“kalenda za kichawi(Sehemu ya nne)”

Na Askofu Dk Josephat Gwajima, Ufufuo na uzima.

Yeremia 25:11 “Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.”
Yeremia 29:10 “Maana Bwana asema hivi, Babeli utakapotimiziwa miaka sabini, nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa.”
Danieli 9:4-7 “Nikamwomba Bwana, Mungu wangu, nikaungama, nikasema, Ee Bwana, Mungu mkuu, mwenye kutisha, ashikaye maagano na rehema kwao wampendao, na kuzishika amri zake;tumefanya dhambi, tumefanya ukaidi, tumetenda maovu, tumeasi, naam, hata kwa kuyaacha maagizo yako na hukumu zako; wala hatukuwasikiliza watumishi wako, manabii, ambao kwa jina lako walisema na wafalme wetu, na wakuu wetu, na baba zetu, na watu wote wa nchi.Ee Bwana, haki ina wewe, lakini kwetu sisi kuna haya ya uso, kama hivi leo; kwa watu wa Yuda, na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kwa Israeli wote, walio karibu na hao walio mbali, katika nchi zote ulikowafukuza, kwa sababu ya makosa yao waliyokukosa.”
Mungu aliwambia wana wa Israeli wamemkosea hivyo wataenda utumwani, wakati wanachukuliwa kwenda utumwani kuna vijana wadogo walienda kule ambao ni akina Shadraka, na Meshaki, na Abednego, Danieli yeye alikuwa anasoma vitabu, wakati anasoma akafahamu kwamba miaka sabini ya wana wa Israeli kuwa utumwani imeshatimia, alipogundua hivyo Danieli akaanza kufunga na kuomba kumtafuta Mungu, Hapa tunajifunza kwamba Mungu akisema jambo juu yako usikae kimya kusubiri kwasababu amesema chukua nafasi yako. kwamfanoMungu akisema nitakubariki, nitakuinua, nitakusaidia, ni lazima ujue sehemu yako tanachotakiwa kufanya ili yale Mungu aliyoyasema juu yako yatimie kama Danieli alivyofanya.
Mambo ya Mungu huwa yanakwenda sawasawa na unavyoamini. Mnaweza kuwa watu wengi mmekusanyika pamoja mnapokea Baraka, lakini kila mtu akachukua sehemu yake sawa sawa na alivyoamini.
Amina ni kama mkono wa Rohoni kupokea Baraka kuwa Mungu, usiposema Amen halijawa lakwako, linakwenda hewani. Unapoambiwa kitu ukasema Amina maana yake hapo umepokea lile jambo ulichoambiwa, hata sheria za Mungu zinapokuwa zinatamkwa mwisho wake zinasema amina.
Imeandikwa:-

Kumbukumbu la Torati 27:16 Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
Kumbukumbu la Torati 27:15 “Na alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga, au ya kusubu, machukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi, akaisimamisha kwa siri. Na watu wote wajibu, waseme, Amina.”
Zaburi 106:48 Na ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Watu wote na waseme, Amina. Haleluya."
Mambo ya Mungu hayaendi kwa mazoea yanakwenda kwa Imani.
Sisi tumegundua mwaka 2017 ni mwaka wa kuinuliwa na Bwana ndiomaana tumeamua kufunga na kuomba, Danieli aliamua kusoma vitabu akagundua kalenda ya Mungu imeshatimia akaamua kufunga na kuomba.

