Kalenda za kichawi (Sehemu ya Pili)

Na Askofu Dk Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima.

Mungu alimtokea Mfalme Nebukadreza akamwambia kalenda itakayompata kwasababu alipata kiburi, zile nyakati saba za Mungu ni miaka saba, Biblia inasema akaota manyoya akawa kama ndege na ile miaka saba ilipotimia akili zake zikamjia. Hii ni kalenda ya rohoni upande wa Mungu.
Danieli 5:18-22”Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye juu alimpa Nebukadreza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu;na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.Na wewe, mwanawe, Ee Belshaza, hukujinyenyekeza moyo wako, ijapokuwa ulijua hayo yote.”
Danieli 5:21 “Akafukuzwa mbali na wanadamu, moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda-mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu Aliye juu ndiye anayetawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.”
Mwanzo 15:13-14”Bwana akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa muda wa miaka mia nne.Hata na taifa lile, watakaowatumikia, nitawahukumu; baadaye watatoka na mali mengi.”
Ibrahimu aliambiwa na Mungu ana wakati mgumu lakini watoto wake watakuwa vizuri na kustawi na uzao wake utabarikiwa ndio hao wayahudi.
Mungu alisema atakupa fedha wewe unatakiwa utafute njia zipi ambazo unatakiwa kufanya ili Mungu akutumie, Mungu akikuambia utakuwa raisi ukalala tu nyumbani bila kupiga kampeni utabakia hivyo, jambo ambalo Mungu amelitaja kwako litimie kwako ni lazima uchukue hatua. Mungu hawezi kuja kukubeba ukiwa umelala bali unatakiwa uanze kutembea mwenyewe. Ahadi inaweza kuchelewa usipo chukua hatua Mungu ni mwaminifu ni lazima uitumie nafasi yako ili ufanikiwe, kuna watu Mungu amewaweka karibu yako ili wakuinue na ubarikiwe hivyo ndivyo Mungu anavyowainua watu.
Kila mtu anayo hadithi yake ya kule alipotoka na anakoendelea, Pale ulipo sasahivi hapajalishi sana lakini kule unakoelekea ndipo kunakojalisha usihofu simama mwamini Mungu atakuvusha utafanikiwa kwa jina la Yesu.
Musa alizijua njia za Mungu aliyajua matendo makuu ya Mungu ndiomaana Mungu akawaambia wana wa Israeli kwa kalenda yake inavyoelekea anaona wana wa Israeli watakwenda utumwani kwa muda wa miaka mianne na baadaye atawatoa tunajifunza Mungu akisema jambo linatimia, kama Mungu amesema atakupa baada ya muda flani ikitimia anza kubeba mizigo yako anza kuondoka usisubiri kuambiwa. Wana wa Israeli hawakufanya hivyo mpaka ikafika miaka mianne na thelathini, wakaanza kulalamika.
Kutoka12:40
Ukiona kwamba unatakiwa kufanya biashara kuna nafasi yako, ukiona kwamba kuna nafasi
Iliandaliwa kalenda ya kuwauwa wayahudi waraka ule waraka ilipangwa wauwawe kwa kalenda maalum na ratiba maalum. Mfalme alikuwa anatawala kwa kuabudu mizimu kwa miezi mitatu, inamaanisha alikuwa mchawi na alikuwa anawatoa watu sadaka.
Tumeona wale walitaka kuwaangusha Esta na wayahudi kwa waraka wao waliouandaa lakini waraka ule ukawageukia. Na sisi tutavuka salama kwa jina la Yesu na tutakapovuka hatutawasahau wale waliotutaabisha na kutupa matatizo, yale mazito yaliyoinuka juu yako hutayakumbuka tena kwa jina la Yesu.

