KUNA MAMBO/VITU LAZIMA VIFE AU UVIUE NDIPO UMUONE BWANA 2017


Bwana Yesu asifiwe Mtu wa Mungu,
Ninayofuraha kubwa kukuandikia ujumbe muhumu sana kwako,

Ujumbe huu ni ujumbe wangu maalumu wa MWAKA MPYA kwa ajili ya Kanisa la Mungu.
Nimeuandika leo tarehe 10/01/2017 kwa sababu ni siku yangu ya kuzaliwa, nimetimiza umri wa miaka 26
(Happy birthdate to me).

Na Mwl Nickson Mabena
Mwaka jana nilianzisha kampeni maalumu niliyoiita TUMFILISI SHETANI kampeni iliyoambatana na Masomo kadhaa yanayofundisha jinsi ya kumfilisi shetani..
Kulikuwa na mambo (Masomo) makuu mawili;
1.NUNUA BIBLIA NA UISOME
2.KUFUNGA NA KUOMBA.

Mwaka huu ninaanza na hili somo, ninamwamini Roho Mtakatifu atakufundisha kitu kikubwa kupitia ujumbe huu, kama ukiyaweka kwenye matendo utakayojifunza humu, hakika HUTABAKI WA KAWAIDA KABISA!.
Neno la Mungu linasema, *"Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwina Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu"* ISAYA 6:1
Isaya anasema Mfalme Uzia ALIPOKUFA alimwona BWANA!,
Nimekuja kugundua 'Mfalme' Uzia alikuwa kikwazo kwa Isaya asimuine Mungu kwenye maisha yake,
Ilibidi 'afe' kwanza ndipo amuone Bwana Yesu akijifunua kwa viwango vya juu kwenye maisha yake.
Nimekuja kugundua pia, hata kwako wewe Wapo wakina MFALME UZIA wengi kwenye maisha yake ndio maana kuna viwango unavyovitaka vya kumuona Mungu huvifikii, nimekuja kukwambia UZIA WAKO SIKU AKIFA NDIO UTAMUONA BWANA!.
Kama UZIA wako hataki kufa mwenyewe basi MUUE akishakufa UTAMUONA BWANA!
Unaweza ukajiuliza maswali, inamaana leo Mwalimu anatufundisha KUUA?, Je! Uzia ni nani?, kwa nini tumuue baba wa watu?
Jifunze polepole, utanielewa tu Mwana wa Mungu!
UZIA wako ni KITU CHOCHOTE KINACHOKUZUIA USIMUONE BWANA KWENYE MAISHA YAKO, au ni KIZUIZI CHA WEWE KUPIGA HATUA KWENYE MAISHA YA WOKOVU!.
Wakina Uzia wapo wengi sana wengine unawajua wengine huwajui, lakini kupitia ujumbe huu utawafahamu wakina UZIA wengine..
Nakupa kazi ya kuwatafuta ili uanze mikakati ya kuwaua ndani ya mwaka huu 2017!
Mfano,
Biblia inasema hivi, *"Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu"* WAKOLOSAI 3:5-6
Nayapenda maandiko hayo kwenye Biblia ya tafsiri ya Ulimwengu mpya,
Imeandikwa hivi, *"Kwa hiyo, fisheni viungo vya mwili wenu vilivyo juu ya dunia kwa habari ya uasherati, ukosefu wa usafi, hamu ya ngono, tamaa yenye kuumiza, na tamaa, ambako ni ibada ya sanamu. Kwa sababu ya mambo hayo hasira ya kisasi ya Mungu inakuja"* WAKOLOSAI 3:5-6
Kutokana na maandiko hayo, nina ujasiri wa kukwambia kwamba;
Kama kikwazo chako kwenye maisha yako ya Wokovu ni Tamaa ya Ngono, Mawazo Mabaya, Uasherati na Uzinzi, Uchafu, Kutamani, na mambo yanayofanana na hayo, basi dawa yake ni KUVIFISHA VIUNGO VYAKO!

Kwa hiyo, UZIA wako ni VIUNGO VYAKO hivyo huwezi kumuona Mungu hadi pale viungo vyako vitakapo kufa kwa habari ya Dhambi!.
Umenielewa?
Usikubali ukakwama kama ulivyokwama Mwaka ukiipita, Mwaka huu ni Mwaka Mwingine, LAZIMA 'UZIA' AFE, NASEMA TENA LAZIMA 'UZIA' AFE!!.
Kama wewe unataka kubaki palepale endelea tu hivyo hivyo, tunaotaka kwenda viwango vya JUU tunamsaka 'UZIA' popote alipo, na tunamuua!
Haiwezekani awe Kikwazo kwako na Bado unachekelea tu!.

Kwenye Mfululizo wa Masomo haya, utajifunza kidogo kidogo VITU/MAMBO YA KUYAUA ili umuone Mungu kwenye Maisha yako!
Kwenye utangulizi wa Somo nimekupa Mfano mmoja tu, KUVIFISHA VIUNGO VYAKO,
Chukua hatua Mpendwa, inawezekana ni vimekutesa kwa miaka mingi safari hii usikubali vikusumbue tena *PUT TO DEATH*.

Huu ni Ujumbe wangu wa Mwaka mpya 2017, Leo ikiwa ni Siku yangu ya Kuzaliwa HAPPY BIRTHDAY TO ME!.
VIFISHE VIUNGO VYAKO, UMUONE BWANA KWA VIWANGO VINGINE TUMFILISI SHETANI 2017!.
Nina imani kuna kitu umejifunza kupitia ujumbe huu, kama ni hivyo basi mshirikishe na Mtu Mwingine na yeye ajifunze!!.
Mungu akubariki sana, Yesu akuonekanie!.
Naishia hapo,
Mimi ni Kijana wako,
Naitwa,
Mwlm Nick
0712265856
(WhatsApp#)

Comments