“Yesu alipofufuka kulitokea uvumi kwamba amefufuka na wanafunzi wake walikuwa njiani wanaulizana kuhusu huo uvumi na yeye akaungana nao akiwauliza kuna nini ili ajue mawazo ya wanawaza nini. Mungu huwa hajitokezi mpaka ajue unamuwazia nini yeye, Yule mwanamke aliyekuwa anatokwa na damu alikuwa anamawazo ya kumgusa Yesu bila kutaka kitu kingine kwa Yesu, hakutaka aongee naye, hakutaka afarijiwe naye alitaka kushika pindo ya Yesu basin a kutokana ana mawazo yake na mtazamo wake Mungu alimponya na Yesu akajua kuna nguvu zimemtoka, amemponya mtu bila kupanga, amemponya mtu bila kunai na Yule mwanamke Biblia inasema damu yake ikakauka saa ileile, Leo hii mguse Yesu kwa namna ya tofauti na haja yako itatimia kwa jina la Yesu.”
Huyu Danieli alipoanza kufunga na kuomba na wakati akiwa anaomba Malaika akamtokta na kumgusa akamwambia nakupa akili upate kufahamu, Kumbe ukifunga na kuomba Mungu atakupa akili juu ya mambo unayoyataka kama ni Biashara utapata akili ya kufanya biashara,
Danieli9:21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni. Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.”
Wakati anaendelea Mungu akampa ratiba yake, Kalenda ya Mungu kwamba nini afanye na wakati gani. Danieli aliomba warudi nyumbani kwao lakini Mungu akamwambia atafanya haya kwa muda wa majuma sabini.
Danieli 9:24 “Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii, na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.”
Biblia ina tafsiri Mbili za nyakati
Hayo majuma sabini maana yake ni hii, Tafasiri ya kwanza ya Biblia siku moja ni sawa na miaka elfu na tafasiri ya pili ni siku moja ni sawasawa na miaka elfu moja.
Hesabu 14: 34 “Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu, ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu”
Wale wapelelezi waliporudi kutoa taarifa kwenye nchi ya ahadi walileta taarifa mbaya na Mungu akawaambia zile siku arobaini zitakuwa miaka arobaini ndiomaana wakatembea miaka aro baini kwenda kwenye nchi ya ahadi.
Ezekieli4: 6 Tena utakapozitimiza hizo, utalala kwa ubavu wako wa kuume, nawe utauchukua uovu wa nyumba ya Yuda; siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagizia.”
Hii ndiyo maana ya siku moja ni sawa mwaka mmoja.
Danieli 9:25 “Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kuujenga upya Yerusalemu hata zamani zake masihi aliye mkuu; kutakuwa na majuma saba; na katika majuma sitini na mawili utajengwa tena pamoja na njia kuu zake na handaki, naam, katika nyakati za taabu.”
Danieli aliambiwa atafanya kazi kwenye kalenda ya Mungu kwa majuma sabini. Yale majuma sabini Mungu ameanza kuyavunja vipande vipande, akamwambia kuanzia Mfalme yule atakaye waruhusu itakuwa majuma saba yaani saba mara saba ni miaka arobaini na tisa, na akamwongezea tena baada ya majuma sabini kutakuwa na majuma mengine sitini na mbili utajengwa ule mji lakini kwa wakati wa taabu, ndio kipindi kile wana wa Israeli walikuwa wanajenga huku mkono mmoja wamebeba silaha, haya mambo yalikuja kutokea tena.
Danieli 9:26 “Na baada ya yale majuma sitini na mawili, masihi atakatiliwa mbali, naye atakuwa hana kitu; na watu wa mkuu atakayekuja watauangamiza mji, na patakatifu; na mwisho wake utakuwa pamoja na gharika, na hata mwisho ule vita vitakuwapo; ukiwa umekwisha kukusudiwa.”