Huyu haman alikuwa waziri mkuu na alikuwa anawachukia watu wa Mungu bila sababu, kumbe duniani utakutana na watu wanaokuchukia ukiinuka kwenye siasa wapo watakaokuchukia, ukiinuka kwenye Elimu wapo watakao kuchukia, ukiinuliwa kwenye idara yeyote ilea dui atatokea, utakapojifanya mpole huongei adui atatokea ukijifanya unawakaribisha watu na kuwapenda adui atatoke anachotakiwa kufanya usisikilize yale watu wanayoyasema wewe simama na Bwana. Hata Mungu anaye adui. Kuna wakati mwingine wewe unaweza kukata tama ujadhani hakuna knachofanyika hapana kuna kalenda inaliyoandaliwa usiogope ukipata maarifa kama haya unaingiwa na ujasiri unaanza kushindana pale unapoona mambo hayaendi vizuri kwasababu unajua nini kinaendelea.
Yeremia 17:7-8“Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea Bwana, Ambaye Bwana ni tumaini lake.Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala hautaacha kuzaa matunda.”
Asili ya Mwanadamu ametengenezwa mbinguni. Wale wanaosema imeshindikana huwezi tena wewe achana nao usiwasikilize maneno yao mwamini Mungu aliyekutengeneza kama ni shida ya moyo atakupa moyo mpya, kama ni watoto atakupa watoto, kama ni biashara atakupa, usiogope wala usitahayarike mtetezi wako yuu hai na kama hajasema huwei basi usiogope simama msikilize Mungu aliyekuumba nawe utaishi na kufanikiwa mahala popote.
1 Yohana 5:14-15”Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba.”

Wayahudi walipoona wameandikiwa waraka ili wafe waliamua kufunga na kuomba kwa muda wa siku tatu kwaajili ya jambo hilo na hakufa hata mtu mmoja. Kuna ulimwengu ambao wachawi wanapanga mabaya na mikosi ikupate kwenye kalenda zao kila siku yakupate mabaya. Kama mabaya yamekupata leo usifikiri yameanza siku ya leo, Hapa! bali yamepangwa siku nyingi kwenye kalenda ili yakupate nay ale yaliyokupata ni utimilifu wake.
Imani yetu haijaanza ufukweni au kwenye mapinduzi, imani yetu haijaanzia kwenye vikao, imani yetu haijaanza kwenye kampeni au kwenye air-conditions, Imani yetu imeanzia kwenye maumivu pale msalababi, imani yetu inamaumi flani unaweza kuumia ukaumizwa na watu kwasababu watu wanapenda kujipendekeza wakuumize, usiogope mtetezi wako yu hai ambaye ni Yesu kristo mwisho wa siku Yesu atakutetea atakusimamia atakuongoza mtetezi wako yu hai usiogope kwa jina la Yesu.

“Efu mbili na kumi na saba waliofanya vita juu yako waanguke juu yako kwa jina la Yesu, huataaibika tena, ile safari ambayo haiendeki itaendeka kwa jina la Yesu, Masomo yatasomeka tena, Ndoa itakuwa sawa na utafanikiwa, utaolewa au kuoa, utachumbiwa au kuchumbia, utanunua kiwanja kwasababu mtumishi wa Bwana amesema na akisema ni Bwana amesema, akivunja ni Bwana amevunja na hakuna mtu kwenye falimia yako atakayepatwa na mabaya ya magonjwa na umaskini na hutapungukiwa kwa jina la Yesu.”
Mungu huangusha chini watu wasio na haki ili waliofunikwa wainuliwe, watu wenye haki waliofunikwa chini huu hi wakati wao kustawi kwenye biashara, kwenye ndoa, kwenye Elimu n.k huu ni wakati wa kutofautishwa na waovu kwenye maisha ya kila siku, wakati wengine wanalia hali nguvu wewe utakuwa unastawi bila shida yeyote ile, endelea kukaa ndani ya Ufalme wa Mungu na utastawi kwa jina la Yesu.
Kufunga na kuomba ni kusimama ili kupata majibu kwenye mambo yaliyoshindikana kwenye hali ya kawaida. Ukisimama ukaomba kwa kufunga na kuomba kwenye jambo lolote unalolitaka kulifanya ukianza kwa kulishinda kwenye ulimwengu wa roho kwa kufunga na kuomba basi lazima utashinda kwenye ulimwengu wa mwilini kwa asilimia 100% na mwaka huu wa 2017 tumeanza kwa kufunga na kuomba na huu utakuwa ni mwaka wako wa kustawi kwenye kila idara ya maisha yako kwa jina la Yesu.
Kufunga na kuomba, Kuacha kula kwaajili ya Bwana ni jambo dogo lakini ni gumu sana kulitimiza, ni jambo dogo lakini lina matukio hasi kwa asilimia miamoja kwenye shida yako.
Kwenye Biblia wale waliofunga maombi ya siku tatu maombi yao yalijibiwa na kuleta majibu makubwa sana, Kule Shushani ngomeni walifunga maombi yasiku tatu uharibifu uliopangwa ukabatilika, na wewe umefunga leo siku ya tatu Mungu amefanya mambo makubwa juu yako mwaka huu mzima kwa jinala Yesu.
Wayahudi walipofunga siku tatu yale yaliopangwa juu yao na Mfalme aliyabatilisha na akatengeneza waraka mzuri wa kuwaokoa ayahudi wote na wewe Mungu atabatilisha kalenda zote zilizopangwa juu yako na wachawi mabaya yote yaliyopangwa juu yako ili yakupate mwaka huu wa 2017 yafutike na uaandikiwe kalenda nzuri ya afya, biashara, kazi, safari utastawi tena kwa jina la Yesu.

