe siku za kushinda na mabaya hayatakupata kwa jina la Yesu. Mabaya yaliyopangwa siku zate jumatatu yabatilike na ushinde na kustawi kwenye biashara, ndoa, kazi, watoto, Afya na ustawi mwaka huu umeshamharibu Yule aletaye mabaya kwenye kalenda za kichawi na yale mabaya yaliyopangwa juu yako na familia yako hayataokea tena kwa jina Yesu Amen.

Comments