Danieli aliambiwa baada ya yale majuma sabini na mbili masihi atakatiliwa mbali. Huyu ambaye anaitwa masihi atakatiliwa mbali ni Yesu kristo na alipokuja Yesu yalitimia hayo maneno ambayo yamenenwa miaka mia nne arobaini na tano kabla Yesu hajazaliwa.
Danieli 9:27 “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.”
Ratiba ya Mungu ni sahihi, kwenye Biblia inasema shetani atafungwa miaka elfu moja kile kipindi cha milenia. Zipo kalenda za kiroho za Mungu ndiomaana kalenda ya Mungu ilisema Yesu atazaliwa akazaliwa, kalenda ikasema atakufa na kufufuka siku ya tatu akafa akafufuka siku ya tatu, akalenda ya Mungu ikasema atapaa kwenda mbinguni akapaa na kalenda ya Mungu imesema atarudi na kweli hakika atarudi. Hii ndiyo kalenda ya kiMungu ilivyo.
Kalenda ya Mpinga kristo nayo ipo vilevile.
2 Wathesalonike 2:7 “Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa.”
Mpinga kristo yupo duniani lakini yuko anayezuia asitende kazi asilimia miamoja, watu wa Mungu bado wapo duniani. Duniani wapo wanaoonekana ni Binadamu kumbe ni mashetani wanazuiwa hawatendi kazi kwasababu watu wa Mungu wapo duniani wanashindwa kujidhihirisha wazi kwasababu watu wa Mungu wanasali na kuomba duniani kote.
Kule Ulaya kwenye bunge la Umoja wa mataifa wanajiandaa kuanzisha kazi ya mpinga kristo ndani ya mfumo wa babiloni ili kuileta dunia mahali pamoja ikae watu wawe wanauraia mmoja waitwe raia wa ulimwengu, kipindi hicho cha mpinga kristo kile kinachopatikana marekani kitapatikana na mahali pengine Hautakuwa na haja ya kusafiri kukifata mpaka marekani,
Sasahivi watu hao wanajiandaa kumleta mpinga kristo kwa kuanzisha umoja wa mataifa ili mataifa yote yawe kitu kimoja, wanaandaa Marekani isiwe taifa lenye nguvu peke yake bali mataifa yote yawe sawa. Mfumo ule wa Babiloni bado upo baadaya ya kujaribiwa kwenye agano jipya Mungu akauharibu.
Leo hii watu wanaajiriwa kule wanatumika na baadaye wakizeeka wanapewa kiinua mgongo kidogo sana na hata ule mshahara wanapewa hautoshelezi.
Mungu akupe akili usiingie kwenye mfumo wa babilon uanzishe biashara yako ufanikiwe ili uende kokote unakotaka umtumikie Mungu akubariki, Mungu akupe akili ya kufanikiwa kwa jina la Yesu.
Dunia inaongozwa na watu wachache, watu hao ni mashetani ni viumbe wanaotokea chini(kuzimu) wanakuja duniani wanavaa miili lengo lao wanakuja duniani ili waitengeneze dunia kwenye mfumo wa kumilikiwa, wanasababisha matukio ili waweze kuwaongoza watu, mfano shehemu ya makutano wakitaka kujua kila mtu ana nini wanasababisha tukio la kulipua bomu ili weze kuweka mfumo wa kuwasachi kila mtu na lengo la kuwamiliki watu. Wametengeneza mfumo wa kutokuwa na amani ili wamiliki watu kwa staili hiyo.
Leo ukiwa unasafiri unakaguliwa kuliko maelezo kwasababu ya mfumo wa Babiloni uliotengenezwa.
Zipo Kalenda za kichawi juu yako ambazo zimetengenezwa na wachawi wanataka uwe kilema mwaka 2017, wamepanga ufilisike, wamepanga upatwe na matatizo uangamie lakini Mungu naye anayo kalenda yale itakusaidia ufanikiwe mwaka huu kwa jina la Yesu.
Haribu kalenda za kutawaliwa na mfumo wa babiloni, haribu kalenda za kichawi zilizopangwa juu yako kwa jina la Yesu.
“kwa jina la naahribu kalenda za kichawi kwenye maisha yangu, kwenye familia yangu kwa jina la Yesu, naharibu kalenda za kichawi kwenye kazi yangu kwa jina la Yesu, naharibu kalenda za kichawi zilizopangwa kwenye mibuyu, baharini, kutokea kwenye anga kwa jina la Yesu. (Endelea kuharibu kalenda za kichawi zilizopandwa juu yako mwaka huu mzima kwa jina la Yesu) Amen.

Comments