Danieli 9
Wayahudi waliambiwa na Mungu watachukuliwa utumwani miaka sabini baaadyae watarudishwa, sabuni Mungu ni Mungu wa kalenda, Angalia Biblia imejaa kalenda za Mungu kila mahali.
Yesu alijaribiwa siku arobaini; Musa alipokwenda mlimani alitumia siku arobaini, Bado Nuhu aliambiwa na Mungu ajenge safina kwasababu atashusha mvua siku arobaini lakini bado baada ya mvua kuisha alichukua siku arobaini kuangalia kama maji yamekauka kwenye nchi, Goriath wa gati aliwatukana wana wa Israeli siku arobaini, Elia alikula chakula kilichompa nguvu ya kutembea kwa siku arobaini, wapelelezi walienda kupeleleza nchi ya ahadi kwa siku arobaini, utaona arobaini arobaini kila mahali Mungu ni Mungu wa kalenda.

Mungu ni Mungu wa kalenda, unakumbuka wana wa Israeli Mungu aliwaambia watakwenda utumwani maka sabini, na Utamwona Danieli anasema kwa kuvisoma vitabu nikaona ratiba ya Mungu imeshatimia kumbe tunajifunza ukitembea kwenye kalenda ya Mungu utafanikiwa, tunakoelekea siku zijazo Mungu anatimiza ratiba ya watu wake wastawi wainuke biashara zao zifanikiwe, tunakoelekea kwenye Ulimwengu ujao watu wa Mungu watainuka kwasababu ile njia ya Injili kutokea Afrika kwenda Israeli inakaribia kufunguka.
Dunia tunayoiendea wanaomiliki asili ndio watakaoimiliki dunia na tulio na Mungu tutatenda miujiza na maajabu kupita kawaida iliyowahi kutokea, mali na pesa na utajiri zienda kanisani ili Injili ya Mungu ifike mahali kokote dunia nzima. Siku zijazo vita itatokea kati ya wale wanaokubali Uyuda watapigana na wale wawasiomkubali Mungu kabisa na utafika wakati wale wanaotembea na Mungu watatembea kwa kutenda miujiza, wengine watalia njaa wao watafurahi, wengine watalia magonjwa wao wanapita katikati yake kwa kuwa na afya kamili.
Isaya 48:6 “Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonyesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua.”
Mithali 22:19 Ili matumaini yako uyaweke kwa Bwana, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe.
KALENDA YA SHETANI
Tunakuelekea kule Galoni ya maji ya mwisho ya kuikomboa dunia itatoka kanisani, Umija wa mataifa hautaweza kuuzima moto huo, wewe unayeyasikia maneno haya umeandaliwa kwaajili ya siku za mwisho, mataifa yenye migogoro wewe ndiye utakayeenda kutatua migogoro yao, hiki ndicho kipindi ambacho watu waliiookoka walionekana kwamba wanalia lia lakini kipindi hicho kitakuwa na maajabu na miujiza ya kutisha kuliko kawaida.
Mpinga kristo atakapokuja atakuja kwaajili ya kuleta ufumbuzi wa migogoro duniani baina ya mataifa, atakuja kwa kusema kwamba anajua kinacholeta mgogoro duniani ni nini atawaambia waarabu tulieni atajua jinsi ya kuwatuliza, atawaambia wayahudi tulieni kwasababu atajua jinsi ya kuongea nao atajifanya kama myahudi ili wale wanaoamini uyahudi wamwamini, ataongea kiarabu ili waarabu wajue ni mwenzao na ataifanya dunia iwe amani kwenye kila idara, kwenye afya, siasa, uchumi, sheria n.k
Lakini wakati huyo mpinga kristo huyo ataamua ile alama ya 666 itatokea siku moja wale watu wanaomwabudu Bwana hawapo na huyu shetani Lucifer ataanza kuelezea kwamba watu wa Mungu ambao walikuwa wanahubiri injili walikuwa sio imara walikuwa wanauovu ndani yao dunia imewameza na sasa imebaki na wema tu sasa tuishi na kufurahia, kipindi hicho watu wote wataiwa raia wa dunia(ukifika kipindi hicho kama bado upo ujue ushaachwa)
alama hiyo kila mtu ataambiwa mtu awe nayo ili dunia nzina itulie kama taifa moja ambalo watu wake ni wamoja hawana ugomvi watu wanaoelewana na kupendana lakini huo utakuwa ni mpango wake ili aitawale dunia kama ilivyoandikwa atatuliza watu wote kwa muda wa miaka mitatu na nusu. Kipindi hicho ndicho kutakapokuwa na amani dunia nzima ili litimie andiko kwamba mtasikia amani amani hapo ndipo uharibifu utakapo kuja.

Baada ya kuwadanganya watu wakati huo kanisa litakuwa limeshanyakuliwa tayari Baada ya miaka mitatu na nusu itatokea vita ya Dunia "almagedon" ataamua kusema kwamba yeye ndiye mungu lakini Dunia nzima itamkubali na watakatifu tunaoitangaza injili ya Yesu na kuhubiri amani na Ufalme wa Mungu duniani watakuwa wameshanyakuliwa.
Kipindi hicho Dunia itakuwa kwenye kalenda ya dunia nzima kupigana na Israeli kwasababu Israeli atakataa kumkubali Mpinga kristo kama Mungu lakini hicho ndicho kipindi vita hivyo itaamuliwa na Yesu pale atakaposhuka kutokea mbinguni na kuwaangamiza wote watakaopigana na Israeli kwa upanga wa kinywani mwake. Kipindi kinakuja ambacho umoja wa mataifa hautaweza kusuluhisha mogogoro tena lakini kipindi hicho ndicho ambacho kanisa litasimama na kwenda kuamua migogoro kwenye mataifa yenye mogogoro kwa jina la Yesu.
Kipindi hiki ndicho kile kipindi ambacho watu wa Mungu tunaishi kwa imani, tukiitangaza injili hii yenye nguvu.
Zaburi 91:10 “Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.”
Kama Bwana asingekuwa pamoja nasi Israeli na aseme sasa, mtu yeyote akija na nia mbaya kwenye mlango wa nyumba yako nia mbaya ile nia haitatimia kwa jina la Yesu awe mtoto, mzee, ama mtu mzima au kijana ile nia mbaya itamrudia yeye kwa damu ya Yesu.
Ufunuo wa Yohana 6:6 “Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, Kibaba cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya shayiri kwa nusu rupia, wala usiyadhuru mafuta wala divai.”

Comments